Tulia Ackson: Nilishaumwa CORONA Mara mbili, watu wasidhani Mimi siijui

Tulia Ackson: Nilishaumwa CORONA Mara mbili, watu wasidhani Mimi siijui

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,480
Reaction score
7,443
Nimepigwa na butwaa baada ya kuona clip ikisambaa kwenye mitandao ikimuonesha Naibu Spika Tulia Ackson akidai kuwa alishawahi kuugua Covid 19 mara mbili.

Clip hii inamuonesha mwanamama huyu akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina Dkt. Likwelile.

Mbali ya kudai kuugua Covid 19 mara mbili, Naibu Spika amedai kuwa huwa havai barakoa sababu ya kuwa na matatizo ya kupumua. Hivyo sio kwa sababu kuna kiongozi anayemuogopa kwamba hatamfurahisha pale akivaa barakoa.

Lakini swali kubwa la msingi, lini huyu kiongozi aliugua Covid 19? Kama aliugua huko nyuma bona hakutaarifu umma? Mbona hatukupewa taarifa kama kuna maabukizi mapya? Je, hata mwaka 2020 wakati baadhi ya wabunge wanafariki, walifariki kwa Covid-19?

Maoni; Kusubiri vifo vitokee alafu ndio mtuambie kuwa mliugua Covid 19 ni unafiki wa kuwaduza watanzania kisasa. Haufai kabisa bora mkae kimya.
 
Bwana wao akisema Covid ipo na wao wanasema Covid ipo na kuwa wote walishaumwa na wakapona. Kesho akikanusha hakuna Covid na wao kwa umoja wao watakana kuwa hakuna.

Sasa hivi mambo yote yanakwenda kwa script. Kilichoandikwa kwenye script, ndicho hicho kitakachoigizwa.

Ogopa mtu ambae anadariki kumchukua mgonjwa alie mahututi na kumuweka mbela ya halaiki ya waandishi wa habari ili tu ku prove point kuwa Corona haiui. We are living in a very sad country in the hands a of sadist tyrant.
 
Kwani mkuu mbona hata wewe uliugua au unadhani kila auguae corona mpaka apumulie gas? ndio mgonjwa,binafsi season 1 ilinipiga ila hii ya sasa bado haijanipata na sijafunga tarumbeta la kuugua.
 
Back
Top Bottom