Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumefika sehemu ya 11 na tayari ameshamranda dada mchawi usiku kuchaKipande cha saba mkuu ushakitoa maana umetuteka jf kwa mda
Sent from my TECNO BC2c using JamiiForums mobile app
Inawezekana aliiranda ile maza ilokuja kumsalimia ila yy kaona ni sura ya binti,huoni anasema binti alikua mzoefu na ushirikiano anautoa vzr sana,...😂😂😂haya mambo ya wachawi bana....unaeza kuta umeranda mbuz na denda umemla kudadadekiTumefika sehemu ya 11 na tayari ameshamranda dada mchawi usiku kucha
.Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 10
Safari mpya ya maisha ilianza rasmi pale nyumbani baada ya Maza mdogo kuja,kabla ya hajaja kutoka mjini tuliishi kwa kujiachia kama vile tupo mamtoni na tulikula na kunywa tutakavyo,lakini sasa yale maisha ya mwanzo yakatoweka,kula nyama ya kuku tena ilikuwa muujiza uliohitaji Mungu mwenyewe kuingilia kati!,kuku wale wa wikiendi walikuwa wakisafirishwa kupelekwa mjini na sisi hapo nyumbani kula Kayabo wa chukuchuku bila viungo,ilifikia sehemu ukila mboga iliyoungwa kwa mafuta na nyanya unamshukuru kwa muujiza wa kipekee!.
Kuku alipopikwa mimi na Ema vyetu ilikuwa ni miguu,shingo na kichwa na tunyama twa kuzugia kama tuwili hivi,nyama nyingine yote iliyobaki ilimuhusu Maza mdogo na mumewe!.
Tabia ile japo haikuwa nzuri lakini mumewe hakuwahi kuikemea,yeye alitulia tuli kana kwamba mkewe alichokuwa akitenda kilikuwa sawa.Sasa tulidhani siku si nyingi angeondoka lakini kumbe tulikuwa tunajidanganya!.Hatukufahamu kumbe kilichomleta hapo kijijini ilikuwa ni kuweka kambi kwa ajili ya biashara ya ushonaji wa nguo!.Pale senta kwa wakati ule hakukuwa na fundi cherehani,sasa nadhani mumewe alimwambia aichangamkie ile fursa iliyokuwa na hela za kutosha kwa kipindi kile hapo kijijini!.
Basi baada ya yule mzee Masumbuko kukataa ile miwa pamoja na mapapai alinikabidhi,nilimuomba anichumie majani ya mgomba ili nifungie ile miwa nipate urahisi kuibeba,yale mapapai aliniwekea kwenye kigunia cha chumvi chumvi(salfeti).Sasa nikanyanyua mzigo wa miwa nikajitwisha kisha nikamwambia yale mapapai aniwekee juu ya mzigo wa miwa ili nitandike kwato kuitafuta senta.
Ule mzigo haukuwa wa kitoto hata kidogo,lakini sikuwa na wakumdekea!,niliogopa endapo nikiutua ili nipumzike ni nani tena angenitwisha?,hivyo nilikomaa nao hivyo hivyo.Ingawaje Senta palikuwa mbali sikutaka kabisa kupumzika njiani,kuna muda nilikuwa nahisi shingo inauma lakini nilijikaza kisabauni kama mtoto wa kiume niliyetokea jamii ya Kikurya!.
Baada ya safari ndefu hatimaye nikafika senta.Sasa nilitafuta sehemu ambayo ni nzuri na yenye kivuli ili niweke ile miwa na mapapai nianze kuuza.Basi nilisogea kwenye mti mmoja ambao hakuwa mkubwa sana kisha nikaisimamisha ile miwa kwenye ule mti na yale mapapai nikayotoa kwenye ile salfeti nikayapanga yakawa tayari kwa kuuzwa!.
Nilipata taabu sana kuuza zile bidhaa kwasababu aliyesema nikauze hakuniambia niuzeje au alitaka faida ya kiasi gani!,nilichokuwa nakumbuka ni yeye kuununua ule mzigo kwa bei ya shilingi elfu 3.
Sasa ilibidi mimi mwenyewe nijiongeze kwenye namna ya uuzaji ili utoe hela ya watu na faida ipatikane.Nilianza kuuza ule mzigo hiyo mida ya saa 4 asubuhi lakini hakukuwa na wateja waliojitokeza kununua.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi,alikuja jamaa mmoja akiwa amefunga mzigo kwenye baiskeli na kuweka kambi lile eneo nililokuwepo.
Jamaa "Aisee mambo vipi?"
Mimi "Mambo poa"
Jamaa "Mbona umenivamia kwenye eneo langu?"
Mimi "Eneo lipi?"
