Tulikabidhiwa Jezi

Tulikabidhiwa Jezi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tulikabidhiwa jezi ya huu mchezo unaoitwa maisha, kabla hata hatujawa tayari kuingia uwanjani.

Wala hatukuwa na uhakika wa kwenda kubadilisha matokeo.

Ghafla tu, tukaambiwa baba amechoka, Mama Hana msaada pale mbele. Nenda kaipe tumaini team.

Sisi ni makipa tunajua kudaka na kusubiri mashuti tu.

Cha kushangaza tuliambiwa tukacheze kiungo, tuitulize team na kutengeneza chance kwa madogo walio nyuma yetu.

Haikuwa rahisi, tulitokea bench mechi tukiwa tunaongozwa bao tatu bila.

Umasikini usio na kesho, familia bila connection, na kipaji pasipo kuaminika.

Ajabu tulivyoingia uwanjani, kuna watu walijiandaa kwaajili ya kutupa injury.

Labda hawakujua, tukiumia sisi, imepoteza mchezo team yenyewe.

Tuna umri mdogo ila ukituona ni kama tumeshazeeka, kwasababu tulipewa kitambaa cha unahodha kitambo, ili team isishuke daraja.

FB_IMG_1728742708089.jpg
 
Yani tumeshakua kama Ntibazonkiza kumbe bado umri kama Denis nkane... ila tatizo zaidi linachangiwa na Shirikisho kumuachia kibendera TaTu Malogo kila tukitaka kufunga Offside ila upande wa pili wanafunga tunarudishwa kati....Tuna miguu ya Aziz Ki ila tuko Mashujaa kama Crispin Ngushi...
 
Waafrika wengi siwatofaitishi na wanyama pori kama nyumbu, swala na wanyama wengine wa mwituni. Mtu anazaa akiwa hana mikakati ya kulea watoto anaowazaa yaani waafrika wakipigwa na maisha ndipo wanafyatua watoto kama tofali sijui wanamini kuwa watoto ndio watakuja kumsaidia pale alipopashindwa.

Inafikirisha!
 
Nje ya mada mkuu,
kwanini ukimtongoza mwanamke akakukataa mnakuwa maadui 😂😂
Kanuni muhimu ya kutongoza: usipige shuti kama huna uhakika wa kufunga! Utapaisha kisha utazomewa halafu utajisikia vibaya
Kanuni ya pili usiondoe gari mpaka kijani iwake! Na kama Umeme umekatika na hakuna traffic epuka gombania goli
 
Waafrika wengi siwatofaitishi na wanyama pori kama nyumbu, swala na wanyama wengine wa mwituni. Mtu anazaa akiwa hana mikakati ya kulea watoto anaowazaa yaani waafrika wakipigwa na maisha ndipo wanafyatua watoto kama tofali sijui wanamini kuwa watoto ndio watakuja kumsaidia pale alipopashindwa.

Inafikirisha!
Starehe ya fukara ni ngono
 
Yani tumeshakua kama Ntibazonkiza kumbe bado umri kama Denis nkane... ila tatizo zaidi linachangiwa na Shirikisho kumuachia kibendera TaTu Malogo kila tukitaka kufunga Offside ila upande wa pili wanafunga tunarudishwa kati....Tuna miguu ya Aziz Ki ila tuko Mashujaa kama Crispin Ngushi...
Una kipaji princess kiendeleze❤❤❤💪🏿
 
Back
Top Bottom