Tulikosea Wapi? Tufanyeje Kujirekebisha?

Tulikosea Wapi? Tufanyeje Kujirekebisha?

Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama asali, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amrbski hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?

Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.

Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.
Ahaha ! nimecheka saana leo mkuu wangu hilo shimo lilozungukwa na nzi inatosha kabisa kunipa picha... Tutaendelea kesho ngoja nipate daku kwanza .. duh umenipa usingizi leo..
 
Chifu Kichuguu, mimi naona taifa kama taifa lilikosea sana 'kuparamia' mfumo wa kibepari katika miaka ya 1980. Taifa lilivyokubali sera za IMF na IBRD/Benki ya Dunia; bila ya taifa kufanya tafakuri ya kina ya namna gani sera hizo zitafit/zingefit mazingira ya Tanzania (kumbuka kipindi hicho taifa lilikuwa linafuata itikadi na misingi ya kijamii).

Tulipoanza kutumia sera hizo - soko huria, kupunguza matumizi ya serikali (haswa katika kusitisha ajira serikalini, kuchangia gharama katika huduma za kijamii - maji,elimu n.k.). Kwa vile watanzania wakiwemo watumishi wa umma walikuwa hawajajianda au hawajaandaliwa kuwa katika mfumo huo,hapo ndipo mikanganyiko (ya kiuongozi,kiutumishi wa umma na hata wa kifikra) ilipoanza kutokea na kushika hatamu. Hali ilizidi kuwa mbaya pale Zanzibar, 'viongozi' wetu walipoamua kulifutilia mbali Azimio la Arusha.

Wapi pa kujirekebisha: kwa mtazamo wangu,kuna haja ya taifa kuamua kwa dhati kabisa ni mfumo gani utatufaa ili kuleta maendeleo kwa watu wake. Mfumo ambao mimi nautamani ni ule wa mchanganyiko - ubepari + ujamaa. Na hapa mchanganyiko nina maana kutumia yale mazuri ya kila mfumo katika kupunguza ama kuondoa kabisa mapungufu ya mfumo mmojammoja. Hii ni kwa sababu taifa letu liliparamia ubepari bila kuchanganua madhaifu ya ubepari,huku likiacha mazuri ya ujamaa. Taifa linapaswa lijifunze na lifahamu kwamba katika uhalisia hakuna taifa linalofuata ubepari au ujamaa kwa asilimia 100 hapa duniani kwa sasa. Hata hizo nchi zinazoitwa za kibepari zina mifumo yenye chembechembe za ujamaa. Angalia ruzuku katika kilimo,usafiri wa umma,upatikanaji wa habari (ambapo serikali usambaza magazeti bure kwa watu wake ili wapate habari),hifadhi za jamii (social security),huduma za bure za chakula,malipo kwa wasio na ajira n.k. Sasa Tanzania ilipoagizwa na IMF/WB ikasahau kabisa chembechembe hizo zenye manufaa makubwa na ya moja kwa moja kwa wananchi.

Hivyo katika mjadala wa katiba mpya,taifa kama taifa tuamue kuwe na mfumo mchanganyiko ili tuutumie katika kuweka dira za maendeleo ya watu.
 
Last edited by a moderator:
MAMMAMIA
..................hilo haswa ndilo jawabu, lakini je wazalendo hao tutawatoa wapi iwapo wote wameshaharibika? Kumbuka kuwa unahitaji kuondoa karibu mahakimu wote, polisi wote, wanajeshi wote, watumishi wa serikali karibu wote.
Maelezo ya kina ameyatoa Mkandara #16: Njaa, Ujinga, Maradhi na katika haya matatu, ujinga ndio unaoweza kusababisha yote hayo na zaidi ya hayo. Juzi tulikuwa tunajadili hapa ilikuwaje Korea ya Kusini kuendelea ndani ya utawala wa kidikteta? Pamoja na mengine, S. Korea imeedelea kwa sababu ya kuweka elimu kuwa ni kipaumbele cha mwanzo. Hapa sitetei udikteta, lakini "kama hakuna budi" basi bora udikteta wa muda lakini nchi ikawa na lengo maalumu, kuliko demokrasia ya kulazimishwa daima bila malengo. Tanzania imepoteza malengo, achana na nyimbo ya MALENGO YA DUNIA YA MAENDELEO; hiyo ni ya kutembezea bakuli tu, tunapewa sumu katika katika kichupa kiliansikwa tiba.

Pia tusisahau falsafa ya Mwalimu Nyerere, Ili tuendelee tunahitaji mambo manne - Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi Bora - Tanzania tumebakiwa na lipi katika hayo? Itaonekana kama vyote vipo lakini hapana hata kimoja.
WATU: Ndio hao tuliojadili juu - Wengi wetu tuna njaa, ni wajinga, ni wagonjwa.
ARDHI: Imtoka kuwa mali ya taifa/umma, imekuwa mali ya wachache, matajiri na wanasiasa
SIASA SAFI: Ni aibu leo kuendelea kusoma kwenye Katiba ya JMT kuwa "Nchi inaongozwa na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea." Ukweli Tanzania hatua siasa.
VIONGOZI BORA: Hapa bora nisiseme sifa moja tu ambayo hata wakinuna, ndivyo walivyo na ndivyo watakavyokuwa hadi pale wathibitishe kwa vitendo kuwa wao si DHAIFU.

Hitimisho - Turudi kwenye kuthamini ELIMU ili tuondokane na njaa na maradhi. Tukielimika tutajua thamani ya CHETU badala ya CHANGU, na huo ndio uzalendo.
 