Jamaa "Hapo ulipoweka mapapai ni eneo langu ambalo huwa naweka biashara yangu"
Mimi "Sikujua kaka,ngoja niondoe"
Jamaa "Hapana usiondoe,wewe sogeza kidogo kule kushoto ili na mimi nikipate kivuli"
Basi nikaamua kuyasogeza mapapai kushoto ya ule mti ambao nilikuwa nimesimamisha miwa.Yule jamaa alikuwa mstaarabu sana,japo kweli nilikuwa nimevamia eneo lake lakini hakutaka kunifukuza pale,alichoniambia ni kwamba nisogeze ili kila mmoja afaidi kivuli cha ule mti!.
Jamaa alifungua ule mzigo kwenye baiskeli kisha akatandika kavelo(turubai) ndipo akaanza kutoa kwenye boksi viatu aina ya kata mbuga(sendeu).Sasa kumbe jamaa ile ndiyo ilikuwa biashara yake pale siku zote ya uuzaji wa kata mbuga!.
Kiukweli baada ya jamaa kufika sikujiona tena mnyonge kwakuwa nilikuwa na mtu wa kupiga nays stori.
Muda ulipozidi kusonga na wateja wa miwa nao walianza kuja,sasa ishu ikawa ni kisu cha kukatia pingiri za miwa ningekitoa wapi!.Kuna kiduka kimoja ambacho kwa nyuma kulikuwa kuna nyumba,nikajongea mpaka pale nimaomba waniazime panga au kisu kwa ajili ya kukatia miwa halafu ningewarudishia!,yule aliyekuwa akiuza kwenye kile kiduka alikuwa mama mmoja ambaye alimuagiza mwanaye aniletee panga ila akasema nikimaliza nirudishe.
Kiukweli miwa niliuza sana ila mapapi hakuna aliyenunua hata moja.Sasa ilipofika mida ya saa 8 mchana nilikuwa nahisi njaa kishenzi na sikujua ningekula nini kwa wakati huo!,sikuwa na namna zaidi ya kukata pingiri tatu za muwa na kuanza kutafuna ili kupoza njaa!.Ilipofika mida ya saa 10 alasiri nilihesabu hela niliyokuwa nayo mfukoni ilikuwa jumla elfu 2600/=,Hiyo ilikuwa ya miwa pekee,papai hakuna lililonunuliwa mpaka muda huo.
Sasa nikiwa naendelea kuuza zile bidhaa pale,kwa mbali nikamuona Ba'mdogo akiwa anakuja pale senta,sasa kwakua alinicheki akiwa mbali hakupata taabu kunitafuta,hata hivyo ile senta haikuwa kubwa kiasi hicho mpaka nishindwe kuonekana.Alipofika niliona kama ananihurumia lakini hakutaka kuonyesha ile hali alijifanya kuvunga.
Ba'mdogo "biashara inaenda?"
Mimi "Ndiyo baba inaenda ila mapapai hayajanunuliwa"
Ba'mdogo "Ningejua ukaja na miwa tu,watu wa huku si walaji wa mapapai,wanapenda miwa"
Sikutaka kumjibu nikawa nimekaa kimya namtazama.
Ba'mdogo "mpaka sasa umeuza shilingi ngapi?"
Mimi "Nimeuza elfu mbili na mia sita baba".
Ba'mdogo "Sawa nipe hiyo hela"
Basi nikatoa ile hela mfukoni nikampatia akawa ameondoka kuelekea kwenye maduka yaliyokuwa upande wangu wa kulia.Hakukaa sana kule akawa amerejea nilipokuwepo.
Ba'mdogo "Yule mama anamuona?"
Akawa anionyesha kwa kidole uelekeo alipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa kwenye matofali ya kuchoma.
Mimi "Ndiyo baba namuona"
Ba'mdogo "Ikifika jioni hayo mapapai hujauza,nenda umpelekee yule mama,nimemwambia tayari"
Mimi "sawa"
Baada ya maelekezo yale yeye akawa ameondoka na mimi kubaki pale.
Ilipofika mida ya saa 12 jioni,kweli nilimpelekea yule mama yale mamapai baada ya kudoda kutwa nzima pale chini!.
Miwa nayo ikawa imebaki miwili,sasa nikaona nimuombe yule mama aliyeniazima kisu ile miwa niilaze pale kwake ningekuja kuifuata asubuhi,yule mama hakuwa na tatizo alikubali!.
Sasa nikaanza kuwaza wakati wa kurudi nyumbani nipite njia ipi,je nipite ile ya mzunguko wa lamboni au nipite ileile fupi iliyokuwa katikati ya ile miembe mikubwa!.Wakati huo mfukoni nilikuwa nina shilingi 700.Basi nikaone ni heri nipite ile fupi ili niwahi kufika nyumbani.
