Tulifika Pabaya: Mwenyekiti Ulinzi na Usalama Wilaya eti ni Jambazi?

Tulifika Pabaya: Mwenyekiti Ulinzi na Usalama Wilaya eti ni Jambazi?

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Naomba tukubaliane wote, kwamba nchi hii katika awamu ya tano tulifika pabaya sana chini ya Amirijeshi mkuu Magufuli.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa au wilaya (RC or DC) ni mtu muhimu sana katika eneo husika kwa ajili ya usalama na ulinzi.

Sasa tulifikaje hapa ambapo mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya anafikia hatua ya kushtakiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha (ujambazi)?

Inamaana serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli ilikuwa haijajui haya aliyokuwa anatenda DC huyu? Au ilijuwa ikanyamaza kwa vile ni DC wa Hai? na ndio maana watetezi wa Sabaya makada wa CCM, walimtetea sana?

Mnaona uchama CCM ulivyokuwa umeifikisha mahali pabaya nchi?

Hii maana yake ni kuwa, kama ya sirini ya Sabaya yanajulikana basi walio mpiga risasi Lissu na kumuua Akwilina mchana wanajulikana, walioteka watu mchana wanajulikana nk.

Sasa ili nchi isafishike walio tenda maovu wote kwa kutumia kivuli cha serikali ya Jamhuri ya Tanzania washughulikiwe bila aibu ili kuliondolea balaa taifa (hii Mshana Jr ) anaweza kuielezea vizuri zaidi maana pengine inahitaji maombi au kafara ya kitaifa.

TULIFIKA PABAYA KAMA TAIFA
 
DC kaiba simu na pesa 35,000 kwa kutumia silaha.

Armed robbery ndiyo hutumika kutuliza vibaka uswahilini, ukiwa ingia toka O'bay au Mabatini haziishi wanakupa hiyo utulie kwanza.
 
Baba jambazi, ulitegemea nini kwa maana watoto pendwa ulitegemea wasiwe majambazi.Ulikuwa utawala dhalimu, utawala uliofitinisha na kufarakanisha huku tukiaminishwa kuwa ni wa Kizalendo.Kodi za dhuruma na makosa ya kubambikiza.Mungu Hajawahi Kukosea.Tusonge mbele Mungu anaipenda sana Tanzania..
 
Kuna uongo mwingi hapa kwa sababu sasa liko kundi lenye uoga kwa matajiri wakwepa kodi na wazungu washenzi wezi wa Mali za umma.

Sabaya katolewa Kafara tu kwa kumtungia kesi za uongo kwa sababu ya wenye pesa kuweka nguvu ktk kila sehemu panapo mshutumu Sabaya ili aangamizwe,kwa ninavyo wajua waTanzania matajiri ni kweli wakati Sabaya akiwawajibisha kulipa kodi siamini kama aliwaonea,hao hua ni wakwepa kodi wakubwa kwa nguvu za pesa wanahonga kuvusha mizigo yao ya kibiashara

Swala la Hayati JPM linaendelea kushutumiwa kwa uongo na nina hakika 90% ya wanaozusha haya ni watu wa Kaskazini wabinafsi na wapigaji...ni ngumu sana kuondoa upendo wa JPM kwa watu zaidi ya 85% hapa nchini isipokua ni watu wasio sema sema wala hawaingii mitandaoni.

Nchi hii mtu ukiwa mkali na kutetea wengi wasinyonywe na wachache unaitwa dikteta,ukiwa mpole na watu wanaiba wanafurahi na wale wasio na mianya ya kuiba wanakuita dhaifu

Tanzania ni nchi yenye watu wasiojua wanatakaga nini.
 
Kuna uongo mwingi hapa kwa sababu sasa liko kundi lenye uoga kwa matajiri wakwepa kodi na wazungu washenzi wezi wa Mali za umma...
Matajiri wapo Wilaya ya Hai tu hapa Tanzania? Mbona Wakuu wengine wa Wilaya hatukuwasikia wakipambana na Matajiri walipe kodi? Kwa nini Sabaya peke yake? Au yeye ndiye Magufuli ajaye?
 
Bado yule "mtoto" wake wa Dalisalama, yakifumuka ya kule tutashangaa hakuna mfano!

Yule ni zaidi ya Sabaya, ametesa watu sana , Ameua watu ukigombana nae kidogo unajikuta kwenye kiloba coco beach ,amebambikia sana watu case za drugs wanakuja kwako wanafanya search wanakuwekewa ili ufungwe

GSM na the late dr Mengi ndio walikamuliwa hela zao Mpaka Basi
 
Hayo makosa ni Yale yanayodhaniwa kufanyika miezi michache iliyopita.
 
Back
Top Bottom