Tulikamatwa kinyume na sheria kwa sababu za kisiasa na tukaachiwa kisiasa

Tulikamatwa kinyume na sheria kwa sababu za kisiasa na tukaachiwa kisiasa

Hawa ndiyo wazalendo wanaopigania Maliasili ambazo watafaidi watoto wetu na wajukuu wetu.Wekeni utaratibu tuwachangie chochote ili kuwapa hamasa ya kuishughulikia hii serikali OVU inayouza maliasili zetu kwa kuahidiwa zawadi za kijinga ambazo ni punguani na kichaa pekee anayeweza kukubali.Aluta continua
 
Historia imeandikwa kwa wino wa dhahabu.
Hawa ndio wazalendo.
Mungu anaonekana waziwazi kupitia kwa hawa watu.
 
Niliwahi sema na leo narudia:

Wengi tulizaliwa ili kuishi katika huu ulimwengu, ila kuna wachache walizaliwa kwa malengo maalumu ili wengine tuweze kuishi/ku-survive kulingana na mapenzi ya alietuweka hapa duniani.

You are one those few selected individuals.

Congratulations!!
 
Hizi aya 2 ni nimezipenda sana:

"Msimamo wetu ni kwamba tumewajulisha polisi kwamba hawana hiyo mamlaka ya kutuzuia sisi kusafiri kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Kwamba tutasafiri na wakitusumbua tumewaambia wadhamini wetu waandike barua za kujitoa halafu waturudishe mahabusu na kisha watupeleke mahakamani. Lakini pia bado niko kwenye mashauriano na mawakili wangu nataka kuwafungulia kesi baadhi ya maafisa wa polisi kwa majina yao badala ya vyeo vyao maana askari unapofanya vitu kinyume na sheria hiyo ni utashi wake binafsi na anapaswa kuwajibika mwenyewe."

"Msimamo wetu ni kwamba maandamano ya nchi nzima yako palepale. Kitu pekee kitakachositisha maandamano haya ni serikali kusitisha mkataba huu mbovu wa bandari kati ya nchi yetu na DP World ya Dubai. Kwenye hili sisi tuko tayari kunyongwa, kwanza kunyongwa kwa ajili ya kupigania rasilimali za nchi hii ni fursa tunayoitaka hata kesho. Hatumuogopi yoyote isipokuwa Mungu muumbaji wa mbinguni."
 
1. 𝗞𝘂𝗸𝗮𝗺𝗮𝘁𝘄𝗮
Mnamo usiku wa manane tarehe 12 august 2023 siku ya ijumaa usiku tukiwa safarini tulikamatwa na askari polisi maeneo ya mikumi check point karibu na mizani. Askari hao walituambia wamepata maagizo kutoka juu ya kutushikilia Mimi pamoja na wezangu Emmanuel Godfrey Masonga pamoja na wakili Boniface Mwabukusi bila kuweka wazi tuhuma zilizokuwa zikitukabili kinyume kabisa na sheria za nchi.

Askari hao walianza kupekua gari yetu na kukisanya simu zetu pamoja na laptop kinyume na sheria Kisha kutuweka kizuizini kituo Cha polisi mikumi. Hata tulivyowauliza mnatushirikilia kwa tuhuma gani walidai wao hawajui chochote isipokuwa Kuna askari wanatoka ofisi ya RCO Morogoro ndio wanaojua.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni wajibu wa askari polisi kumjulisha mtuhumiwa tuhuma zake kabla ya kumkamata na mtuhumiwa anapaswa kuhojiwa ama kuandika maelezo ya kosa lake kwa masaa yasiyozidi manne tangu kukamatwa kwake kisha kufikishwa mahakamani kwa masaa yasiyozidi 24. Lakini sisi mpaka tunasafirishwa kutoka kituo cha polisi Mikumi kwenda Mbeya bado mashtaka yetu hayakuwekwa wazi huku Masonga akiachiwa kwa dhamana kwa kosa ambalo bado halikuwekwa wazi.

Siku 1 baadaye yani jumapili usiku mimi na wakili Mwabukusi tulihojiwa kwa nyakati tofauti kwa tuhuma za uhaini. Kwamba mimi Mdude Mpaluka Nyagali na wenzangu tunapanga kumpindua Samia na serikali yake. Nilikataa kutoa maelezo na badala yake niliwajulisha polisi kwamba maelezo yangu nitatolea mahakamani.

