Hamjambo Walimwengu!
1. Kuna wale watu ambao hupotosha na kuwaweka watu under the Cage, kwamba mtu hatakiwi kujipost akiwa na furaha au akifurahia. Jambo ambalo sisi Watibeli tunapingana nalo kwa nguvu zote
2. Sio kwamba hatujui kwamba kuna watu wenye wivu, tunajua
Sio kwamba hatujui watu wabaya wenye husda na chuki. Tunajua.
3. Lakini Sisi Watibeli hatutishwi wala kuendeshwa wala kupangiwa na nguvu za giza, watu wenye nguvu hasi hawawezi kutuzuiia kufurahia na kuonyesha furaha zetu.
4. Tunajua tunaishi mara moja. Na safari hii ya maisha ni fupi.
5. Tulia Ackson pamoja na madhaifu yake lakini moja ya ubora wake ni kujua kuishi. Maisha ayapendayo to the fullest
6. Kuna Wakati hasimu wake walimfananisha na Kikatuni Fulani maarufu Kama RANGO. Na walimuita RANGO Moja ya Animation maarufu duniani.
7. Sikuwahi kujua mtazamo wake anapopitia maoni na watu kumuita RANGO. Lakini leo kapost Picha ya RANGO Mwenyewe.
8. Binafsi nilijikuta ninacheka, nimefurahi sana na imenipa mwanga anachukuliaje jina hilo.
Rango kimaudhui alipewa dhamana kubwa katika animation hiyo iliyosheheni sanaa na maudhui ya ukombozi.
9. Rango Kama Mtetezi wa wanyonge,
Rango kama mtatuzi wa changamoto za jamii. Ndio dhamira kuu mbili alizozibabe Rango katika filamu Ile.
10. Tulia Ackson life style yake watu wengi wanaipenda. Tatizo kubwa ni kuwa Wengi wapo under the Cage, wengi wamepotoshwa, wengi Wana fikira potofu.
11. Kwamba hutakiwi kujipost, hutakiwi kuonyesha furaha yako.
Hutakiwi kutoa maoni na kujieleza.
Kwa Sehemu kubwa watu wengi wanamitazamo hiyo.
12. Lakini waliombele ya wakati wanajua dhana na mitazamo hiyo ni potofu.
13. Watu kama Tulia husaidia kuonyesha njia pasipo na njia kwa kuwapa Uhuru wale ambao hutamani kufurahia maisha yao kwa kile kidogo walichonacho lakini wapo under za cage,
14. Nimeona pia baadhi ya Watumishi wakijipost wakifurahia maisha. Mamia ya watu huumizwa, hutukana, hulia. Kana kwamba kupost na kufurahia maisha ni dhambi au ni kuvunja Sheria.
15. Hii yote kitaalam inaonyesha bado watu wengi wanaukungu kwenye fikra zao. Wanamawazo hasi, wivu na chuki
16. Kutotaka kuona wengine wakifurahia maisha ni uchawi, NI husda na wengi wenye tabia hiyo hujikuta wakiwa na misongo ya mawazo, familia zisizo na furaha, kushindwa kimahusiano.
17. Nilimuona IPM na mkewe wakifurahia Maisha kama Familia. Wakileta Utani.
Mamia ya Watu walichukizwa na kulia, wakilalama, wakitukana.
Unajiuliza IPM na mkewe wamekosea wapi?
18. Unagundua ni Chuki, husda, mioyo yenye nguvu za Giza, broken people, Losers, walioshindwa, waliofeli.
Ndio wengi hujikuta hawapendi maendeleo n wengine wakifurahia.
19. Wengine wanasema ushamba, Mtu kujipost anafurahia maisha yake kwako unaona ushamba, ujanja kwako ni upi? Unagundua wengi wenye mitazamo ya kutotaka kuona wengine wanafurahia na kuonyesha mafanikio na furaha wengi ndio Washamba na wenye roho za kwa nini, watu wasio na shukrani, wasiojua Maisha ni kitu gani.
20. Hujamuibia mtu, hujamdhulumu mtu, hujala cha mtu. Kwa mini uhofie kufurahia maisha?
Ukiwa jizi, ukiwa mwovu unayohaki ya kujificha na kuchekelea chooni.
21. Lakini pia kama sio tabia yako, usizuie mkeo na watoto kama hauna sababu za msingi. Maisha ni hayahaya.
22. Privacy ipo kwenye njia za mafanikio, mipango, mbinu, lakini sio kwenye mafanikio yenyewe.
23. Utaficha mindinyo, style za chumbani, lakini Mimba na mtoto huwezi ficha.
24. Mwisho wenye chuki waendelee kuwa na chuki.
Wasiopenda wengine wakifurahia waendelee kukosa furaha.
Wenye husda na hasidi waendelee kuwa mkia wakiona wengine wakibarikiwa.
25. Siku zote Taa huwekwa juu ya kianga sio uvunguni.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa SASA Dar es salaam