Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Ila Mkuu UMUGHAKA Story yako ni nzuri sana Naomba niambie Nikitaka kuchangia Bando hapo natumaje??
 
KUFANIKIWA NA KUFELI KWA MWANDISHI

KUFANIKIWA
1. Mwandishi kafanikiwa kutupa visa vilivyopangika katika muundo mzuri wa moja kwa moja vilivyojaa SUSPENSE ya kufuatilia episode moja baada ya nyingine

2. Uumbaji mzuri wa wahusika umeipamba vilivyo hadithi hii ukichagizwa na mandhari sadifu.


KUFELI KWA MWANDISHI

1. Mwandishi bado katuacha njiani na maswali mengi yaliyopaswa kuhitimishwa kulingana na jina la hadithi mathalani

.a..Inaonekana mzee Makono tu ndiye aliyedhurika katika kisa hiki je wachawi wengine katika kijiji waliishia vipi?

b. Mkasa wa mapenzi ulivyokuwa ukihadithiwa baina ya Umughaka na Monica pamoja na maagano ya kutomuacha kama ahadi ya kumnasua na kurogwa uliishia vipi?
 
Aisee hii shule isije ikawa ni Idete pale wilaya ya Uyui maana niliwahi kutana na visanga pale Ilalwansimba
 
Shukrani sana UMUGHAKA yaani umetuburudisha na kutuelimisha sana. Sasa na mimi naenda kununua kibuyu Kariakoo sokoni kisha nikilala nakiacha wazi ili wachawi wakija wanase na wawe wqnazunguka tu chumbani.

Weka namba ya Tigopesa/M-Pesa/Airtel money nk Basi tukutumie shukrani maana umetuburudisha bure kiroho safi kabisa.....

Atakayependa atakuwekea Muamala kidogo 🙏🙏🙏
 
Mkuu Impimpi Mbona nimeeleza vizuri kuhusu wale wachawi wengine!,baada ya wale waliokuwa wameingia ndani kushituka na kuondoka aliyeshughulikiwa ni mzee makono,ndiyo maana hata mama yake Monica alisema watapata habari huko waliko,yaani watasimuliana!,sasa unadhani kwa tukio lile lililokuwa gumzo pale kijijini kuna mchawi alirudi?,nilisema kuanzia hapo Headmaster na nyumba yake viliogopwa na mpaka anahama hakuwahi kuona tena viroja!.

Kuhusu mimi na Monica,nimeeleza vizuri ya kwamba niliondoka hapo kijijini kwenda shule advance na Monica nikamuacha kwao,sikufahamu maisha yake yaliendelea vipi kwa wakati huo huko kwao kwasababu sikuwa hata na simu,ila nikasema kuna mwaka nilikutana na mtu mmoja tuliyekuwa tukifahamiana pale kijijini na akaniambia Monica sikuhizi anaishi Mwanza ila sijajua ni sehemu gani maana hata aliyeniambia aliishia tu kusema anaishi Mwanza,maisha ya mimi na Monica yalikuwa niyale ya ujana lakini baada ya hapo hatujawahi kuonana!
 

KUFAULU NA KUFELI KWAKO KWENYE KUMCHAMBUA NDUGU MWANDISHI

KUFAULU
Ume elezea vizuri jinsi matukio,visa vilivyo patikana katika muundo mzuri wa moja kwa moja vilivyo jaa mashaka{suspense} ya kufatilia kipindi{episode} moja baada ya nyengine.

KUFELI KWAKO MTOA MAONI.
Ume haribu kiswahili adhimu/murua katika kujibu kwako,ilifaa utumie misamiati fasaha ya kiswahili pale ulipo weka msamiati wa kwanza ilifaa uweke MASHAKA{SUSPENSE} na KIPINDI{EPISODE.}
 
Nenda eagt city centre Kwa pastor Katunzi mpeleke huyo dogo pale Kwa maombi utqkuja simulia hapa Yule pastor katunzi namba wani in Tz nenda tu kanisani Kwa maombi bure kbsa Trust me nimempeleka mtu pale nimeonabkwa macho sasa HV anatoa shuhuda tu
 
Bravo
 
Emma kayavagaa tena[emoji23]
 
Asante sana Umughaka, bila shaka kupitia uzi huu utaongeza ndugu jamaa na marafiki, barikiwa kwa kuchangamsha jukwaa
 
Hadithi imesimuliwa imeisha bila mbamba safi sana. Kuna wengine wanasusa au wanaanza kujbizana na wale wavamizi wa uzi tuseme wachafuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…