Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin

Hali imekuwa si Hali huko IPU wakati Rais wake Dk Tulia alipokutana na maswali magumu ikiwepo nani alimpa ruhusa ya kwenda Russia kabla ya kwenda Ukraine.

Maswali mengine ni Kwa nini hajaenda Gaza badala yake akaenda Israel?

Akijibu maswali hayo ameonesha kuwashangaa Wabunge wake vilaza Wazungu ambao hawajui dhima ya IPU na hawafuatilii ziara za Rais wao.
View attachment 3126291

My Take
Kuwa tempared na Unaongea kizungu hakuleti ukakasi kama kwa Kiswahili.

Dk.Tulia ajifunze kuzuia hasira zake vinginevyo atakuja kutoa kubwa kuliko maana Wazungu lazima waweke fitina Kwa sababu za mambo Yao.πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://youtu.be/qLdmO5Ou0rU?si=bjwbMFi78ASMFVMP

Ila amejibu vizuri sana, ametuheshimisha
 
Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU), Tulia Ackson, amewataka wajumbe kumheshimu wakati wa mkutano wa Bunge uliofanyika Geneva siku ya Jumatatu Oktoba 14, 2024.

Mvutano ulianza baada ya Artur Gerasimov, mwakilishi wa Ukraine, kuomba "ripoti kamili ya mchakato" wa mkutano wake na kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, na aliuliza ikiwa maazimio ya IPU kuhusu "uchokozi wa Urusi" yalijadiliwa.

"Nataka sote tukumbuke kuwa hili lilitokea siku chache tu baada ya makombora ya Urusi kuharibu hospitali maarufu ya watoto huko Kiev," alisema Gerasimov, huku mwakilishi wa Canada pia akiunga mkono wito wa majibu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Gerasimov alijaribu mara kadhaa kumkatiza na kuchukua tena nafasi ya kuzungumza, kabla ya Tulia kumwambia: "Umeshazungumza, ulipata nafasi ya kuzungumza hapa. Nipe, niachie muda kwanza kulihutubia baraza kuu, nijibu masuala yaliyotolewa kisha turudi kwenye ajenda."

Ziara hiyo, aliendelea kusema, ilipaswa kuanza na Ukraine. "Ukraine ilijibu siku tuliyokuwa tayari kuwatembelea, [kwamba] Bw. Zelensky na Spika wangekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa NATO. Ningewazuia? Hapana, isingekuwa busara, na kwa hali yoyote sina mamlaka hayo," Dkt. Tulia aliendelea kusema.

Pia Dkt. Tulia aliongeza kuwa hakuna atakayemzuia kuhudhuria Mkutano wa BRICS wiki ijayo huko Urusi.

Pia, soma:
Mnyakyusa kacharuka!!
 
Ukifuatilia historia ya kuanzishwa kwa IPU yaani manifesto kutoka kwa William Randal Cremer pamoja na FrΓ©dΓ©ric Passy utakuja kuona msingi mzuri wa hoja hujibiwa na hoja sio jazba.
Wabunge waliopo kwenye bunge la IPU sio wabunge wa CCM wala Chama au Mlengo mmoja bali ni mchanganyiko wa wabunge. Tulia atulie na afanye mambo kwa utaratibu na kanuni za IPU sio za Dodoma! Hao jamaa kukuondoa hapo kitini ni kitendo cha haraka sana!
 
Toka akiwa mwalimu wangu wa Sheria, na hadi sasa, ninaukubali uwezo wake wa kujieleza na kuzungumza Kiingereza kwa umahiri kabisa.

Hongera sana (Mwaisa) Tulia Ackson Mwansasu (LL.B., LL.M., PhD)
[/QUOTE
Mwaisa ni mwanamke sio mwanamke
 
Wabongo mkiona mwenzenu anaongea kiingereza vizuri mnaona anaakili sana. Hamuangalii kilichoongelewa na namna kilivyoongelewa.

Binafsi hata kazini kwangu naonekana genius sana maana ninajua vizuri Kiingereza.

Bongo raha sana
Pole
 
Kumbe ni lugha tu kama lugha zingine, watu wanataka utendaji kazi, huyu ajuza hata kaa asahau, Ulaya hakuna upumbavu wakuitana Mheshimiwa sijui mama mitano tena, kule ni kazi kazi
 
Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU), Tulia Ackson, amewataka wajumbe kumheshimu wakati wa mkutano wa Bunge uliofanyika Geneva siku ya Jumatatu Oktoba 14, 2024.

Mvutano ulianza baada ya Artur Gerasimov, mwakilishi wa Ukraine, kuomba "ripoti kamili ya mchakato" wa mkutano wake na kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, na aliuliza ikiwa maazimio ya IPU kuhusu "uchokozi wa Urusi" yalijadiliwa.

"Nataka sote tukumbuke kuwa hili lilitokea siku chache tu baada ya makombora ya Urusi kuharibu hospitali maarufu ya watoto huko Kiev," alisema Gerasimov, huku mwakilishi wa Canada pia akiunga mkono wito wa majibu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Gerasimov alijaribu mara kadhaa kumkatiza na kuchukua tena nafasi ya kuzungumza, kabla ya Tulia kumwambia: "Umeshazungumza, ulipata nafasi ya kuzungumza hapa. Nipe, niachie muda kwanza kulihutubia baraza kuu, nijibu masuala yaliyotolewa kisha turudi kwenye ajenda."

Ziara hiyo, aliendelea kusema, ilipaswa kuanza na Ukraine. "Ukraine ilijibu siku tuliyokuwa tayari kuwatembelea, [kwamba] Bw. Zelensky na Spika wangekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa NATO. Ningewazuia? Hapana, isingekuwa busara, na kwa hali yoyote sina mamlaka hayo," Dkt. Tulia aliendelea kusema.

Pia Dkt. Tulia aliongeza kuwa hakuna atakayemzuia kuhudhuria Mkutano wa BRICS wiki ijayo huko Urusi.

Pia, soma:
Rais wa IPu awafukuze hao wabunge watovu wa nidhamu waondoke kikaoni.
 
Back
Top Bottom