Mkuu Kichuguu,

Nimeona nianzie hapa,

Kwa watu walioshi miaka ya sitini na ile ya sabini wakati bado kuna siasa za Ujamaa na Kujitegemea, mtakubaliana nami kuwa mambo hayo hayakuwamo miongoni mwa jamii yetu. Yalianza kukua kidogo kidogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baada ya vita, na yakaua kwa kasi sana kuanzia mwishoni mwa miaka hiyo ya themanini, ambapo miaka ya leo hii tumefikia mahali ambapo ni alarming sana.

Nina maswali mawili ya kujiuliza:

(a) Ni wapi tulipokosea hadi tukajenga element mbovu hizo katika maisha yetu?

Sikuishi miaka hiyo lakini nimeelewa unacho maanisha... Naagalia driving forces zinazoijenga na kuifanya Tanzania iilivyo hivi leo. Tulikuwa na Chama kimoja Tukiite CCM ambacho kipo hadi leo na serekali yake ndiyo imeijenga hii nchi.

Nina maono kama yako akini niyaweke hivi.

CCM ya miaka kabla ya Vita Niite CCM Conservative na Hiyo iliyofuata hadi sasa Niite CCM Liberal
Kwangu mimi nivyama viwili tofauti kabisa. Kwani hiii Conservative unaweza kuuita CCM Azimio La Arusha hii Ya Wasanii wa wa sasa unaweza kuita CCM Azimio La Zanzibar! Honestly Ni vyama viwili tofauti.

Kujibu swali ?

Wapi tumekosea ni kuwa na vyama viwili ndani ya chama kimoja. AND That is illusion on the play!

Kuwa more specific wapi tumekosea ni kuwa na CCM Liberal ... Kiukweli ni CCM Hovyo Kabisa.

Tujikwamue vipi?

Ni kuhakikisha Tunakuwa na CCM Conservative katima MTIZAMO wa SASA na kuitwaa Nchi.

KIVIPI?

CCM ivunjike sasa hihi na kuwa vyama viwili ambavyo ni dhahiri. Kwa kuwa hilo haliwezekani na sioni likitokea karibuni Basi. Kitokee Chama ambacho kitakuwa Mbadala wa CCM conservative kwa mtizamo wa sasa na kuikomboa nchi katika misingi ile ile ya kujenga MAENDELEO KATIKA MISINGI YA UTU NA MAADILI YAKE.
 
Mkuu Mkandara mimi ningependa kutofautiana nawe katika hili swala la umaskini, ujinga na maradhi. Ni kweli hivi vitu viliwahi kuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu lakini kuanzia mwaka 2000 ambapo "wawekezaji" hasa katika sekta ya madini walipoanza kuingia nchini haya matatizo makubwa matatu yalitakiwa yapungue sana au kutokomea kabisa katika uso wa nchi yetu.

Tanzania si nchi maskini ni nchi yenye utajiri kubwa sana duniani. Bofya hapa: Gold Production by Country (Kilograms)
Nchi yetu inasemekana ni ya nne Africa na ya 16 duniani katika uzalishaji wa dhahabu, lakini ikija kwenye mapato ni ya mwisho kutokana na mikataba ya kifisadi iliyosainiwa na Mkapa mwaka 2000 ambayo inaendelea hadi hii leo huku kukiwepo modifications ndogo sana pamoja na kelele za Watanzania miaka nenda miaka rudi kwamba mikataba ya uchimbaji wa madini yetu ikiwemo dhahabu haina maslahi na nchi.

Tukija kwenye Tanzanite, Tanzania ni nchi pekee duniani yenye madini hayo lakini kwenye mapato ni ya nne duniani baada ya USA, India na Kenya. Hili linajulikana miaka nenda miaka rudi hivyo lingweza kabisa kufanyiwa kazi na kuziba mianya iliyopo ili Tanzania iwe nchi ya kwanza duniani yenye mapato makubwa sana yatokanayo na Tanzanite tena kwa kuziacha nchi nyingine kwa mbali sana lakini hali si hivyo.

Angalia mikataba ya gasi tulioingia na makampuni kama songa n.k. nayo imejaa wizi mtupu!!! miaka nenda miaka rudi watawala wanaliona hili lakini kwa kuwa kwa namna moja au nyingine wamehongwa na makampuni hayo basi wanalipotezea huku makampuni hayo yakiendelea kufaidi mali asili za Watanzania.

Tuna uranium pia ambapo inasemekana Tanzania ni nchi ya nane duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya madini hayo, Almasi ambayo nayo mikataba yake ni wizi mtupu!!!

Kwa hiyo utajiri huu mkubwa tuliojaliwa kama watawala wangesikia vilio vya Watanzania na hivyo kusaini mikataba yenye maslahi kwa Tanzania na Watanzania basi tungeweza kabisa kupiga hatua kubwa kimaendeleo na kuboresha sekta zetu mbali mbali ikiwemo elimu, usafiri, maji safi na pia kuongeza vipato vya Watanzania kwa kiwango cha hali ya juu na hivyo kuifanya Tanzania iwe moja ya nchi zenye maendeleo makubwa sana Afrika kama siyo duniani.

Angalia Rwanda, pamoja wahutu na watusi kuuana kwa idadi kubwa mnamo mwaka 1994 baada ya kipindi cha miaka 18 wameibadilisha nchi yao na kuweza kupiga hatua kubwa sana katika maendeleo pamoja na kuwa hawana utajiri mkubwa wa rasilimali kama Tanzania.

Viwango vya maisha vimepanda sana, huduma mbali mbali muhimu kama vile elimu, afya, usafiri upatikanaji wa maji na umeme ni wa kiwango cha juu ukilinganisha na Tanzania. Leo hii wataalamu wa Kitanzania toka nchi mbali mbali duniani wako radhi kwenda kufanya kazi Rwanda kuliko kufanya kazi nchini. Kulikoni hapa? Kama Rwanda wamepata mafanikio makubwa katika kipindi cha muda mfupi pamoja na kuwa hawana "amani" ukilinganisha na Tanzania ni kipi kinasababisha watawala wetu washindwe kwe nda kujifunza kwa watawala wa Rwanda kuhusu siri ya mafanikio yao makubwa?

