Tulia Ackson aache upotoshaji, Kiti cha Naibu Spika kiko wazi kikatiba

Tulia Ackson aache upotoshaji, Kiti cha Naibu Spika kiko wazi kikatiba

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Hoja ya Naibu spika Dr. Tulia inasimama kwenye maneno mafupi anayoyachagua bila kumaliza yote katika Ibara ya 84(2) ya katiba. Maneno aliyoyachagua katika Ibara hiyo haijatoa katazo la moja kwa moja kwa Naibu spika kugombea Uspika. Waliokatazwa kwakutaja moja kwa moja ni Waziri au Naibu waziri lakini ibara hiyohiyo ina maneno mengine ili ikamilike, ambayo yanazuia watu wengine kugombea uspika kwakutumia maneno yasemayo, "..........au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya Ibara hiyo, huyu ndio hataweza kuchaguliwa kuwa Spika".

Dr. Tulia ni mwanasheria anatumia udhaifu wa Watanzania wachache na hasa Wabunge wenzake waliowengi ambao ni mbumbumbu wa Sheria anawarubuni kuwa Katiba ya Tanzania haijamzuia yeye Naibu Spika kugombea Uspika. Hivyo anaamua kutojiuzulu kwanza Unaibu Spika ndipo agombee, badala yake anaamua kwenda navyo pacha.

Dr. Tulia anajenga hoja kwamba hakuna sheria ya Bunge inayomzuia. Lakini kikatiba ni kwamba, kwa kuwa hakuna sheria iliyotungwa na Bunge kumzuia Naibu Spika kuchaguliwa kuwa Spika, ni wazi kuwa Kisheria tunalazimika kuitumia Katiba kuwa sheria kwakuwa Katiba ni sheria MAMA. Sasa kwa Mujibu wa Ibara ya 84 (2) inayosema waliokatazwa ni Waziri au Naibu waziri au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa madhumuni ya Ibara hiyo. Maneno ya kikatiba kwamba "au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote itakayotajwa na sheria.....", yana nguvu za kisheria.

Baada ya hapo turejee kwenye katiba, cheo cha Naibu Spika kinatambuliwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ibara ya 85 (1). Isemayo, 85.-(1) Kutakuwa na Naibu wa Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge.

Hivyo ndio kusema kinatambuliwa Katiba ambayo ni sheria MAMA, na kwahivyo, Naibu Spika anaingia kwenye kundi la wanaokatazwa kugombea Uspika kupitia Ibara ya 84 (2) kwa maneno ya kikatiba yasemayo "au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote itakayotajwa na sheria....."

Kuna athari nyingi za kisheria, kimantiki na kimaslahi ikiwa Naibu Spika ataachwa aendelee na mchakato wa kugombea Uspika,

1. Ni wakati gani Naibu Spika ataachia kiti chake ili kujinadi na kupigiwa kura kuwa Spika?

2. Je wakati anaomba kura na zoezi la kura likiwa linaendelea je ataendelea kuwa Naibu Spika?

3. Iwapo Naibu spika aamue kutokujihuzulu wakati wa mchakato wa kura mpaka matokeo kutangazwa na akashinda, maana yake ni kwamba, kwa vyovyote vile kuna muda walau hata wa dakika moja atakuwa ameshika vyeo vyote viwili kwa pamoja.

4. Mchakato hauwezi kuwa huru sana, hata kuanzia kwenye chama chake kwa kuwa watalazimika kujadili intergrity ya mtu ambaye bado ni kiongozi, je implication ya chama chake au bunge kutompitisha ni yapi?

Ukisoma ibara ya 85(4) a to c, zimeelezea events za Naibu speaker kupoteza mamlaka yake. Kitendo cha yeye kuchukua fomu kugombea U-Speaker, it means kinamfanya apoteze mamlaka yake ya Unaibu Speaker chini ya Ibara ya 85(4)(b).

Wako wanaodhani kuwa kwakuwa kachukua fomu tu kwenye Chama chake basi hajavunja sheria ambayo ndio Katiba, hadi angalau apitishwe na chama chake ndio anaweza kujiuzulu. Nooo mchakato wa Kugombea kisheria na Kikatiba unaanzia pale dakika ya kwanza unapochukua fomu tu kwenye chama chako.

Ukweli unabaki kuwa, Mamlaka ya Speaker & Deputy Speaker yamewekwa na Katiba ya JMT.
Under common Jurisprudence ya Katiba ya Tanzania haiwezekani mtu mmoja kushikiria hizi mamlaka 2 kwa wakati mmoja. Hata kwa sekunde moja tu.

Ikitokea Tulia akapata U Speaker, automatically anakua ni Speaker na Naibu Speaker at the same time, this is Constitutional breach. She is supposed to resign her current position in order to be eligible to contest nafasi ya U- Speaker.

Ili kuelewa zaidi Msimamo wa Kikatiba na Kisheria, Soma kwa Construction approach kwa pamoja Vifungu vifauatavyo;

1. Ibara ya 84 Katiba.

2. Ibara ya 85(1&2) Katiba.

3. Kif.41(2) Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

4. Ibara 149(1)(c) Katiba.

Swali la kujiuliza ni Je, Kujiuzulu kwa Spika Ndugai kumefuta na Naibu wake Tulia Ackson automatically?

Kama Tulia hajafutiwa madaraka yake, je anagombeaje nafasi ya Spika wakati yeye kwa sasa ndiye anakaimu nafasi ya Spika kwa Kifungu cha 41 cha Sheria ya Madaraka ya Bunge.

Na Yericko Nyerere


Screenshot_20220113-092612.png

Screenshot_20220114-102927.png
 
Sijui kwanini watu hawajitokezi kuchukua form ya kugombea Unaibu Spika wakati sheria ziko wazi, au tatizo mgombea ili ashinde lazima awe na DNA ya CCM ndio maana watu wa nje wanaogopa kuchukua form, na CCM wenyewe wako kimya kwasababu wameshazoea kuvunja sheria.
 
Lakini pia kimgongano tu na kibinadamu hivi tuchukulie akipitishwa na chama chake akagombea alafu akashindwa wakati wa actual uchaguzi bungeni ( Ofcoz kwa ccm ilivyo ni ngumu) ataendelea unaibu wake maana hajajiuzulu sasa atafanyaje kazi na spika mpya kibinadamu?
 
Hoja ya Naibu spika Dr. Tulia inasimama kwenye maneno mafupi anayoyachagua bila kumaliza yote katika Ibara ya 84(2) ya katiba. Maneno aliyoyachagua katika Ibara hiyo haijatoa katazo la moja kwa moja kwa Naibu spika kugombea Uspika. Waliokatazwa kwakutaja moja kwa moja ni Waziri au Naibu waziri lakini ibara hiyohiyo ina maneno mengine ili ikamilike, ambayo yanazuia watu wengine kugombea uspika kwakutumia maneno
Ikitokea Bi Mdash kajiuzulu unaibu na atakaim nafas ya mgogo
 
Hoja ya Naibu spika Dr. Tulia inasimama kwenye maneno mafupi anayoyachagua bila kumaliza yote katika Ibara ya 84(2) ya katiba. Maneno
Haiwezekani mtu anavunja katiba na anaachwa tu na wanasheria wapo na chama chao kimekaa kimya.

Tabia hii ya kuwaacha hawa waarifu wa kikatiba ndio inafanya tuwe laugh stock of East Africa,mko wapi wanasheria?

Pelekeni hii kesi mahakamani ASAP!
 
Back
Top Bottom