Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Back to the story,
Hata Mimi sija mwelewa pale anasema baba yake angempiga na asingesomeshwa shule na angekua mchunga ng'ombe endapo baba yake angejua amelala kwa Monica....

Huyu anasoma saa ngapi wkt anauza miwa?
Eps 01
UMUGHAKA ni mhitimu wa shule ya upili (sekondari), baada ya kuhitimu vidato vyake aliamua kwenda kumsalimu baba yake mdogo ambaye ni mkuu wa shule moja iliyopo usukumani.

Mpaka kufikia Eps 18 UMUGHAKA bado inaonekana ni mtu ambaye aidha anasubiri matokeo ama anasubiri kuendelea na masomo kwahyo hofu yake ilikuwa ni kwamba endapo baba yake mzazi ( ambaye ni kaka wa mkuu wa shule) ikitokea akapata taarifa hizo zingefanya asimsomeshe( yaani asimpe mahitaji ya shule muda wa kurudi shule utakapofika) badala yake akachunge ng'ombe.

Natumaini nitakua nimempunguzia mtunzi muda wa kutype, ili kuwaelewesha
 
Katika EPS zote, hii niliiisubiri kwa hamu na kwa muda mrefu sana, na nimeisoma kwa muda mfupi sana.

Ama kweli, KUSUBIRI KUNYONGWA, NI MATESO KULIKO HATA KUNYONGWA KWENYEWE!
 

Look before you leap. Na bado tunakosea ku look za uso tuu [emoji3][emoji3]
 
Tunaomba kiti cha UMUGHAKA kisikaliwe na mtu mwengine yoyote kwa kuwa ikifika muda wa kutuletea madude ya Monica plas Mwise basi mambo yote yaende vizuri,sio unafika muda wake UMUGHAKA mara kiti hamna tukazidi kupoteza muda.
 

We ni mtoto wa juzi endelea kubishaana but mtu ambaye sio mwanafunzi kupigwa pared na mwl ni kitu cha kawaida sana vijijin
 
Upo sahihi.Hapo mtunzi ameweka kitu kisicho na uhalisia.Jamaa sio mwanafunzi halafu ni mkubwa kuliko wanafunzi,at least angekuwa mdogo labda.Tena headmaster anamshtakia kwa wanafunzi kuwa hajalala nyumbani eti!

Halafu eti assemble!!Dah!
Hapo kidogo haina uhalisia ila sio kesi,tunaenjoy...
 
Hayajawahi kukukuta mzee tulia hivyohivyo
 
Ni kweli. Ndo shida kubwa humu ndani. Mtu yeyote akijua kusoma na kuandika anakuwa member.
Kaka we bado mdogo vingine acha vipite tu shule za enzi hizo ukiwa haupo alikuwa anachapika yeyote tu tena mbele ya wanafunzi awe ni mwanafunzi au asiwe mwanafunzi kwa hiyo wewe ni wa juzi kwa hiyo vilivyo juu ya uwepo wako viache tu.

Mfano mleta uzi kwenye simulizi zake nimezifuatilia kwa karibu mfano vitu anavyotaja unagundua kabisa hii stori kama ni chumvi iko kwa mbali sana
 
Huyo ni dogo hajui chochote achana nae mkuu, amekuta walimu wakuu wa siku hizi wanavaa mlegezo sasa utamwambia nn
 
Huyo ni dogo hajui chochote achana nae mkuu, amekuta walimu wakuu wa siku hizi wanavaa mlegezo sasa utamwambia nn

Atuulize sie watoto wa waalimu wakuu wa Kijijini enzi hizo.

Kwanza Mzee akikuta umejihusisha na ugomvi wa aina yeyote ile, haulizi umeonewa au nani anamakosa, lazima uchezee fimbo zisizo na idadi. Hata kama tayari umeshapewa adhabu na mwalimu mwingine. Na siku hiyo ukifika nyumbani, una kamisheni ya adhabu Kwa kosa lilelile la shule ambalo tayari umeshatumikia adhabu. Hapo anakuadhibu kama Baba Mzazi mbele ya wadogo zako iwe fundisho kwao.

Kuna siku tunalima shambani, akatokeza mjusi, dogo anaenifuatia akajipendekeza kuinama wakati nimeinua Jembe kumkata mjusi, si likatua kichwani kwake! Damu zinamwagika USO mzima, tukaenda nyumbani mbio, Ile amefika tu, akadakwa na fimbo za rasharasha mwili mzima...hapo nikasema kama wanaufanyia hivi mti mbichi, mkavu itakuwaje? Piga picha huyo anatembezewa kipigo ni mtu aliyekatwa Jembe, Sasa mwenye kumkata itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…