Tulimkosoa Hayati Magufuli na sasa tutamkosoa Rais Samia. Kama mtaumia poleni sana Tanzania Kwanza

Tulimkosoa Hayati Magufuli na sasa tutamkosoa Rais Samia. Kama mtaumia poleni sana Tanzania Kwanza

Mwendawazimu kawavurugia sana CCM, Samia kazi anayo..
Wameparaganyika sana, kumtuliza mwanaccm kwa sasa lazima umuonge teuzi. yetu macho😂😂😂
🤣🤣🤣 wachatu Mkuu wamefura ile mbaya wanazunguuka zunguuka tu Dodoma na vikao vya kahawa......
 
Nimekuelewa kabisa Mkuu tupo pamoja. Akikosea lazima tumkosoe Tumeweza kumkosoa Mwenda zake tushindwe wajawo kuwakosoa
 
Mi naona amekaa zaidi kusherehekea urais na kuwaringishia wanawake wengine. Hajakaa kikazi. Pia ana mwelekeo wa ubadhirifu tofauti na magufuli.

Juzi kampa rais mstaafu benz eti zawadi ya kuzaliwa. Jana anamtupia mwimbaji zawadi manoti ya shilingi kumikumi mengi karibu milioni nzima utafikiri ni wale mapedeje wa matumizi ya ovyo.
 
Kuna watu wanataka kuuaminisha Umma kuwa Rais Samia Suluhu hakosei.

Hawa watu kwa kuendelea na upuuzi ule ule kwa waliokuwa wanazi na mashabiki wa Magufuli ambao nao walikuwa wanataka kuuaminisha Umma kuwa hakuwa akikosea.

Watanzania wengi wanajikita katika Ushabiki, Mahaba, Jazba, Mihemko na Ashki hata katika mambo ya msingi ya Kitaifa.

Kwa sasa limeibuka kundi la watu ambalo ukimkosoa tu Rais Samia unaonekana ulifaidika na utawala wa Magufuli. To hell.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
Ni muendelezo wa kutumia matumbo kufikiri toka miaka na miaka tunaposhindwa kukemea ubovu kwa kuamua ku side na waovu kwa kuangalia kabila,dini,chama,jinsia,dhehebu n.k

Mimi nitasimama kama Mtanzania hawa wote watapita Tanzania itabaki. Tutamkosoa Samia na akija Mwingine akakosea tutamkosoa kama ambavyo tulimkosoa Kikwete na Magufuli pia.

Na atakayefanya vizuri tutampongeza kwa mazuri yake.
Katika dhana ya kukosoa, kuna mawili! mosi, unaweza ukamkosoa mtu kwa kutumia mtu mwingine kama reference yako. Mfano yawezekana wewe ulikowa ni mfuasi wa Raisi aliyepita. Ukaona Raisi SSH anaenda kinyume na sera za aliye pita apo utakosoa. Hakuna tatizo ila lazima ujiandae kupingwa na kundi kubwa ambalo litatumia bad reference za huyo kipenzi chako kumtetea aliyepo madarakani. Mfano, sera kama za haki, biashara, uchumi, umeme, uhuru, usawa, nk, utakosoa kipi kwa SSH amabacho unaona hatatendea haki? Ni lazima upingwe tu!. Dhana ya pili ni kukosoa bila ya kuwa na reference kichwani mwako. Ukosoaji wa namna hii mara nyingi unakuwa wa haki, humjudge mtu kulingana na performance za mtu fulani aliyepita, hivyo ukikosoa apo unaweza kuachwa ukakosoa na pendine ukapata few followers. Kumalizia ni hivi, Mh Raisi SSH, haja fanya lolote la kuwafanya critical thinkers, wanaharakati, wapenda haki, au watetezi wa haki za binadamu kumpinga nk. Nimuonavyo mm, ni mcha mungu , Mama mzazi mwenye roho nzuri, mpenda haki, usawa, uhuru na amani kwa watu wote. mtenda haki kwa wote na hatafanya mambo yatakayo wakera wengi except wale wanazi wasiopenda uhuru wa watu, haki na amani.
 
Kukosoana kunaleta tija hasa ikiwa kukosoa kunapokuwa sahihi, kutoka kwa mtu sahihi, kuhusu jambo sahihi kwa mtu sahihi. Tatizo linakuja sio kila kitu kinakosolewa.

Ndio maana Hayati hakupenda kukosolewa kwa sababu waliokosoa hawakukosoa kwa murua na heshima bali vilikosolewa hata visivyohitaji kukosolewa.

