Tulia Ackson: Naagiza Serikali ifanye utafiti wa Mapungufu ya Sheria ya Ushoga na Usagaji ili iendane na uhalisia wa sasa

Haya mambo kwa tamaduni zetu ni marufuku hata kuziongelea...
 
Nchi hii ni masikini wa kutupwa ,mnaanza kupambana na city ambavyo hamuwezi kuvizuia
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 6 leo Aprili 13, 2023 jijini Dodoma.

SERIKALI YAAGIZA NHIF ITOE KIBALI MATUMIZI YA CT SCAN HOSPITALI YA IRINGA
Agizo hilo limetolewa baada Mbunge Jesca Msambatavangu kuhoji Bungeni sababu za wagonjwa wanaotumia Bima ya NHIF katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kutopewa kibali kutumia kadi zao kupata huduma ya CT Scan.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema “Namuagiza DG wa Bima kwamba mpaka kesho saa mbili asubuhi (Aprili 14, 2023) watu wanaostahili na waliotimiza vigezo waanze kupata huduma hiyo.”

MWONGOZO KUHUSU MASUALA YA USHOGA NA USAGAJI NCHINI
Akitumia kanuni ya 76, Mbunge Noah Saputu ameomba mwongozo unaotaka Bunge litoe msimamo wake kuhusu suala la ushoga kwa kuwa Mamlaka zote za Nchi ikiwemo Rais Samia, viongozi wa dini pamoja na taasisi zingine kubwa zimetoa msimamo wa kutokuafikiana na jambo hilo.

Ameomba Muswada utakaoleta Sheria kali uletwe Bungeni haraka ili Bunge liupitishe.

Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson amesema hoja hiyo imeibuka baada ya hotuba ya Waziri Mkuu kutolewa Bungeni. Amekiri kuwa viongozi wa sekta zote wamelizungumzia na Serikali imeelewa inapaswa kufanya nini.

Amesema wakati mwingine kuyazungumza sana mambo haya inaweza kuwa sababu ya kuyasambaza na kuongeza uharibifu zaidi. Kwa kuwa Tanzania inafuata utawala wa Sheria, Spika Tulia amesisitiza kuwa Tanzania tayari ina Sheria ya Makosa ya Kujamiiana pamoja na Sheria ya Makosa ya Jinai ambazo zote zina vipengele vinavyozungumzia jambo hilo.

Ameiagiza Serikali kufanya utafiti kupitia tume ya kurekebisha sheria ya mambo yapi yaongezeke kwenye Sheria ya kuzuia Ushoga na Usagaji ili kuziba mianya iliyopo sasa. Sheria hiyo inapaswa kutungwa kwa uhalisia pasipo kufuata mihemko baada ya kufanya utafiti wa kutosha.

RIPOTI YA CAG KUFANYIWA KAZI MWEZI NOVEMBA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amesema Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka 2021/22 itafikishwa Bungeni baada ya Kamati zinazosimamia masuala ya Fedha kuipitia na kuwahoi watuhumiwa kisha majibu yatatolewa Novemba 2023.

Amesema kwa sasa hoja zinazoibuliwa na Wabunge hazitapatiwa majibu ikiwemo wahusika kuchukuliwa hatua yoyote hadi pale ambapo wahusika watahojiwa na Kamati za Chombo hicho kwa kuwa Serikali inazingatia haki za msingi za binadamu zinazojumlisha “Haki ya kusikilizwa kwa watuhumiwa”

Amebainisha kuwa kikao cha mwezi novemba kitatoa maazimio ya pamoja kwa Serikali ambayo yataonesha sura ya jumla ya mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa wahusika.

Mbunge Asia Abdulkarim Halanga ashauri wasanii wa kiume kuacha kuvaa uhusika wa kike

Mbunge Asia Abdulkarim Halamga ameshauri Wasanii wa Kiume Nchini kuacha kutumia Mavazi ya kike wakati wanapoigiza badala yake watafute njia nyingine ya kufikisha ujumbe kwa kuwa tabia hiyo inachangia kuhamasisha Mapenzi ya Jinsia moja

View attachment 2586538

Anaongea kwa jazba kama Mkarismatiki.
 
Mwanzo nilihisi hii ishu itakuwa ngumu mno kiutekelezaji ila kwa maneno ya Lisu hivi majuzi na jinsi wanavyoshungulikiwa ni jambo mzuri naamini hata alokawa anawaza kuingia kwenye hicho chama nadhani atakuwa ashabadilisha mind yake labda awe hajui kinachoendelea juu yao.

Nisisitize kwa kumalizia kuzipiga pin zile NGO's zote za mchongo zenye kufundisha huo uchafu pia washughulikiwe na Mabasha ambao wameathiriwa na huo ushenzi na naamini baada ya hapo nchi itakuwa salama kabisa kwa vizazi vyetu.
 