2. 𝗞𝘂𝗴𝗼𝗺𝗮 𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮
Kwamba tangu tulipokuwa tunashirikiwa mikono mwa polisi tulizuiwa kuonana na mawakili wetu pamoja na ndugu. Polisi walikuwa wanalazimisha sisi kula chakula bila kutuweka wazi chakula kilikotoka. Kwa mazingira hayo tukalazimika kugoma kula wala kunywa chochote kwa siku 4 mfululizo mpaka waliporuhusu ndugu yetu kutuletea chakula moja kwa moja.

3. 𝗧𝗲𝘁𝗲𝘀𝗶 𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗲𝗹𝗲𝗸𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗵𝗮𝗸𝗮𝗺𝗮𝗻𝗶
Kwamba mnamo 16th august 2023 mimi na mwenzangu wakili Mwabukusi tulijulishwa na ofisi ya RCO Mbeya kwamba tutafikishwa mahakamani siku hiyo kwa mashitaka ya uhaini baada tu ya kuchukua simple za sauti zetu. Kwa bahati mbaya hatukufikishwa mahakamani na wala hatukuambiwa kitu gani kimekwamisha kwani tayari sisi tulikuwa tumejiandaa kwenda gerezani.

4. 𝗞𝘂𝗮𝗰𝗵𝗶𝘄𝗮
Mnamo 18th August 2023 siku ya ijumaa mimi na mwenzangu wakili Mwabukusi tuliitwa tena ofisini kwa RCO na kutujulisha kwamba tutafute wadhamini. Kwanza tulipigwa na butwaa maana kwa mujibu wa sheria za Tanzania makosa ya uhaini hayana dhamana, lakini pia hatukuhojiwa kosa lingine isipokuwa uhaini.

Kwa mazingira hayo sisi tulikataa na badala yake tukataka watufikishe mahakamani na hata kama hawajaandaa hati ya mashitaka sisi tuliwajulisha kwamba tutakuwa tayari kukaa kituoni hapo mpaka watakapokuwa wameandaa hati hiyo. Lakini pia tulitaka kuonana na mawakili wetu ambao walikuwa wanatuzuia kuonana nao. Baada ya kuonyesha msimamo huo tulirudishwa mahabusi lakini masaa mawili baadaye tuliitwa na kujulishwa kwamba mawakili wetu wamekamilisha dhamana bila ya kuwasiliana na sisi kama tulivyotaka. Na tulipoachiwa tumeambiwa kwamba moja ya masharti ya dhamana hiyo ni kutosafiri nje ya mkoa wa Mbeya.

Msimamo wetu ni kwamba tumewajulisha polisi kwamba hawana hiyo mamlaka ya kutuzuia sisi kusafiri kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Kwamba tutasafiri na wakitusumbua tumewaambia wadhamini wetu waandike barua za kujitoa halafu waturudishe mahabusu na kisha watupeleke mahakamani. Lakini pia bado niko kwenye mashauriano na mawakili wangu nataka kuwafungulia kesi baadhi ya maafisa wa polisi kwa majina yao badala ya vyeo vyao maana askari unapofanya vitu kinyume na sheria hiyo ni utashi wake binafsi na anapaswa kuwajibika mwenyewe.

5. 𝗔𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮𝗻𝗴𝘂
Kwamba baada ya kuachiwa nilipata matatizo ya tumbo katika mfumo wa chakula na choo. Kwamba baada ya matibabu kwa wiki sasa naendelea vizuri.

6. 𝗠𝘀𝗶𝗺𝗮𝗺𝗼
Msimamo wetu ni kwamba maandamano ya nchi nzima yako palepale. Kitu pekee kitakachositisha maandamano haya ni serikali kusitisha mkataba huu mbovu wa bandari kati ya nchi yetu na DP World ya Dubai. Kwenye hili sisi tuko tayari kunyongwa, kwanza kunyongwa kwa ajili ya kupigania rasilimali za nchi hii ni fursa tunayoitaka hata kesho. Hatumuogopi yoyote isipokuwa Mungu muumbaji wa mbinguni.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

Vwawa - Songwe.View attachment 2727459
Hawa ndio wanaume hapa Tz.
 
Back
Top Bottom