Naomba tukubaliane wote, kwamba nchi hii katika awamu ya tano tulifika pabaya sana chini ya Amirijeshi mkuu Magufuli.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa au wilaya (RC or DC) ni mtu muhimu sana katika eneo husika kwa ajili ya usalama na ulinzi.
Sasa tulifikaje hapa ambapo mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya anafikia hatua ya kushtakiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha (ujambazi)?
Inamaana serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli ilikuwa haijajui haya aliyokuwa anatenda DC huyu? Au ilijuwa ikanyamaza kwa vile ni DC wa Hai? na ndio maana watetezi wa Sabaya makada wa CCM, walimtetea sana?
Mnaona uchama CCM ulivyokuwa umeifikisha mahali pabaya nchi?
Hii maana yake ni kuwa, kama ya sirini ya Sabaya yanajulikana basi walio mpiga risasi Lissu na kumuua Akwilina mchana wanajulikana, walioteka watu mchana wanajulikana nk.
Sasa ili nchi isafishike walio tenda maovu wote kwa kutumia kivuli cha serikali ya Jamhuri ya Tanzania washughulikiwe bila aibu ili kuliondolea balaa taifa (hii
Mshana Jr ) anaweza kuielezea vizuri zaidi maana pengine inahitaji maombi au kafara ya kitaifa.
TULIFIKA PABAYA KAMA TAIFA