Mama kama kiongozi wa serikali anaweza akakosoa hivyo kukosolewa kunatarajiwa, lakini tukosoe kwa adabu, heshima na kuzingatia hadhi ya cheo chake. Na pia tukosoe vyenye tija..

Acha nicheke tu, hiyo lugha ya kusema kukosoa kwa staha na lugha ya adabu, imekuwa ikitumika sana kukwepa kuhojiwa wala kukosolewa. Na ukitumia hiyo lugha inayoitwa ya kistaarabu hakuna mtu atawajibika. Huyo hayati unayemsema hakuwa anataka kukosolewa kwa aina yoyote, iwe ya staha wala ya ukali. In short hakustahili kuwa rais kutokana na mapungufu yake. Ajabu aliyekuwa anataka kukosolewa kwa staha, alikuwa anawadhalilisha wengine bila kujali hiyo staha!
 
Mzee Kikwete aliruhusu kukosolewa na mambo yakawa werawera. Probably na Madam yupo hivyo nimeona ishara yake...!
 
Mi naona amekaa zaidi kusherehekea urais na kuwaringishia wanawake wengine. Hajakaa kikazi. Pia ana mwelekeo wa ubadhirifu tofauti na magufuli.

Juzi kampa rais mstaafu benz eti zawadi ya kuzaliwa. Jana anamtupia mwimbaji zawadi manoti ya shilingi kumikumi mengi karibu milioni nzima utafikiri ni wale mapedeje wa matumizi ya ovyo.

Nimeona hapo kuwa amekaa kimwelekeo wa kiubadhirifu tofauti na Magufuli, kisha nikakumbuka uwanja wa ndege huko Chato ulioanza kumea nyasi kwa kasi, nimekudharau vibaya sana.
 
Nyie mliefkia level za kimataifa kwa kusifu hadi mnamwita binadamu mwenzenu Mungu hamkuona hizi kufuru eeh?kaeni kwa kutulia tunajenga Nchi ss iv hatuna muda wa kupoteza
 
Nyie mliefkia level za kimataifa kwa kusifu hadi mnamwita binadamu mwenzenu Mungu hamkuona hizi kufuru eeh?kaeni kwa kutulia tunajenga Nchi ss iv hatuna muda wa kupoteza
Well said Mkuu....
 
Yaa
Yaan yapo majitu yanakera sanaa,ukimwambia atuoneshe hata clp moja tu mwendazake akikosolewa kwa aliyokuwa anayafanya jibu n hakuna hata moja,sasa kwa nin huo umuhim wa kukosoa uwe kwa Mama Samia ila c kwa Magu?mlipewa vichwa ivo kifikir na c kubebea meno jmnn!khaaaaa!!
Wakachunge ng'ombe Mpanda bado kuna mapori mengi tu huko...
 
tatizo humu ndani wengi hukosoa kwa milengo yao, watu wakiacha ushabiki na mahaba watakosoa kwa tija bila kujali milengo yao.
 
Kuna watu wanataka kuuaminisha Umma kuwa Rais Samia Suluhu hakosei.

Hawa watu kwa kuendelea na upuuzi ule ule kwa waliokuwa wanazi na mashabiki wa Magufuli ambao nao walikuwa wanataka kuuaminisha Umma kuwa hakuwa akikosea.

Watanzania wengi wanajikita katika Ushabiki, Mahaba, Jazba, Mihemko na Ashki hata katika mambo ya msingi ya Kitaifa.

Kwa sasa limeibuka kundi la watu ambalo ukimkosoa tu Rais Samia unaonekana ulifaidika na utawala wa Magufuli. To hell.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
Ni muendelezo wa kutumia matumbo kufikiri toka miaka na miaka tunaposhindwa kukemea ubovu kwa kuamua ku side na waovu kwa kuangalia kabila,dini,chama,jinsia,dhehebu n.k

Mimi nitasimama kama Mtanzania hawa wote watapita Tanzania itabaki. Tutamkosoa Samia na akija Mwingine akakosea tutamkosoa kama ambavyo tulimkosoa Kikwete na Magufuli pia.

Na atakayefanya vizuri tutampongeza kwa mazuri yake.
Wacha blabla lini ulimkosoa magufuli waliomkosoa magufuli hawakubaki salama aidha wamepotea au wamefunguliwa makesi ya uhujumu uchumi
 
Back
Top Bottom