Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama asali, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amrbski hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?
Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.
Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.