Yule Mkuu wa Wilaya ya Same , sijui anaitwa nani vile. Yule jamaa apewe tuzo katika kukabiliana na suala hili.

Jamaa yupo vizuri sana!!!
 
Mara nyingi mambo yanayofanikiwa ni yale yasiyo na matangazo ya kuji mwambafaiii

hata katika shughuli binafsi ukiwa na mission hutakiwi ongea wala kubadilika kitabiaaa ..... unanyatia hadi unakamata mwizi men
 
Yule Mkuu wa Wilaya ya Same , sijui anaitwa nani vile. Yule jamaa apewe tuzo katika kukabiliana na suala hili.

Jamaa yupo vizuri sana!!!
Natamani kujua kafanyaje huyo mkuu wa wilaya?
 
Iendane na mazingira ya sasa maana yake nini? Kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu uwepo wa mapenzi ya jinsia moja?
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 6 leo Aprili 13, 2023 jijini Dodoma.

SERIKALI YAAGIZA NHIF ITOE KIBALI MATUMIZI YA CT SCAN HOSPITALI YA IRINGA
Agizo hilo limetolewa baada Mbunge Jesca Msambatavangu kuhoji Bungeni sababu za wagonjwa wanaotumia Bima ya NHIF katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kutopewa kibali kutumia kadi zao kupata huduma ya CT Scan.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema “Namuagiza DG wa Bima kwamba mpaka kesho saa mbili asubuhi (Aprili 14, 2023) watu wanaostahili na waliotimiza vigezo waanze kupata huduma hiyo.”

MWONGOZO KUHUSU MASUALA YA USHOGA NA USAGAJI NCHINI
Akitumia kanuni ya 76, Mbunge Noah Saputu ameomba mwongozo unaotaka Bunge litoe msimamo wake kuhusu suala la ushoga kwa kuwa Mamlaka zote za Nchi ikiwemo Rais Samia, viongozi wa dini pamoja na taasisi zingine kubwa zimetoa msimamo wa kutokuafikiana na jambo hilo.

Ameomba Muswada utakaoleta Sheria kali uletwe Bungeni haraka ili Bunge liupitishe.

Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson amesema hoja hiyo imeibuka baada ya hotuba ya Waziri Mkuu kutolewa Bungeni. Amekiri kuwa viongozi wa sekta zote wamelizungumzia na Serikali imeelewa inapaswa kufanya nini.

Amesema wakati mwingine kuyazungumza sana mambo haya inaweza kuwa sababu ya kuyasambaza na kuongeza uharibifu zaidi. Kwa kuwa Tanzania inafuata utawala wa Sheria, Spika Tulia amesisitiza kuwa Tanzania tayari ina Sheria ya Makosa ya Kujamiiana pamoja na Sheria ya Makosa ya Jinai ambazo zote zina vipengele vinavyozungumzia jambo hilo.

Ameiagiza Serikali kufanya utafiti kupitia tume ya kurekebisha sheria ya mambo yapi yaongezeke kwenye Sheria ya kuzuia Ushoga na Usagaji ili kuziba mianya iliyopo sasa. Sheria hiyo inapaswa kutungwa kwa uhalisia pasipo kufuata mihemko baada ya kufanya utafiti wa kutosha.

RIPOTI YA CAG KUFANYIWA KAZI MWEZI NOVEMBA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amesema Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka 2021/22 itafikishwa Bungeni baada ya Kamati zinazosimamia masuala ya Fedha kuipitia na kuwahoi watuhumiwa kisha majibu yatatolewa Novemba 2023.

Amesema kwa sasa hoja zinazoibuliwa na Wabunge hazitapatiwa majibu ikiwemo wahusika kuchukuliwa hatua yoyote hadi pale ambapo wahusika watahojiwa na Kamati za Chombo hicho kwa kuwa Serikali inazingatia haki za msingi za binadamu zinazojumlisha “Haki ya kusikilizwa kwa watuhumiwa”

Amebainisha kuwa kikao cha mwezi novemba kitatoa maazimio ya pamoja kwa Serikali ambayo yataonesha sura ya jumla ya mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa wahusika.

Mbunge Asia Abdulkarim Halanga ashauri wasanii wa kiume kuacha kuvaa uhusika wa kike

Mbunge Asia Abdulkarim Halamga ameshauri Wasanii wa Kiume Nchini kuacha kutumia Mavazi ya kike wakati wanapoigiza badala yake watafute njia nyingine ya kufikisha ujumbe kwa kuwa tabia hiyo inachangia kuhamasisha Mapenzi ya Jinsia moja

View attachment 2586538

point taken!!!!!!!.....................................
 
Back
Top Bottom