Tukutane hapa wale tuliowahi "Kuchapiwa", ni kitu gani kilikuuma zaidi na ulichukua maamuzi gani kwa mwenzako?

Na mwanaume anaejielewaa kamwe USIJIBUU MSG ZA MWANAMKE ANAEKUPIGA KIBUTI.
 
Dada ake ungempiga paipu kawaida tu, mtungo labda mngempiga huyo mshkaji. Dada ulimuonea!
 
Mimi ilikuwa hivi nilikuwa na men wangu ni kisu yaani handsome balaa sasa siunajua lazima ukajishaue kwa marafiki zako .

Wakadai okay shem tumekuelewa walahi mtu akaiba namba yake akamsaoundisha wakalana sijajua kabadilika kwanini.
Nikawabana mafriends wangu waniambie weeh nikajua ni mke wamtu kafanya hilo na ndio best yangu kinyama .

Sawa nikasema poa ...
Nikaanza ufisadi hadi nikampata mume wake nikampa vizuri hadi basi akawa anapigwa tu wala hapendwi kisa mie akaona mapenzi na mchepuko ni mbaya akamwomba yule mkaka arudi kwangu na mimi nimuachie mumewe nikagoma kabisa.

Aliendaga kwao kapewa talaka moja akaaa mwaka 1 ndio nikaona nimuhurumie nikaachana mumewe wakarudiana

So alikaambali na mpenzi wangu japo sijarudiana naye
 
Eeeh kumbe hivi visasi na niny wadada mnavyo [emoji3064]

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mi Kuna Kuna manzi Tena wa kitaa kimoja nilikuwa namkubali sana ila kila nikimtongoza hakubali Wala hakatai, yupo kati kati baada ya mda kama miezi 6 hivi akakubali. Kumbe bwana, yule manzi wakati ananizungusha alikuwa ana boy mwingine ila aliniweka Mimi kama spare tyre. Nilivokuja kugundua akaniambia waliachana mda ila huyo msela bado anamsumbua halaf huyo msela ni malaya, mixer player na maneno yote ya shombo akamsalandia huyo mhuni. Mi nikawa najilia TU vinono kumbe baada ya kama miez 6 yule msela akarudisha majeshi Kwa yule manzi na yule manzi akawa anatuchanganya mi na yule muhuni, baadae yule msela akagundua bwana basi jioni Moja Sina Hili Wala Lile yule msela akanipigia Kwa simu ya manzi bas yule msela Wacha anitukane kuanzia Kwa kunipigia, Kwa sms ananitumia picha wapo wote uchi, mara wanajirekodi ili mradi TU wanirushe roho, mi uzuri nilishajuaga Kuwa tunakula wote na alikuwa mchepuko kwangu, nikawa mpole Ingawa iliniuma kishenzi maana msela aliniita mi mvamizi nimevamia coloni lake. Ila niliplay gentleman na manzi akaniandikia meseji ndeefu ya kibuti mixa mipasho na matusi, nikajibu TU haya Asante na kila la heri. Kwan hata mwez uliisha eti ananitext amemfuma boy wake na bestie yake laivu. Nikamwambia dada, we si uliniacha Kwa zarau,vijembe na matusi juu, pambana na Hal Yako na nikambloku kabisa kila sehem asinizoee. Sasa baada ya miaka 6 ana watoto wawili kila dogo na baba yake maisha yamemchapa Hadi uruma, Kuna siku akaja ofisin maana alikuwa anapajua na kuniomba msamaha labda nilimpa laana na mikosi nikamwambia hapana awe na amani TU ila kurudiana nae hapana hata Kwa bure. Mabinti wengi wana tamaa, mwisho wanaluka maji na kukanyaga Mafi na kuanza kujuta na ningejua nyiingi.
 
Kamwe usimrudie, ukafikiri ndio ataachana na huyo jamaa yake.

Sikio la kufa halisikii dawa, sanasana wote yeye na huyo jamaa yake watakuona boya sana na watakudharau kisha wataendeleza game zao.
 
"Message za kuchoma wakati wa kibuti". Niliandikiwa moja mwaka 2007, ilichoma mpaka basi, sikujibu hata text moja.

Nkatulia na maumivu yangu mpaka yakaja kupoa, maisha yakaendelea. 2010 anakuja na misamaha kibao. Nikamwambia kwa kuwa hakuna Guarantee kuwa hutoniandikia tena message kama ile siwezi kurudiana na wewe. Nimekusamehe roho safi lakini siwezi rudiana.

Leo kazalishwa watoto wawili, wote baba tofauti na ni Waume za watu wenye ndoa zao takatifu. Amebaki tu TikTok kutingisha bunyero
 
Mmmh upo vizuri kwa kweli
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…