Tulia Ackson: Wanaotaka Kugombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini Wapime Kina Cha Maji

Tulia Ackson: Wanaotaka Kugombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini Wapime Kina Cha Maji

Tu hakikishe Msigwa, SUGU, LEMA ,LISU wanarudi bungeni kwa manufaa ya umma.
 
Mbunge wa Mbeya mjini kupitia CCM, Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la kugawanya jimbo la Mbeya mjini ni kusogeza huduma kwa wananchi na mchakato huo sio wa Mbeya pekee. Dkt Tulia aliongea hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha wasafi leo asubuhi.

Tulia amesema ubunge wake yeye haijalishi kama jimbo litagawanywa ama halitagawanywa, amedai kama alimtoa mtu(Sugu) kata zikiwa 36 ataweza kumtoa kata zikiwa chache? Alihoji mbunge Tulia.

Tulia amesema anaona akijadiliwa na wao inawapa sifa na katika mambo ambayo amasema huwa anayafurahia ni kujadiliwa hivyo ameupenda mjadala unaoendelea.

Tulia amesema wanaosema watamfuata amefurahi, anataka wajipime na kama wanaona kina cha maji kinawatosha wamfate.

Tulia amesema hata zikibaki kata 36 anawafyeka

Eti wapime kima cha maji mwee! Hivi wee daa Tuu A. Mwansasu police wakikaa zao kambini na kuruhusu wanasiasa washindane kisiasa huku wakurugenzi wakiondoshwa kabisa katika usimamizi kwa kuwa ni makada wa CCM, unaweza kumshinda kaka mkubwa Sugu? Muogope Mungu japokuwa najua wanasiasa na hofu ya Mungu siyo kivile.
 
Eti utafananisha na huyu anayelingushia miwani na suti mitandaoni. Waliokuwa wabunge wa chadema wanachosahau ni kuwa ccm ikiwa moja hakuna anayetoboa.

Wengi ukiangalia ushindi wao ulitokana na ccm kugawanyika kwenye kura za maoni. Miaka ile wengi walipita kwa rushwa. Watu wakachukia kwa watu muhimu kukatwa.

Wakapigia kura upinzani. Ndio siri ya ushindi upinzani. Sasa wao upinzani wanahisi walipita kwa sababu ya wafuasi wao ama wanapendwa sana.

Ndio maana Sugu anaongea kwa kutamba akidhani alipigiwa kura za haki kumbe ni kura za hasira kutoka ccm wenyewe.

Ye aombee tu ccm wagawanyike, ushindi wake utakuwa saa tatu asubuhi. Ila ccm ikiwa moja atandelea tu kuonyesha miwani na suti huku akizidi kuzeeka kwenye bustani za desderia hotel
Unakariri, uliyoandika yalishasemwa miaka 20 iliyopita
 
Na wewe kama unaakili ungepata namna ya kupambania haki unazodhani inanyanyanywa

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
Unaposema kuwa sasa Magufuli amekufa kwa nini musipeleke mashataka mahakamani, lazima utambue kuwa tayari hayo ni mapungufu makubwa. Kama watu wanashauriwa waende Mahakama baada ya Dikteta kufariki.

Hapo ndipo umuhimu wa kuwa na Katiba nzuri ambayo watu wote kwenye sheria wanakuwa sawa inapopata uzito
 
Tulia amesema ubunge wake yeye haijalishi kama jimbo litagawanywa ama halitagawanywa, amedai kama alimtoa mtu(Sugu) kata zikiwa 36 ataweza kumtoa kata zikiwa chache? Alihoji mbunge Tulia.

Tulia amesema anaona akijadiliwa na wao inawapa sifa na katika mambo ambayo amasema huwa anayafurahia ni kujadiliwa hivyo ameupenda mjadala unaoendelea.
Kwahiyo ni mtazamo wa kugombania kuwa fulani siyo kuwatumikia watu, after all ni huduma gani mbunge anasogeza kwa wananchi kama siyo kutaka kula kodi zao
 
Mheshimiwa Pohamba unasema kwamba sugu na Tulia wameridhia kugawana majimbo lakini kinachoendelea sasa ni maigizo ya kupoteza maboya?
 
Naunga mkono hoja , Tulia namkubali Sana huyo mother , ni ujinga wa Hali ya juu kukitoa kichwa kama Tulia alaf uingize mvaa mitepesho na mvuta bangi ,
Tangu Tulia amekuwa spika amefanya jambo gani bungeni kama spika?
 
Kuruka ruka kwa maharage ndo kuiva kwake, hapo Betina anarukaruka tu kwanza, subiri moto ukolee
 
Mbunge wa Mbeya mjini kupitia CCM, Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la kugawanya jimbo la Mbeya mjini ni kusogeza huduma kwa wananchi na mchakato huo sio wa Mbeya pekee. Dkt Tulia aliongea hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha wasafi leo asubuhi.

Tulia amesema ubunge wake yeye haijalishi kama jimbo litagawanywa ama halitagawanywa, amedai kama alimtoa mtu(Sugu) kata zikiwa 36 ataweza kumtoa kata zikiwa chache? Alihoji mbunge Tulia.

Tulia amesema anaona akijadiliwa na wao inawapa sifa na katika mambo ambayo amasema huwa anayafurahia ni kujadiliwa hivyo ameupenda mjadala unaoendelea.

Tulia amesema wanaosema watamfuata amefurahi, anataka wajipime na kama wanaona kina cha maji kinawatosha wamfate.

Tulia amesema hata zikibaki kata 36 anawafyeka

Unasogezaje huduma kwa wananchi kwa kuongeza walaji wa kodi
za wananchi?
 
Tulia nakuhakikishia hufiki mbali na hali ya Mbeya ilivyo kwa sasa na ulivyoharibu!
katafute kazi nyingine!
 
Back
Top Bottom