Asante kwa jf humu tunaongea bila kujuana hata katika vitu ambavyo huwa hatupendi kuviweka wazi kama kuchapiwa maana ni aibu, humu hatujuani inakuwa rahisi kuweka mambo wazi...
kisa changu
Nilimuaga ex girlfriend wangu kwamba nimepata safari ya kikazi nitakua nje ya mji kwa muda flani kuna tajiri anataka nimwekee makabati nyumba anayofanyia finishing anyokaribia kuhamia, nilifika huko lakini nilikuta kuna wenzangu wengine kwa hio kazi iliisha mapema , niliwahi kurudi nikiwa nimeshalipwa na tajiri kama laki 3 hivi, nilifika kwangu kuweka begi na kisha nikaanza safari ya kwenda kwa ex wangu, nilifika kwake nilimkuta hayupo, nikaanza safari ya kurudi nikaona wacha nipate chakula lodge flani ya karibu,
wakati nakula wali kuku kwa jeuri ya pesa nilizopata huko kibaruani nikaona kuna gari rav 4 imekuja pale lodge ikapaki sehemu ambayo naweza kuiona, kuna jamaa alishuka akaingia ndani kwenye lodge nadhani alienda kuulizia chumba na kufanya malipo, mda huo nipo kwenye angle ya ku observe mengi, nikaona jamaa katoka nje karibu na mlango wa kuingia lodge katoa simu mfukoni anaitumia, itakuwa alikuwa anatuma mesej, baada ya sekunde chache kuna binti akashuka kwenye rav 4 kisha akaanza kumfata jamaa alipo, , LA HAULA!! Sikuamini macho yangu, alieshuka alikuwa ni dem wangu jamani.
nilipatwa na mshangao kumuona dem wangu japo yeye hakuweza kuniona, kiukweli alikuwa amependeza hio siku alienda saloon, nikawa siamini amini nachokiona, yani dem wangu kaingia lodge na hio njemba, , aaaaahhh!! maumivu makali mno!!
hata msosi ukageuka mchungu, nililipa na kuondoka hapo hapo,,, siwezi kuanzisha varanga kwa demu ambae kwa maamuzi yake kakubali kuliwa..
nilifika gheto nampigia lakini simu inaita tu, hapa nikawa navuta picha game imeiva, huo moto anaopelekewa huko si wa kitoto, niliumia sana kwakweli..
nilienda pharmacy ya karibu kununua sleeping pills (vidonge vya usingizi) maana mawazo yalinisonga sana, nilirudi geto nikagonga vidonge viwili nikajilaza kitandani huku naendelea kuwaza lakini usingizi ukanichukua.
kesho yake naamka kama kawaida ila daah!! nikikumbuka kilichotokea jana yani maumivu tu, nikacheki simu nikaona ex alinipigia kama mara tatu hivi na kuacha mesej kwamba alikuwa kanipigia sipokei, ila muda alionipigia hapo nilicheki ilikuwa ni baada ya masaa mawili na nusu hivi.
nilimwambia aje geto, ile kafika akaanza kujifanya kamaindi sikupokea simu alizopiga akaanza ku act kujifanya alikuwa kapatwa wasi wasi kudhani labda nilipatwa na tatizo, hapo hapo akaanza kujifanya anajichekesha kufurahi nimewahi kurudi na kanimisi sana, mimi namchora tu.
nikaanza kumpiga maswali pale moja kwa moja kwamba jana alieshuka nae kwenye rav 4 ni nani,, akaanza kama kujistukia hivi akawa anakazia kwamba alikuwa kwake labda nimemfananisha,,, nilimnasa kibao taaa!!! cha nguvu ili ajue nipo seriois,, akaanza kulia, nilimkazia ajibu swali hayo machozi yake hata ajaze ndoo nahitaji majibu, akawa anaendelea ubishi kusingizia namuonea na kwamba sio yeye, nilimnasa tena vibao vingine viwili vya nguvu zaidi na vilisikika aisee... akaanza kukiri kweli ni yeye na kuniomba msamaha kwamba hatarudia, haikuwa nia yake, bla bla bla,,,,, nilifungua mlango nikamwambia its over!, hatuwezi kuendelea ....
Ilikuwa shughuli nyingine kuanza kumtoa, alipiga sana magoti kuniomba msamaha, namuinua asimame yeye anapiga magoti na kunukamata miguu, ilibidi nguvu ya ziada itumike sambamba na vibao vitatu vya zaida, alijifuta futa machozi, nikamtoa mpaka getini nikafunga geti nikarudi chumbani kwangu, uzuri siku hio nilikuwa mpangaji peke yangu niliebaki.
nilikuwa na maumivu mengi moyoni lakini kwenda kazini na mazoezi kulisaidia kimtindo, sikutaka kujifungia ndani,,,maumivu yalikuwepo pindi muda wa kulala ukifika nikianza kuwaza nilivyochapiwa, daaah!! yani nikaanza kuwaza jinsi ex alivyokuwa anapelekewa moto kuna siku nilitoa chozi kama mtoto mdogo. hali hii ilidumu kwa wiki hivi ila baada ya hapo niliweza kupata nguvu ya ku-move on mdogo mdogo.
baada ya miezi miwili niliweza kujitosa upya kuanza mahusiani mapya, mahusiano mapya yalinisaidia kwa kiasi kikubwa kupooza maumivu na hatimae nikasahau kabisa.
KISASI::
Kwa sasa huyo jamaa alienichapia ndie aliemuoa ex wangu lakini cha ajabu mpaka leo ex wangu ni kama analazimisha mawasiliano, huwa hapitwi kunitumia mesej za pasaka njema, idi njema, n.k. ila namjua kabisa anachotaka ni ukaribu tu, kuna siku nilikutana nae nikampanga twende kwangu alikubali kabisa na nilipanga nimtafune nilipize kisasi kwa huyo jamaa alienichapia na hata nipige picha au video nimtumie ili nae aumie lakini nafsi ilisita, nilahirisha na kumwambia ex lakini ajabu yeye alijaribu kunibembeleza twende akijua kabisa kinachoweza kutokea lakini nilisimamia msimamo wangu nikazuga tutapanga siku nyingine,,, ni kwamba huyu ex mda wowote nikimtaka anaweza kunipa mzigo lakini sioni ambacho ntafaidika nacho, nimekubali yaishe tu maisha yaendelee.