Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Tulikabidhiwa jezi ya huu mchezo unaoitwa maisha, kabla hata hatujawa tayari kuingia uwanjani.
Wala hatukuwa na uhakika wa kwenda kubadilisha matokeo.
Ghafla tu, tukaambiwa baba amechoka, Mama Hana msaada pale mbele. Nenda kaipe tumaini team.
Sisi ni makipa tunajua kudaka na kusubiri mashuti tu.
Cha kushangaza tuliambiwa tukacheze kiungo, tuitulize team na kutengeneza chance kwa madogo walio nyuma yetu.
Haikuwa rahisi, tulitokea bench mechi tukiwa tunaongozwa bao tatu bila.
Umasikini usio na kesho, familia bila connection, na kipaji pasipo kuaminika.
Ajabu tulivyoingia uwanjani, kuna watu walijiandaa kwaajili ya kutupa injury.
Labda hawakujua, tukiumia sisi, imepoteza mchezo team yenyewe.
Tuna umri mdogo ila ukituona ni kama tumeshazeeka, kwasababu tulipewa kitambaa cha unahodha kitambo, ili team isishuke daraja.