Tukirudi kwenye viwango vidogo vya mishahara ambavyo sasa vimekuwa chanzo cha migomo isiyokwisha hasa ya madaktari, walimu na hata wahadhiri wa vyuo vya elimu ya juu utaona Serikali jinsi inavyotaka kutumia ubabe wa kutishia kuwafukuza kazi waliogoma na kutumia kisingizio cha "Serikali haina uwezo" wakati waheshimiwa wenyewe wanajiongezea mishahara na marupurupu ya hali ya juu kila kkukicha. Angalia hadi hii leo mishahara na marupurupu mbali mbali ya waheshimiwa ikiwemo ya Rais na Mawaziri inavyofanywa siri kubwa. Kama utakumbuka kama sikosei mwaka jana/juzi katika kikao cha bajeti ambapo Wabunge walitaka kujiongezea posho kwa kiwango cha hali ya juu Watanzania tulipinga kwa nguvu zetu zote, lakini ikija kwenye kuongeza mishahara ya walimu, madaktari, wahadhiri Serikali haikawii kutoka kauli "Serikali haina uwezo" na kutumia vitisho ili kuepusha migomo ambayo mimi naona inastahili ili wahusika wapate ujira wa kuwawezesha kufanya kazi zao kwa mioyo mikunjufu na hivyo kujituma zaidi

Kwa kumalizia napenda kurudia kwamba nchi yetu si maskini hata kidogo. Kama tungeweza/tutaweza kuingia mikataba na "wawekezaji" katika sekta ya madini (Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Uranium, Gas n.k) na kuhakikisha mianya yote ya wizi na udanganyifu inayofanywa na makampuni hayo basi umaskini, ujinga na maradhi vitakuwa historia nchi mwetu na Tanzania inaweza kuwa kioo cha maendeleo katika Africa na hata duniani.


Kichuguu,
Ndivyo Tulivyo inaambatana na ulemavu wa UTU kutokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi..Hao wote walioendelea ukitazma kwa makini wamepigab hatua kubwa sana kuondoa kwanza maadui hao ktk jamii zao. Hata tukisema Kenya wao wamesoma kuliko sisi, sii maskini kama sisi na poengine naweza sema hata vifo ni vichache zaidi kwa sababu unapoondoa Ujinga na umaskini hata maradhi na vifo pia hupungua..

Sisi kwa kuacha vita yetu, tumeingia ktk Ubepari bila Mtaji isipookuwa Kiburi, kile kiburi cha maskini jeuri na ndi maana hata tunapoomba msaada husema huwezi kunipangia nitaufanyia nini, wewe kama unanipa nipe halafu mimi nitajua la kufanya kama vile msaada ni sadaka au Zaka. Na kwa ujinga ule ule hufikiria neno MSAADA ni lina maana unapewa bure na hudaiwi wala hauna riba.

Kwa Umaskini na Ujinga tulokuja nao ktk Ubepari tumejikuta sisi wenyewe ni virusi vya maendeleo yetu wenyewe. Hatuwezi kuwa na Ethics mkuu wangu haiwezekani. Umaksini wetu ndio adui wa maendeleo yetu wenyewe. hatukurogwa wala kurudishwa nyuma zaidi ya sisi wenyewe kushindwa kujipanga kuweka mfumo bora zaidi ktk kuhakikisha Umaskini, Ujinga na maradhi vinaangamizwa..

Na Unapokuwa na kilema hicho ustaarabu nao unatoweka.. Nimeshatoa mfano zamani ya kwamba Jaribu siku moja weka makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza wapange mezani kila mtu na sahani yake ale kwa kisu na uma, halafu kundi la pili wamwagie sinia la biriani mkekani halafu uone tofauti ya jinsi watu hawa watakavyo behave ktk chakula.
Wa mkekani hawataweza kula na uma na kisu wala hata kijiko maana it's about speed, quantity na shibe..Wa mezani wakaweka ustaarabu fulani na pengine hata kuwacheka walioko mkekani, lakini hata yule mtu alokuwa mezani jana ukimweka mkekani kesho utamwona akigombania nyama na yule wa mkekani ukimweka mezani utamwona akibadilika.

Hivyo mimi na wewe mkuu wangu tumekuja huku mezani umebadilika na kuwa na ustaarabu fulani lakini tukikumwaga Bongo tu haitachukua miezi sita wewe mwenyewe utaanza kugombania biriani.. lazima utatia akili..

Uchumi wa nchi za kiafrika ni sawa kabisa na sinia la mkekani, hatukufanya maandalizi ya mageuzi ktk mfumo wa kiuchumi kwa kutazama kwanza WATU na MAZINGIRA tulokuwepo ila tuliiga tu Ubepari wa nchi za Ulaya.. Huweiz chukua watu wmaskini, wajinga na wenye matatizo makubwa ya kifaya ukawapachika mfumo wa Ulaya.. Sisi tulipigania Uhuru lakini tulichopewa ni Demokrasia hatua ambayo haikulingana na mazingira yetu..Hivyo kwetu sisi maskini hata hata kama tukiacha biriani tukawekewa vianzi vya mbatata (Fries) na kuku bado watagombania. Na yule ulomweka(msomi) Jikoni atajiona yeye ndio mwenye shughuli, mpishi na mgawaji chakula na bila shaka ataona ni haki yake kuacha chakula kingine pembeni abebe nyumbani kwake baada ya shughuli mbali kabisa na malipo alopewa.