Nilimuaga yule jamaa tuliyekuwa tukiuza wote hapo nikamwambia tungeonana kesho yake,jamaa nae akawa ameniambia naye angeondoka muda si mrefu.
Nikaanza kupiga kwato mdogo mdogo kurudi nyumbani.Wakati natembea kiukweli nilikuwa nina mawazo mengi sana,ukizingatia nilikuwa sijala chochote zaidi ya kutafuna vipande kadhaa vya muwa!.Niliona kabisa mambo endapo yangenishinda ningerudi nyumbani!.Wakati huo giza nalo lilikuwa halichezi mbali maana ilikuwa mida ya saa 1 usiku.
Sasa wakati natembea huwaga nina kawaida ya kuangalia chini kama kondoo,huwa naangalia mbele,kushoto na kulia kwa muda mfupi sana lakini muda mwingi huwa natazama chini!,sijajua ni kwanini uenda ndivyo nilivyozaliwa na kurithi kwa mzee wangu!.
Sasa wakati nakwenda sikumuona mtu nyuma yangu wala mbele yangu akiwa anakuja,nilishitukia tu ghafla naitwa jina langu na mzee ambaye nilikuwa napata taabu kumkumbuka.
Mzee "Hujambo Umughaka"
Nikashituka sana!,nikabaki nashangaa ametokea wapi yule mzee mtu mzima!,nikadhani uenda muda ambao nilikuwa natembea huku nikitazama chini sikumuona.
Mimi "Sijambo,shikamoo"
Mzee "Marhaba,vipi mwalimu yupo?"
Mimi "Eenh yupo"
Mzee "sawa utamsalimia"
Mimi "Sawa,nimwambie nani vile!"
Mzee "we mwambie Makono anamsalimia"
Mimi "Sawa"
Yule mzee nilianza kuvuta taswira nimewahi kumuona wapi lakini nikawa sikumbuki vizuri!.Alikuwa mtu mzima mwenye miaka kama 50 -60 hivi!.
Sasa wakati natembea zangu nikawa nageuka nyuma ila cha ajabu yule mzee sikumuona!,nikabaki nashangaa kwasababu lile eneo pembe zoni hakukuwa na njia ya mchepuko,pia kulikuwa na katani za kutosha ambazo kama ungejifanya kuchepuka basi zingekuchoma na ile miba yake mpaka uchanganyikiwe na kile kibarabara kilikuwa kimenyooka moja kwa moja.Tulikuwa tumetoka kuzungumza kwa sekunde kadhaa tu lakini cha ajabu kugeuka nyuma sikumuona tena!,Kuhusu jina langu sikuwaza sana nikawa nasema huenda Ba'mdogo aliwahi kumwambia mimi ni kijana wake na jina langu ni umughaka.
Basi namshukuru Mungu siku hiyo niletembea kwa amani kabisa hakukuwa na viroja wala vituko nilivyokutana navyo pale kwenye miembe.Nilifika nyumbani mida ya saa 2 usiku.Sasa wakati usiku tukiwa tunakula Ba'mdogo akawa ameniambia hela niliyokuwa nayo nihakikishe asubuhi naelekea kwa mzee masumbuko kufata miwa mingine ili nikauze kwa kuwa hiyo ndiyo iliyokuwa kazi yangu.
Tulipokuwa tukiendelea kula nikamwambia Ba'mdogo alikuwa anasalimiwa na yule mzee niliyekutana naye muda si mrefu.
Ba'mdogo "Makono?,makono ndiyo nani?"
Mimi "mimi sijui baba,yeye ameniambia nikwambie hivyo utamfahamu"
Ba'mdogo "Uenda atakuwa mzee mwalukala huyo,yule ndiye huwa anamajina mengi ya utani"
Basi mimi sikutaka makuu,nilipomaliza kula nilielekea zangu kulala kwakuwa nilikuwa nimechoka,Ema yeye alipoingia ndani akaanza kupiga buku kama kawaida.
Sasa picha ya yule mzee ikaanza kunijia vizuri na nikakumbuka ni yule mzee ambaye alikuja na mwenyekiti pale nyumbani siku ile ambayo Ema alikuwa ametoka kukung'utwa viboko darasani na watu wasiofahamika.Yule mwenyekiti wakati anakuja na headmaster pale nyumbani kumohoji Ema alikuwa na huyo mzee,ndipo nikawa nimemkumbuka vizuri.
Basi asubuhi mida ya saa 1,niliwahi kuamka lakini sikumuona Ema,nikasema uenda aliwahi mapema kwenda shuleni wakati mimi nikiwa nimelala.Nilipomaliza kupiga mswaki wakati navaa viatu ili niende nikamsalimie Maza mdogo na mumewe ili niondoke zangu,mara nikaanza kusikia sauti za wanafunzi huko shuleni wakipiga kelele kwa nguvu.