Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Kuna muda unawaangalia wapumbavu humu JF unashindwa kuelewa nani aliyewaroga unakosa majibu,hivi nyie mmezaliwa Tanzania hii hii au labda kuna nchi mlitoka tofauti na hii?[emoji2]au labda kusoma ndiko hujui?

Nilichosema hapo ni kuwa hao wanafunzi 12 ndiyo waliomaliza form 4 kwa mwaka wa kwanza toka shule hiyo ianzishwe mwaka 2003 na walifaulu wote! Kwenda shule za michepuo ya sayansi!.,Huko ni kijijini na yawezekana wanafunzi walikuwa hata 20 ila kwasababu ya mambo ya Bush wakawa wanapungua na waliofanya mtihani wakawa 12,sasa hapo wewe mwenye akili ambacho huelewi ni nini?.

Halafu wewe unataka kunilazimisha kwenye banda nililipa 500 wakati mimi ndiye niliyekuwa nalipa 100[emoji23][emoji23],yaani wewe kwa akili yako unaona mia ya mwaka 2004 ilikuwa ndogo,hebu tuambie wewe uko ulipokuwa mlikuwa mnalipa shi ngapi!,yaani mtu anataka akulazizimishe useme ambacho hata hukufanya ilimradi tu yeye alidhike[emoji23]

Hilo swali la kwanini tulilipa shilingi 100 alipaswa ajibu mtu wa banda na siyo mimi mlipaji,pengine gharama za vifurushi vya dstv vilikuwa bei chee ili kuwavuta wateja wengi, siwezi jua,sasa kama mjini tulikuwa tunalipa shilingi 200 iweje kijijini kusiko na biashara na mzunguko wa hela tulipe 200?,Unajua kama kuna maisha hukuwahi kuyaishi usiwe unakaa mbele ya wanaume unavimbisha kitambi na tumbo lako kwa ubishi![emoji23],Na ndiyo maana nikasema mwenye banda alikuwa akisubiri mpaka muda wa gemu uanze ndipo anawasha,yale mambo ya kuangalia uchambuzi yalikuwa hamna!.

Wewe nahisi kichwani hazikutoshi T14 Armata
 
Achana nao, ikiwaje usiwe unasoma comments unaweza kupanic ukatuacha na arosto buree
 
Wajuaji wengi mkuu
Endelea achana nao hao na kingine waambie huo mwaka nauli ya daladala ilikua 150 wakati nauli ya kutoka Dar mpaka Moro uliwa ndani ya Abood Andare Class nauli 2500
Wakati sasa daladala 500 nauli ya Abood Yutong Dar mpaka Moro 10000.
Ungewaongezea na tusi lingine mkuu.
 
Tumeweka kambi hapa endelea na stori mkuu
 
Wakuu kuweni na subra kidogo nakimbia kucheki gemu ya Arsenal vs Tottenham ikiisha nakuja kuendelea tulipoishia,kama nilivyosema mimi ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal,hivyo sipaswi kukosa gemu hata moja inayoihusu Arsenal,ikiwa itapigwa au ikishinda kwangu huwa ni raha tu!,ingawaje matokeo mabovu sometimes yananikata sana stimu!.

Nipeni nafasi wakuu narudi.
 
Arsenal anakufa leo

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Malizia story, Deborah alimfanya nini Emma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…