Tuliambiwa Mzee Yusuph anarudi kwa kasi ya ajabu, sijafanikiwa kusikia chochote hadi sasa

Tuliambiwa Mzee Yusuph anarudi kwa kasi ya ajabu, sijafanikiwa kusikia chochote hadi sasa

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Tuliambiwa kuwa anarudi kwa kasi ya ajabu kuja kuifufua taarabu iliyoonekana kupotea. Safari hii akitumia Safina na si Jahazi tena!
sijafanikiwa kusikia chochote mpaka muda huu.

Nimeona muda unaniacha au sipo sambamba na ya dunia ndo maana nimekuja kuuliza humu huweza nikasikia lolote. Sipendi hii miziki yetu ipotee kizembe hivi.....ni asili yetu.

Vipi, alifanikisha kutoa album? imezinduliwa? imefanya vizuri?

Ahsanteni
 
Atajijua na balaa lake, alijidai kumpenda Mungu, kajaribiwa kidogo na dhiki yamemshinda, ni aidha ana mwisho mbaya kidunia ama hatowika tena, hiki ndio nilifikiri pale tu niliposikia anarudi kwenye taarabu.

Kuna hadithi moja"bwana mmoja alimfata mtume s.a.w akamwambia anampenda, basi mtume akamwambia ajiandae kwa dhiki na mitihani mingi mingi"
 
Atajijua na balaa lake, alijidai kumpenda mungu, kajaribiwa kidogo na dhiki yamemshinda, ni aidha ana mwisho mbaya kidunia ama hatowika tena, hiki ndio nilifikiri pale tu niliposikia anarudi kwenye taarabu.

Kuna hadithi moja"bwana mmoja alimfata mtume s.a.w akamwambia anampenda, basi mtume akamwambia ajiandae kwa dhiki na mitihani mingi mingi"
Mzee yusufu kwemye dunia kaharibu akakimbilia kwenye dini, nako kwenye dini akaharibu kisha anataka kurudi tena kwemye dunia ambako alishaharibugi kitambo.

Kutoboa kwa taarafu kwake yeye kwa sasa ni ngumu
 
Mzee yusufu kwemye dunia kaharibu akakimbilia kwenye dini nako kwenye dini akaharibu kisha anataka kurudi tena kwemye dunia ambako alishaharibugi kitambo.

Kutoboa kwa taarafu kwake yeye kwa sasa ni ngumu
Kazi ipo.. Apambane na hali yake.
 
Haha juzi tu nimewaza juu ya huyu mzee na kauli zake za kejeli huko YouTube.
Niliwahi hudhuria shoo yake hivi karibuni, aah aisee, uwezo wa kuimba Hana tena,(pumzi& performance), watu tulikuwa wachache mno,lol better angebaki kushika Dini tu,maana anasikitisha
 
Upepo wake ulishapita. Halafu mziki wa taarabu umepungua sana umaarufu wake sio kama zamani. Alikua ana mpango wa kuja kwa kasi ila jamii imeshindwa kumpokea kwa kasi
Amechemka...sijui aende upande upi sasa
 
Haha juzi tu nimewaza juu ya huyu mzee na kauli zake za kejeli huko YouTube.
Niliwahi hudhuria shoo yake hivi karibuni, aah aisee, uwezo wa kuimba Hana tena,(pumzi& performance), watu tulikuwa wachache mno,lol better angebaki kushika Dini tu,maana anasikitisha
👍 👍
 
Upepo wake ulishapita. Halafu mziki wa taarabu umepungua sana umaarufu wake sio kama zamani. Alikua ana mpango wa kuja kwa kasi ila jamii imeshindwa kumpokea kwa kasi
inasikitisha.....maisha yanakimbia sana sana sana!
 
Back
Top Bottom