Tulia Ackson umepotosha umma: Rais wa Tanzania ni mkuu wa nchi ya Tanganyika, Zanzibar wana mkuu wa nchi yao

Tulia Ackson umepotosha umma: Rais wa Tanzania ni mkuu wa nchi ya Tanganyika, Zanzibar wana mkuu wa nchi yao

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nimemsikiliza ndugu Tulia Ackson akisema kuwa Rais wa Tanzania ni mkuu wa nchi.

Ukweli ni kuwa mamlaka ya rais wa Tanzania yako limited sana huko Zanzibar

Hata katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyorekebishwa mwaka 2010 inatamka wazi kuwa Rais wa Zanzibar ni mkuu wa nchi ya Zanzibar.

Kwa hiyo kwa muktadha huo ni sahihi kusema kuwa Rais wa Tanzania ni mkuu w Tanganyika iliyovaa koti la muungano lakini si mkuu wa nchi ya Zanzibar

Hata Kiprotokali, Rais wa Tanzania awapo Zanzibar kiitifaki Rais wa Zanzibar huwa yuko mbele yake

Naweka hapa katiba ya Zanzibar inayotamka wazi kuwa rais wa Zanzibar ni mkuu wa nchi ya Zanzibar

Screenshot_20220112_081811.jpg
 
Hapa nimegundua kuwa rais wa JMT kwa upande wa zanzibar anabakiwa na jukumu moja tu, nalo ni amirijeshi mkuu

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Hata kwenye ishu ya majeshi, Rais wa Zanzibar ana amri ya mwisho juu ya vikosi vya SMZ.
Sasa watu huwa wanajaribu kudogosha vikosi vya SMZ kuwa eti siyo majeshi but infact ni majeshi yale, yana structure zote na komandi kamili za kijeshi.
 
Atatoka tu kwa kudra za Mwenyezi Mungu kama Mandela alikaa jela zaidi ya miaka ishirini Mbowe ni nani?
Kwa hiyo Mandela alipata nini?

Rais mweusi South Africa?

Kwamba hilo ndilo lilikuwa hitaji la watu wa SA?
 
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar mkuu wa nchi yao ni rais wa Zanzibar na siyo rais wa Tanzania.

Ndiyo maana tunahitaji katiba mpya ili iharmonize mambo haya.
 
Back
Top Bottom