Tulia Ackson: CCM haitoachia Dola KAMWE

Tulia Ackson: CCM haitoachia Dola KAMWE

Hapo ndipo napojpendea ccm, ukweli unasemwa hataa jwa lugha ngumu. CCM haitoachia dola hata siku moja. Ambae anaona hawezi kuishi chini ya CCM atafute nchi ya kwenda
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa hakuna siku itatokea chama hicho kikaruhusu nafasi ya kuachia kuitawala nchi kwakuwa imejiwekea mizizi imara katika kuwatumikia wananchi wake.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Februari 4, 2023 akiwa Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kichama ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya Chama hicho iliyofanyika katika Mkoa wa kusini Unguja.

Amesema kuwa ni wakati sahihi kwa wanachama wa chama hicho hususani vijana kuendelea kukipigania na kuwapigania Viongozi wao wakuu akiwemo Mwenyekiti wa Chama taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuyasemea mazuri anayoyafanya kwa nchi.

“Mwana CCM hupaswi kukaa kinyonge hata siku moja, kote Tanzania bara na visiwani kuna miradi ya ujenzi wa shule kila kona, miundombinu ya barabara, zahanati, vituo vya afya n.k haya yote ni mafanikio ya kujivunia sasa unakaaje kinyonge? tunaposema kwamba chama hiki hakitaachia dola tunamaanisha” Amesisitiza Dkt. Tulia.

Chanzo: Clouds Media

Uyu naye arudi tu nyumbani kwao Rwanda, Mnyakyusa gani mwembamba namna hiyo!
 
Naunga mkono hoja.
Kuna watu tukiwaambia ukweli kuhusu CCM kutawala milele, hawaamini, na kwa vile maneno hayo ameyasema Tulia, bado kuna watu hawataamini hadi maneno hayo ya CCM kutawala milele Tanzania, yatakaposemwa na nanilii!. Sii wengi wanaojua kuwa kauli huumba, ila pia ukitoa kauli mbaya kama kuwatukana wazazi, kauli hiyo inasababisha one to be cursed!. Kauli kama hii ya CCM kutawala milele huko nyuma iliwahi kutolewa na kiongozi fulani who, very unfortunately, he was cursed!. Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. humo nilisema "Wanabodi,

Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga blah blah tuu, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah tuu, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton's laws of motion, ile kanuni ya "a body in motion" or

" a static body", itaendelea kubaki hivyo hivyo milele, hadi kutokea nguvu nyingine itakayoibadilisha, hivyo kwa hali hii ilivyo sasa, CCM is the body in motion, itaendelea kutawala milele, kwa sababu watu wenye uwezo wa Kimungu, wameishaona kuwa kwa Tanzania, hakuna kabisa uwezekano wa kutokea nguvu nyingine ya kuizuia CCM isitawale milele nchi yetu ya Tanzania, hivyo CCM, itatawala milele!.

Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM kama chama, ina mwanzo hivyo ni lazima nayo iwe na mwisho, unless CCM ndie Mungu mwenyewe, ambaye Yeye ndiye Pekee Alfa na Omega hivyo CCM hii iliyopo sasa nayo ni CCM Alfa na Omega, haina mwisho, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kuitawala Tanzania milele!, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote, tuupokee, tuukubali na tuutekeleze. Wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli kabisa watapata taabu sana!.

Jee Umilele wa CCM Kutawala Tanzania Milele, Unatokana na Nini?.

Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu wa CCM (not Mungu Baba) kuiteua CCM na kuipatia hati miliki ya kuitawala Tanzania milele na milele, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM.

Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
NB: Baadhi ya kauli kama hizi, zinasababisha curses, msije kushangaa watoa kauli kama hizi kuja kuwa cursed na kuchomoka kabla ya wakati kwa sababu neno milele ni mamlaka ya Mungu mwenyewe!.

Kidumu Milele Chama Cha Mapinduzi.
Pasco"

P
Mkuu Mayalla aka Njaa, pale Zanzibar, ccm huwa inashinda au inatangazwa kushinda!? Je, ule alioendesha mkono wa chuma JPM 2020 ni uchaguzi au uchafuzi!? Kwa kuwa upinzani haujajipanga kama unavyodai na ccm inakubalika sana na wananchi, huoni ni vyema wakiweka mazingira ya level playing field ili wathibitishe ubora wao!?
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa hakuna siku itatokea chama hicho kikaruhusu nafasi ya kuachia kuitawala nchi kwakuwa imejiwekea mizizi imara katika kuwatumikia wananchi wake.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Februari 4, 2023 akiwa Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kichama ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya Chama hicho iliyofanyika katika Mkoa wa kusini Unguja.

Amesema kuwa ni wakati sahihi kwa wanachama wa chama hicho hususani vijana kuendelea kukipigania na kuwapigania Viongozi wao wakuu akiwemo Mwenyekiti wa Chama taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuyasemea mazuri anayoyafanya kwa nchi.

“Mwana CCM hupaswi kukaa kinyonge hata siku moja, kote Tanzania bara na visiwani kuna miradi ya ujenzi wa shule kila kona, miundombinu ya barabara, zahanati, vituo vya afya n.k haya yote ni mafanikio ya kujivunia sasa unakaaje kinyonge? tunaposema kwamba chama hiki hakitaachia dola tunamaanisha” Amesisitiza Dkt. Tulia.

Chanzo: Clouds Media

Sisi wananchi ndio tutakaoamua kuiondoa CCM madarakani nje ya box la kura,Maana tunakuwa kwenye kura ndipo mnapotuibia. Kwakuwa tangu 2005 hamjawahi kushinda uchaguzi kihalali.
 
Mkuu Mayalla, pale Zanzibar, ccm huwa inashinda au inatangazwa kushinda!?
Hili nimeisha lisema humu Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
Je, ule alioendesha mkono wa chuma JPM 2020 ni uchaguzi au uchafuzi!?
Uchaguzi wa 2020 niliisha usema humu Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? nilisema
Wanabodi.

Kwa maoni yangu, 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, kutakuwa tuu na igizo la uchaguzi, na kwenye ubunge na udiwani , kwa udikiteta huu, sijui kama kuna mpinzani atatoka!, uchaguzi wa 2020 itakuwa ni uchaguzi wa CCM only and only CCM!. Uchaguzi mwingine wa rais na uchaguzi wa vyama vingi ni uchaguzi wa 2025 only if ...(Mungu hatafanya yake hapa katikati)

Paskali
Kwa kuwa upinzani haujajipanga kama unavyodai na ccm inakubalika sana na wananchi, huoni ni vyema wakiweka mazingira ya level playing field ili wathibitishe ubora wao!?
Hiki ndicho anachokifanya Mama Samia, atabadili katiba, sheria, ataleta tume huru ya uchaguzi na bado 2025 ni CCM pekee!.
P
 
Hili nimeisha lisema humu Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Uchaguzi wa 2020 niliisha usema humu Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? nilisema

Hiki ndicho anachokifanya Mama Samia, atabadili katiba, sheria, ataleta tume huru ya uchaguzi na bado 2025 ni CCM pekee!.
P
Hiyo ni kitu iko wazi ,siasa za upinzani nchi hili zilimulikwa na majina ya akina Lema na Mbowe na wameshindwa kupeleka siasa husika maeneo mengine ya nchi
 
Nebukadneza alifedheheshwa akala majani akasahaulika sehmbuse CCM? Wajitapa tu mwisho wa siku watajuta
 
Wapinzani halisi wa CCM watatoka ndani ya CCM,,tofauti na hapo tunajilisha upepo
 
Back
Top Bottom