Kwa Umaskini, Ujinga na maradhi, usitegemee kabisa kwamba kuna kujituma hapa. Sisi wote ni waaliwka tu ktk dunia hii ya demokrasia maana hatujui kilichopikwa. Zamani tulikuwa tukisisitiza zaidi Kilimo na kusema ndio uti wa mgongo, Tukipambana na Umaskini, Ujinga na maradhi lakini badala yake tukaletewa Demokrasia na ndio ikawa vita yetu kwa sababu Ulaya ndio wanachopigania na wachosisitiza. Sasa wewe nambie kwa Mtanzania maskini, mjinga na mwenye afya mbovu hii demokrasia itamsaidia nini zaidi?..Yet ukiwauliza watu wengi sasa hivi kila mtu atakwambia Demokrasia, demokrasia kaa vile UTU wa binadamu aumaendeleo ya Mtanzania yatathaminika kwa Demokrasia..

Kwa kumalizia tu ni kwamba sisi tupo ktk mfumo mbaya usolingana na WATU wala MAZINGIRA yetu..Tumeacha maadui wetu na kuvamia maadui wa nchi za magharibi na ndio maana hadi leo sisi bado ni watumwa wa kimfumo. Umaskini hautakwisha na wala Ujinga hautakwisha kkutokana na kwamba sisi tuna maradhi tofauti kabisa.. Tunaumwa Malaria wanatupa dawa za mafua kwa sababu tu mafua inaua watu wengi Ulaya nasi tumeweka vituo na karantini za matibabu ya mafua - Tutapona wapi?..
 
BAK,
Mkuu wangu uloyazungumza yote hayo yametokana na UJINGA na UMASKINI wetu.. Unajua ni rahisi sana kufikiria sisi tume elimika ama wajanja lakini siku zote ni maamuzi yetu our final decision tunazofanya ndio huashiria nini destiny yetu. Maadam umesema wazi nchi yetu maskini wakati tuna utajiri mkubwa basi bila shaka wenye tatizo ni sisi - UJINGA.. Elimu sio kwenda darasani au kushinda mitihani mkuu wangu kwa sababu wengine huenda shule kukariri na kuhifadhi waloyasoma lakini haimaanishi loote ktk matendo namaamuzi yao..

Sisi ktk Uislaam wapo watu wanakusomea msahafu mzima toka kichwani na anakwenda aya kwa yaya nukta kwa nukta bila kuacha hata herufi moja nyuma kupoteza maana. Utachoka wewe kumsikiliza na utasema ama kweli kuna watu wana vipaji..lakini ukwlei ni upi?.. ni wachache kati yao wanajua maana halisi ya aya hizo, uzito wake halafu ni wachache zaidi tena toka kundi hilo wanaotimiza yale waloyasoma na kuyasetiri kichwani au niseme mioyoni.
Pili Umaskini umechangia pia kwa sababu pengine huelewi jinsi gani Uhaba unavyoweza kuwachanganya watu akili.. Jiulize kwa nini watu hugombania kupanda Daladala? Kwa nini wakati wa Nyerere tulikuwa tukigombania kuingia sinema au foleni ya sukari ktk maduka ya RTC? - Umaskini!
Umaskini unatuweka sawa na kaa wa bahari walowekwa ktk kapu au tenga la mvuvi. Kaa hushindwa kutoka nje kwa sababu kila mmoja wao hujaribu atoke yeye kwanza akimvuta mwenzake chini.. Umaskini huteka hata akili za watu ni kama meli imezama, hofu mnayokuwa nayo ku survive ni wachache wanaoweza kufikiria vizuri..

Na ndio maana nimetoa mfano wa watu wanaogombania chakula ukiwawekea ktk sinia mkekani.. Hii ni njia za ku control mind set za watu wafikirie kwamba bila wao hamtaweza kula, bila wao hamtapata next meal na ndivyo nchi za magharibi zimetuweka ktk nafasi hiyo ya Umaskini na kutumia UHABA kutuendesha ktk umaskini na wanafurahia sana tunapogombania mali kama inavyotokea Kongo.

Unafikri hawajui kwamba Congo RDC wameisha kufa watu zaidi ya millioni 5 toka vita vianze? Wanajua sana lakini who cares?. Wao wanataka tuendelee kuuana wakati wao wanaiba madini yao, Na stupid enough Wazaire au wakongo wenyewe wanafikiri Americans do care! Leo wameshasau kabisa Mobutu aliingiaje halafu ilitokaje na leo watataka iweje?. Huu Uzoba wa kusahau, kupuuza na kufikiria its a fair game sijui a win win situation ndio Ujinga wenyewe.

- Kichuguu nipe muda natengeneza kitu cha kututoa shimoni..
 
Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama asali, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amrbski hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?

Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.

Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.
Kwanza lazima nikushukuru kwa kunielewa niloyaandika hapo nyuma na utata wa hali na maisha yetu kwa ujumla... Na kusema kweli sisi tuko ktk serious trouble economically na sidhani kama viongozi wanaelewa uzito wa janga hili.

Pamoja na wao kutoelewa, ama wanaelewa na wanafanya makusudi inatupa shida pia kuelwa kama vyama vya Upinzani nao wanasikia harufu, karaha na mateso ya shimoni ama hutetea walioko shimoni wakati wao bado wamesimama nje ya shimo hilo.. maana tuukubali ukweli kwamba baada ya Dr.Slaa na uchaguzi wa mwaka 2010 harakati za mageuzi zinafanywa sana na wananchi kuliko vyama vya Upinzani. Vyama vimekuwa vikiendesha zaidi siasa ya majitaka wakati wananchi wanaendelea kuumia.. Na kwa kiburi na jeuri zile zile za umaskini na ujinga wamekuwa hata majibu yao sii ya kuridhisha..

Yawezekana kabisa migomo ya madaktari, Walimu na Machinga waking'ang'ania sehemu tu ya wananchi waliokwisha kosa tumaini hata kupitia vyama vya siasa hivyo kuchukua mamlaka mikononi mwao. Na ndio maana seriikali hudai migomo hii kuwa kinyume cha sheria.. sijui ni sheria gani hapa inatumika..

Hivyo Makundi ya wanaharakati wa Change Tanzania, M4C na hata Uamsho ni dalili kubwa ya kuonyesha wananchi wamechoshwa na mfumo dhalimu wa kiutawala ambao unaendelea kuweka rasilimali na urithi wao rehani. Na kwa ujumla wetu sisi wote ndio mageuzi yanayotakiwa kutokea na sii kusubiri Chadema, CUF au NCCR kwa sababu sasa hivi siasa imekuwa sehemu ya maisha na uhai wetu. Nguvu ya Chadema inatokana na kwamba wao wanakubaliana na madai ya wananchi lakini hali iliyopo haikutoka kwao na hii inaweza kuwa dalili mbaya zaidi kwa chama tawala.

Kuna njia mbili muhimu sana za kutuwezesha sisi kuondoka ktk shimo hili la taka..hatuwezi kusubiri mageuzi kutoka sanduku la kura kwa sababu CCM na viongozi walotuweka hapa tayari wapo ktk maandalizi ya kuhakikisha tunabakia tulipo. Tukumbuke tu kwamba haya ndio maisha yao, ufisadi ndio unawaweka mjini ama niseme hapo walipo na hawatakubali kuondoka kwa gharama yoyote ile kwa sababu wanayoyafanya ni dhulma...

Aidha serikali iliyopo ikubali kubadilisha mfumo wake kabisa kiuongozi.. Nimeshangaa sana na kushtuka kwa hotuba ya waziri wa nishati na madini Profesa Muhongo ambaye amezungumza maneno mazito sana utafiri rais,.. Ilifikia mahala nikasema wow! huyu ndio kiongozi tunayemtaka. Kiongozi mwenye vision, spirit na aliyetayari kuchukua lawama zote lakini kuhakikisha Tanesco inafanya kazi ipaswavyo...Again huyu ni waziri tu ambaye anaweza kusema yote hayo lakini nyuma ya Pazia kuna siri kubwa ilojificha, hata hivyo nampa benefit of the doubt inabidi tuanze kuaminiana.

Na ukimsikiliza kwa makini alichodai ni kusimamisha MIIKO na MAADILI halafu SHERIA ichukue mkondo wake. Kuna watu waliosema tunatakiwa kuwa na sheria tu bila miiko na maadili lakini ndio yale yale ya Mahalkama ya kadhi kutaka kuwapa watu haki zao wakati miiko na maadili ya imani ya dini yanakiukwa..Simamisheni miiko na maadili, watu watafuata hizo ethics tunazozidai na itakuwa rahisi hata kutoa hukumu za haki maana imekatazwa na tumelazimika kufanya kadhaa wa kadhaa na hivyo kuiheshimu sheria.. Huwezi kuwahukumu watu na sheria pasipo kuwepo miiko na maadili hizo sheria zitajengwa vipi?. Kwa hiyo basi turudishe MIIKO na MAADILI badala ya kuwa na tume za maadili sijui kuchunguza vitu gani..
 
BAK

Swala ulioongelea na kutumia mfano wa Rwanda ndilo hilo nilaozungumza kuwa Watanzania hatuna maadili ya kazi zetu (Viongozi kusaini mikataba ya hovyo ni kutokana na kukosa maadili), Watanzania hatukubali kuwajibika kwa makosa yetu na wala hatuko tayari kuwawajibisha wanofanya makosa dhidi ya umma (ndiyo maana pamoja na kujua kuwa viongozi wetu hawafanyi kazi zao ipasavyo, bado hatuwawajibishi.) Tumeshuhudia nchi nyingine nyingi duniani wananchi wakiwawajibisha viongozi wao kwa nguvu kwa kupitia ama uprising au kwa kuwanyima kura, sisi huo ni mwiko!
 
Last edited by a moderator:
Nzi,

Mfumo unaojulicana kama "mixed economy" yaani mchanganyiko wa ujamaa na ubepari ndio mfumo uliozikomboa nchi nyingi sana duniani hasa huko Asia. Serikali inasimamia maswala ya elimu, huduma za afya, na kumilik biashara nyeti kwa taifa kama mali asili, nishati, na njia kuu za usafirishaji kama treni, usafiri wa anga huku ikiwahimiza raia wake (siyo raia wa nje) kuwekekaza katika biashara hizo. Wakati huo huo ikiwaachia watu binafsi wajifanyie biashara zao nyinginezo.

Ma-giants wote wa uchumi huko Asia: Singapore, Taiwan, China, Korea, na Japan walifanya hivyo. Sehemu nyingi za skandinavia zinaendesha uchumi wa namna hiyo hadi leo, na Hata Australia nayo inafuata uchumi wa aina hiyo hiyo.

Je Tanzania tuchukue hatua gani ili kurudi kwenye uchumi huo iwapo viongozi wetu walishasaini mikataba ya miaka 99 na makampuni ya nje?
 
Azimio Jipya

Nadhani hicho kitu CCM Conservative hakipo kabisa; hebu angalia tena CCM-CC na CCM-NEC, ni watu gani unaodhani wanarepresent hiyo CCM Conservative?
 
Last edited by a moderator:
Mkandara

Ukweli wa mambo ni kuwa kutokana na mfumo mbovu uliokwisha jengeka kwenye jamii yetu mabadiliko yanaweza kutokea kwa hatari pia. Iwapo tu raia kuandamana ikiwa na haki yao ya kikatiba wanapigwa risasi na kuuwawa tena mchana kweupe na vyombo ambavyo jukumu lake ni kulinda na kutunza usalama wa raia, unadhani kweli serikali inayolindwa na vyombo vya namna hiyo itakubali mabadiliko?

Unaonaje iwapo outsider huyo ndani ya serikali ndiye akitumika kuchochea mabadiliko hayo? (I am just wondering). Outsider huyo akipewa madaraka makubwa zaidi kama uwaziri mkuu, je unadhani ataendelea na moto huo huo siku zote, au akishasettle atasahahu na kurudi tulikotoka? Tumewahi kuwa na wabunge vocal sana kuishambulia serikali na "kuwatetea wananchi" lakini walipopwea uwaziri mdogo tu wakawa ndio wanaongoza kwa ufisiadi. Kwa tabia yetu watanzania huwa hatuna 'sustained effort,' tuna kitu kinajulikana "nguvu ya soda" tu, au nguvu ya upepo tu utapita.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara

Ukweli wa mambo ni kuwa kutokana na mfumo mbovu uliokwisha jengeka kwenye jamii yetu mabadiliko yanaweza kutokea kwa hatari pia. Iwapo tu raia kuandamana ikiwa na haki yao ya kikatiba wanapigwa risasi na kuuwawa tena mchana kweupe na vyombo ambavyo jukumu lake ni kulinda na kutunza usalama wa raia, unadhani kweli serikali inayolindwa na vyombo vya namna hiyo itakubali mabadiliko?

Unaonaje iwapo outsider huyo ndani ya serikali ndiye akitumika kuchochea mabadiliko hayo? (I am just wondering). Outsider huyo akipewa madaraka makubwa zaidi kama uwaziri mkuu, je unadhani ataendelea na moto huo huo siku zote, au akishasettle atasahahu na kurudi tulikotoka? Tumewahi kuwa na wabunge vocal sana kuishambulia serikali na "kuwatetea wananchi" lakini walipopwea uwaziri mdogo tu wakawa ndio wanaongoza kwa ufisiadi. Kwa tabia yetu watanzania huwa hatuna 'sustained effort,' tuna kitu kinajulikana "nguvu ya soda" tu, au nguvu ya upepo tu utapita.
Kusema kwlei binafsi yangu sina hope tena baada ya Dr.Slaa pengine sijui mipango ya Chadema lakini kutoka ndnai ya CCM sina hakika maana tayari najua kinachokuja..Wapo watu wanao amini kila kitu kina mwisho.. Well Afrika tulikoloniwa kwa zaidi ya miaka 500, are ready to wait that long?.

Kuhusu Outsider mkuu wangu kwa Bongo yetu unahitaji kukaa miezi sita tu wewe mwenyewe utabadilika maana huyo mtu naye atatupwa aidha ndani ya shimo na kukoromea huko au atawekwa meza kubwa na hatayajua na mkekani. Ndio yale niloyasema mwanzo.. Mageuzi ya kweli Tanzania yatatoka kwa wananchi wenyewe, pengine kwa kuisisitiza serikali ifanye wanayoyataka isipokuwa hofu yangu ni umoja wa kaa inaelekea ndivyo tulivyo kutokana na umaskini na Ujinga..

Kwa leo CCM wanafikiri kuna uchochezi kutoka Chadema au CUF lakini binafis yangu nimegundua ya kwamba wananchi wamechoka na wanataka mageuzi leo kama sio leo kesho hawajali tena support ya Chadema CUf wala mwansiasa yeyote. Ni juu ya JK kulitazama hili lakini inaelekea mwisho wake sii mzuri na itasikitisha sana anaweza kuondoka kama rais anayechukiwa kuliko wote while I think JK katupa uhuru mkubwa sana..
 
Mfumo unaojulicana kama "mixed economy" yaani mchanganyiko wa ujamaa na ubepari ndio mfumo uliozikomboa nchi nyingi sana duniani hasa huko Asia. Serikali inasimamia maswala ya elimu, huduma za afya, na kumilik biashara nyeti kwa taifa kama mali asili, nishati, na njia kuu za usafirishaji kama treni, usafiri wa anga huku ikiwahimiza raia wake (siyo raia wa nje) kuwekekaza katika biashara hizo. Wakati huo huo ikiwaachia watu binafsi wajifanyie biashara zao nyinginezo.
Kichuguu,

...Tatizo sio mfumo wa uchumi, bali ni kujiongopea na kukubali kuongopewa. Pale Mwl. Nyerere aliposema waTanzania ni wajamaa -na kuukumbatia u african socialism- alikuwa anamwongopea nani? Kila kitu alisema waTanzania wameamua. Je, kuna kura ya maoni ilipigwa?

...Hata sasa, utasikia watu wanasema ....."serikali yetu sikivu". Wanamwongopea nani? Hebu waulize walimu kuhusu hili.

...Tukiacha huu uongo, tutakuwa tumeanza kuelekea tunakotakiwa kwenda, kiuchumi and otherwise.
 
Kichuguu,

...Tatizo sio mfumo wa uchumi, bali ni kujiongopea na kukubali kuongopewa. Pale Mwl. Nyerere aliposema waTanzania ni wajamaa -na kuukumbatia u african socialism- alikuwa anamwongopea nani? Kila kitu alisema waTanzania wameamua. Je, kuna kura ya maoni ilipigwa?

...Hata sasa, utasikia watu wanasema ....."serikali yetu sikivu". Wanamwongopea nani? Hebu waulize walimu kuhusu hili.

...Tukiacha huu uongo, tutakuwa tumeanza kuelekea tunakotakiwa kwenda, kiuchumi and otherwise.

Nakubaliana nawe kuwa tumjenga mfumo wa utawala ambamo tunaongopeana, ila naona ugumu wa kukubaliana nawe unasema kuwa Nyerere alisema kuwa Tanzania ni wajamaa.

Binafsi nilikuwa mwanafunzi wa siasa za Nyerere kwa karibu sana kwa vile nilikuwa natayarishwa kuwa afisa wa jeshi la wananchi, ingawa baadaye haikuwa hivyo. Katika utawala wa Nyerere, alikuwa akihimiza kuwa tunataka kujenga taifa la kijamaa na wala hakusema kuwa Tanzania ni wajamaa, na hata pale alipotoa ile hotuba ya siwezi kugeuka jiwe alikuwa akisema kuwa huenda tunakaribia kuwa wajamaa ndiyo maana tunapata misukosuko ili tukigeuka nyuma tuwe mawe. Ukiweza kupata nakala ya Africa Now ya mwaka 1983, utakutana na ile interview yake aliyofanya na mwandishi Peter Enahoro. Katika interview ile alikiri kabisa kuwa kujenga taifa la kijamaa kuna vikwazo viongi sana na wala hatujafika hapo.

Vile vile sikubaliani nawe kuhusu madai ya kuulizia kura za maoni wakati huo kama ambavyo wapinzani wa kila jambo aliloasisi nyerere wamekuwa wakidai. Sera zote zilizotokea Tanzania miaka hiyo zilikuwa zinapitishwa na organs halali zilizokuwa zinawakilisha wananchi kwa mujibu wa katiba iliyokuwapo. Vikao hivyo vilikuwa vikifanyika kwa mujibu wa sheria za nchi zilizokuwapo wakati huo. Inawezekana katiba ya nchi na sheria za wakati huo vilikuwa na mapungufu lakini katika sheria huwezi kutunga sheria leo halafu ukaitumia kuhukumu makosa ya mwaka jana.

Mwisho, turudi kwenye maswali yangu, ni wapi tulipokosea hadi kupoteza sifa muhimu za utu nilioztaja hapo juu, na tufanyeje kujiondoa. Kulaumu maamuzi ya mwaka 1960 ni kujirudisha kwenye sifa hiyo hiyo niliyosema kuwa watanzania hatutaki kuchukua responsibility, kila wakati tunatafuta mtu mweingine wa kulaumu, na tunapomkosa, basi tunasingizia Mungu. Nyerere (RIP) amekuwa ni scapogat rahisi sana kwetu kutumia lakini kwa vile katanguliea mbele ya shria hatuwezi kubaki tukilia na Nyerere badala ya kutafuta namna ya kujiendeleza.
 
Sera zote zilizotokea Tanzania miaka hiyo zilikuwa zinapitishwa na organs halali zilizokuwa zinawakilisha wananchi kwa mujibu wa katiba iliyokuwapo. Vikao hivyo vilikuwa vikifanyika kwa mujibu wa sheria za nchi zilizokuwapo wakati huo.
...I doubt this. Na utamaduni huu umeendelea toka kipindi kile. Kumbuka fikra za mwenyekiti zilikuwa "sahihi". I very much respect and admire Mwl. but that doesn't make me blind to the facts.

...Tunahitaji kurudi nyuma mpaka kipindi chake cha uongozi, kujua tusonge vipi mbele.
Kulaumu maamuzi ya mwaka 1960 ni kujirudisha kwenye sifa hiyo hiyo niliyosema kuwa watanzania hatutaki kuchukua responsibility, kila wakati tunatafuta mtu mweingine wa kulaumu, na tunapomkosa, basi tunasingizia Mungu. Nyerere (RIP) amekuwa ni scapogat rahisi sana kwetu kutumia lakini kwa vile katanguliea mbele ya shria hatuwezi kubaki tukilia na Nyerere badala ya kutafuta namna ya kujiendeleza.
...Kuonyesha baadhi ya mambo yaliyotufikisha hapa tulipo si kulaumu bali kubaini upungufu na kujifunza. Mwl. atatumika kama rejea -katika mambo mbalimbali- siku zote za maisha ya Jamhuri hii. Na wanaomfanya scapegoat wamepotoka! Simply, we learn from mistakes, or we don't learn at all.

...Kujibu swali lako la msingi, ni kwamba, tunahitaji viongozi bora -in the fullest sense of the word- na si bora viongozi. Hawa, watakuwa ni watu wanaoweza kujifunza kutokana na makosa waliyofanya viongozi waliopita kabla yao. Its basics my friend, basics!
 
...I doubt this. Na utamaduni huu umeendelea toka kipindi kile. Kumbuka fikra za mwenyekiti zilikuwa "sahihi". I very much respect and admire Mwl. but that doesn't make me blind to the facts.
Hiyo doubt uliyo nayo kuhusu ukweli huo ndiyo inayoondoa uzito wa hoja yako. Angalia kuwa Azimio la Arusha lilipitishwa na kikao halali cha TANU wakati huo na kupitishwa kwa pamoja pale kwenye mkutano wa Arusha chini ya misingi iliyokuwapo kihalali. Baadaye ukafuatia Mwongozo wa TANU uliotoka mwaka 1971 pale Dar es Salaama na kupitishwa na kikao halali kilichokuwa kinatambuliwa kikatiba; kuna maamuzi mengine kama Siasa ni Kilimo, Mtu ni Afaya, Azimio la Musoma na mengineyo yaliyofuatia; yote yalikuwa halali katika mazingira yale. Hebu angalia swala hilo intellectually kama unaweza kuona uharamu wa maamuzi yale kisheria uuonyeshe.

Nimekubaliana nawe kuhusiana na mapungufu ya katiba wakati huo na hivyo namna ambavyo katiba hiyo ilivyokuwa inaruhusu vikao hivyo kupitisha maamuzi dhaifu; hata hivyo mapungufu hayo hayawezi kufanya maamuzi yaliyofanyika wakati huo yasiwe halali. Kilichotokea ni kuwa system yetu ya utawala mwanzoni ilikuwa na mapungufu ikiwa ni pamoja na kutoruhusu challenge kwa kuwa tulikuwa chini ya chama kimoja. Tatizo hilo tumeshaliondoa miongonii mwetu takribani miaka 20 sasa tangu tulipoanzisha vyama vingi. Tulianza kufungulia milango ya kupishana mawazo tangu mwaka 1992 hata kabla ya mauaji ya Rwanda. Kwa nini tuendelee leo kulalamikia jambo hilo? Viongozi wote tulio nao leo hii isipokuwa Malecela na Kingunge hawakuwapo wakati wa TANU lakini bado wanafanya mambo ambayo in fact yalikuwa hayafanyiki wakati wa TANU. Kwanza kama ulikuwapo wakati wa utawala huo wa TANU sidhani kama kweli una ushahidi wowote wa kuonyesha kuwa kulikuwa na viongozi wa serikali au TANU ambao walikuwa wakifanya kama ambavyo leo tunavyofanya kazi zetu. Mwaka 1972 mshahara wa kima cha chini ulikuwa ni Sh 160 wala hakukuwa na rushwa, wizi au uzembe wowote kwenye taasisi za umma.

Hata kama maamuzi yaliyokuwa chini ya TANU yalikuwa na upungufu lakini je ni kweli kuwa yalichochea viongozi wa serikali kuwa wanachukua rushwa kutoka makapuni ya madini na kufungua account huko Uswiss? au hii tabia yetu ya leo kutokujali ethics za kazi. Na iwapo hailo ni kweli, TANU haipo tena, na maamuzi yote yaliyofanywa na TANU hayapo kabisa katika maisha yetu ya kila siku: hakuna ujamaa, hakuna Azimio la Arusa na wala hakuna zidumu fikra za mwenyekiti, lakini ndiyo tunazidi kwenda Kombo. Tatizo halisi liko wapi? Na tutalitatua vipi?


NYONGEZA: Nona tunaweza tunaishia kwenda nje ya mada kwa kuanza kujadiliana maamuzi ya zamani. Nakumbusha tena kuwa nilikubalina nawe kuwa mfumo wa utawala wa kuongopeana pia umechangia kutufikisha hapa; kwa mfano serikali inaposema kuwa hina fedha kwa hiyo haiwezi kutekeleza majukumu yake huku ikiwa na pesa nyingi za kuchezea tu. Je tuuonde vipi mfumo huo?
 
Ukiwa na mfumo fulani wa maisha na miongozo yake hutumika ili kuleta/kufikia malengo ya mfumo huo............kilichotokea hapa kwetu ni kuwa tumebadili mfumo....lakini miongozo ni mfumo wa zamani.....kwa hiyo utakuta watu wanatumia miongozo ya zamani kama stepping stone........halafu wanatumia katika mfumo wa sasa..............matokeo yake ndio hayo matatizo uliyoya-ainisha..........

Tatizo lililopo sasa ni kuwa wale wanaofaidika na mfumo ulivyo sasa wana nguvu za ajabu........na wanatununua watanzania kw abei rahisi sana........wakitokea akina "Kichuguu" na mapendekezo ambayoni kwa manufaa ya Taifa utaona utavyopigwa vita.....mara wewe unatuletea sera za Mwl JKN (RIP) ambazo zilifeli etc etc.........ili mradi tu kuufisha mjadala ili usilete mabadiliko yoyote...........

Hivi sasa tupo kwenye mchakato wa Katiba............huu ni wakati mzuri wa kuiweka katiba yetu na ikatupa miongozo inayofaa kwa hali tuliyo nayo sasa..........

Inabidi tubadilike......na kubadilika huku inabidi tubadilike kweli kweli...........na tuukubali ukweli......kwa mfano......kwa nini Waziri alzima awe Mbunge?..........au kwanini ukitaka kuwa mbunge lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa?....au kwa nini ukiwa Mbunge basi ndio imetoka hiyo mpaka miaka mitano ipite...........yaani assume Mbunge anaboronga....inabidi wananchi wasubiri either Mbunge huyo afe au mpaka miaka mitano ipite....nguvu ya wananchi iko wapi? ndio maana nasema hizi demokrasia zingine za ku-copy zinatupeleka kusiko........

Katika Nchi yetu Chama Tawala au kitakacho tawala kiko powerful kuliko.....nguvu ya wananchi....that is WRONG!......ushiriki wa wananchi kwa masuala ya maendeleo yao ni mdogo sana.......utawala uliopo wa sasa zaidi wanacho fanya ni ku-impose.........sustainability...zero! kuna maprogram na maprogram.....lakini kama uanzishwaji wa maprogram hayo hayakuwashirikisha wananchi toka mwanzo......matokeo yake huzaa white elephant projects

Hatuna ethics na ni wavivu kwa sababu........hatuna standards tunazosimamia and/or performance oriented standards and administrations...watu wanaenda ofisini wamechelewa, wakifika wanapiga gumzo, ofisi zimekuwa mahala pa umbeya na kufanya biashara binafsi.....
 
Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama nyuki, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amebaki hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?

Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.

Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.

Mwl Kichuguu,
BTW.......unakumbuka tuliwahi kuwa na mijadala ya namna hii......na kuna sehemu tulifika kwenye ule mjadala tukaona tunachokosa ni Katiba inayokidhi yale tuyatakayo kama nchi..............tukaanza mchakato wa kukusanya maoni na mapendekezo yetu.....yaliyotokana na ule mjadala katiba ikiwemo......mpaka ikawekwa electronic copy ya katiba........tena nakumbuka wewe ulijitolea kuhariri maoni......hivi ile kazi iliishia wapi......au ndio matatizo yenyewe tuliyonayo?
 
Back
Top Bottom