The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU), Tulia Ackson, amewataka wajumbe kumheshimu wakati wa mkutano wa Bunge uliofanyika Geneva siku ya Jumatatu Oktoba 14, 2024.
Mvutano ulianza baada ya Artur Gerasimov, mwakilishi wa Ukraine, kuomba "ripoti kamili ya mchakato" wa mkutano wake na kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, na aliuliza ikiwa maazimio ya IPU kuhusu "uchokozi wa Urusi" yalijadiliwa.
"Nataka sote tukumbuke kuwa hili lilitokea siku chache tu baada ya makombora ya Urusi kuharibu hospitali maarufu ya watoto huko Kiev," alisema Gerasimov, huku mwakilishi wa Canada pia akiunga mkono wito wa majibu.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Gerasimov alijaribu mara kadhaa kumkatiza na kuchukua tena nafasi ya kuzungumza, kabla ya Tulia kumwambia: "Umeshazungumza, ulipata nafasi ya kuzungumza hapa. Nipe, niachie muda kwanza kulihutubia baraza kuu, nijibu masuala yaliyotolewa kisha turudi kwenye ajenda."
Ziara hiyo, aliendelea kusema, ilipaswa kuanza na Ukraine. "Ukraine ilijibu siku tuliyokuwa tayari kuwatembelea, [kwamba] Bw. Zelensky na Spika wangekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa NATO. Ningewazuia? Hapana, isingekuwa busara, na kwa hali yoyote sina mamlaka hayo," Dkt. Tulia aliendelea kusema.
Pia Dkt. Tulia aliongeza kuwa hakuna atakayemzuia kuhudhuria Mkutano wa BRICS wiki ijayo huko Urusi.
Pia, soma: