Tulimchukia Hayati Magufuli bila sababu za msingi, sasa tumetambua kuwa alikuwa sahihi, yanayofanyika sasa ni aibu

Tulimchukia Hayati Magufuli bila sababu za msingi, sasa tumetambua kuwa alikuwa sahihi, yanayofanyika sasa ni aibu

Mwananchi anayesoma Uzi huu na mada yeyote ile iliyoibuka na msamiati wa kuwabeza kabila la Wasukuma. Muelewe hawa ni mamluki waliojichimbia hapa kufanya siasa za uchonganishi na utenganishi....Kama ni kweli wanampinga mleta mada? kwanini wasingeleta Uzi au Mada za Kumpinga na Kumzodoa Tundu Lissu na alichokisema kuhusu Hayati na suala hili la Bandari? Muwasome na kuwaelewa. Hawako humu kutetea maslahi ya Mtanzania hata kidogo, bali kuendeleza mashambulizi ya kisaikilojia kuwa Watanzania hatuwezi, kuwa Falsafa ya Kujitegemea(economic independence) ni mbovu! Hawa ndio waliomchanganya SSH na washauri wake. Mabeberu wote wana nia moja nayo ni kututawala.
 
Ukweli ni kuwa kwenye misingi madhubuti ya kudhibiti rushwa , mikataba mibovu na upigaji wa ajabu ajabu hayati alinyoosha hii nchi. Maana tulianza kusahau haya maugoro.

Sisi sababu tulishazoea janjanjanja hasa Mbowe na baadhi ya makamanda tukachukia. Tukawa tunahitaji wajanja wakae madarakani.

Leo hii tunashuhudia madudu ambayo yanamuumiza mwannanchi wa kawaida huku Vigogo wa CCM wakifurahia .

Inaumiza sana
Upande wangu jpm hakustaili kuwa rais wa nchi kwa sababu maovu aliyokuwa nayo
 
Umegusia jambo lenye mantiki kidogo, lakini ulipoweka ugoro wako nilionukuu hapa chini kutoka katika mada yako, umeharibu kila kitu.
R.i.p Magufuli
"Sisi sababu tulishazoea janja janja hasa Mbowe na baadhi ya makamanda tukachukia. Tukawa tunahitaji wajanja wakae madarakani"
 
Ukweli ni kuwa kwenye misingi madhubuti ya kudhibiti rushwa , mikataba mibovu na upigaji wa ajabu ajabu hayati alinyoosha hii nchi. Maana tulianza kusahau haya maugoro...
Kuwa specific hapo yanawaumiza wananchi unataka kusema maisha yetu yalikuwa bora kuliko sasa? kuwa specific ni wapi tulikuwa na maisha bora na wapi tumeshuka tusiweke statement za kijumla. Katika kila utawala kuna wanufaika na kuhasarika lakini weka wazi mwananchi wa kawaida tu ni lini alikuwa na maisha bora?
 
Ukweli ni kuwa kwenye misingi madhubuti ya kudhibiti rushwa , mikataba mibovu na upigaji wa ajabu ajabu hayati alinyoosha hii nchi. Maana tulianza kusahau haya maugoro.

Sisi sababu tulishazoea janjanjanja hasa Mbowe na baadhi ya makamanda tukachukia. Tukawa tunahitaji wajanja wakae madarakani.

Leo hii tunashuhudia madudu ambayo yanamuumiza mwannanchi wa kawaida huku Vigogo wa CCM wakifurahia .

Inaumiza sana
Yaani we unaona Mshenzi yule alikuwa sahihi kutuletea aina ya wabunge hawa!
Ht wewe hauko sawa
 
Magufuli alituchapa viboko tukiwa ndani ya ardhi yetu kwa muda, huyu wa sasa ametuletea nyapara wajomba zake toka Arabuni waje kutuchapa viboko ndani ya ardhi yetu milele.

Kwa hali hii kumkumbuka Magufuli ni haki.
Mchukueni Gwajima mwende mkamfufue
 
Vision ya kuuza nchi kwa Waarabu Dubai ni vision?
Nyumbu mfata mkumbo. Hiyo nchi iliyo uzwa ni ipi? Na imeuzwa kwa shilingi ngapi? Nchi siyo nyanya au bamia iuzwe.

Hivi leo mmesahau ya Ben saanane, Lisu kupigwa risasi, watu kuokotwa kwenye viroba,

uwanja wa ndege chato, mtu mmoja kufanya manunuzi ya ndege.
 
Mkataba wa bandari haufai na bado haumtakatishi magufuli mambo mabaya yaliyofanywa na Magu hayatasahaulika na hata mazuri yake hayatasahaulika
 
Ukweli ni kuwa kwenye misingi madhubuti ya kudhibiti rushwa , mikataba mibovu na upigaji wa ajabu ajabu hayati alinyoosha hii nchi. Maana tulianza kusahau haya maugoro.

Sisi sababu tulishazoea janjanjanja hasa Mbowe na baadhi ya makamanda tukachukia. Tukawa tunahitaji wajanja wakae madarakani.

Leo hii tunashuhudia madudu ambayo yanamuumiza mwannanchi wa kawaida huku Vigogo wa CCM wakifurahia .

Inaumiza sana
Yaani ilitegemea Mtu anyang'anye watu uhai halafu apendwe Kwa Hilo? Magufuli alikuwa na mazuri yake na Mbowe amekuwa amiyasema mara Kwa mara na hata Lissu kayarudia. Lakini aliporuhusu watu wasio na hatia kuuliwa Kwa kisingizio cha kutofautiana misimamo alijitengenezea chuki mwenyewe.
Tunakumbuka lawama za Watanzania dhidi ya madaktari wakati mgomo wao kipindi cha Kikwete, lakini aliporuhusu kutekwa mateso dhidi ya Dr Ulimboka watu wakamchukia yeye.
 
Unaweza kuwataja hao walionyang'anywa uhai na Magufuli na ni wangapi wameuawa na tawala zilizopita mbona hauongei hivi na ukiwataja weka ushahidi Magufuli alihusika vifo vyao sio unaongea unafiki na propaganda zenye influence za chuki wewe sema unachomchukia Magufuli kama alikutumbua vyeti feki usidanganye watu mambo ya uhai hakuna ushahidi Magufuli aliua mtu mlitumia hii propaganda kumchafua kisiasa nyie vyeti feki na mafisadi na walamba asali
 
Back
Top Bottom