Tulimsingizia na kumhukumu Hayati Magufuli juu ya utekaji, Je leo tutamsingizia nani? Magufuli hayupo

Tulimsingizia na kumhukumu Hayati Magufuli juu ya utekaji, Je leo tutamsingizia nani? Magufuli hayupo

Msaidizi wa Mwenyekiti Mbowe,alivyopotea tukasema Magufuli kamteka eti msaidizi wa Mbowe alikuwa anapinga PhD ya Magufuli,Leo kapotea Msaidizi wa katibu Mkuu Mnyika,Je tutamsingizia nani wakati Magufuli hayupo!?

Soma Pia: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Ndugu Deogratias Balile mwandishi wa Habari aje atuambie maana yeye anajua zaidi kwenye malumbano ya hoja pale ITV aliuambia umma wa watanzania kwamba serikali ya JPM ilikuwa inateka watu,na sasa ktk awamu ya sita ya rais SAMIA kuna amani sana na watu hawana hofu tena.Deo aje atusaidie.
 
Maswali jadidi juu ya utekaji.

1.Je ni kweli kwamba matukio haya yanamfaidisha mkuu wa dola?

2.Je Inawezekana vipi mkuu huyo wa dola aruhusu matukio ya utekaji na mauaji yanayoharibu taswira yake kisiasa?

3.Tuanze awamu ya tano,je matukio haya yalianza baada ya nani kuondolewa madarakani?

4.Awamu ya sita,matukio haya yalianza baada ya nani kuondolewa madarakani? baada ya nani kukosa trust ya mkuu nchi?

4.Ninahofia uwepo wa genge la watu lenye nguvu kifedha na kisiasa,wanaotumia assets za Serikali kufanya utekaji na mauaji,mfano unaweza kugombana na ndugu yako ukamwambia wewe utaona wewe,adui yako akajua,akaenda kummaliza,Dunia itakunyooshea wewe kidole uliyegimbana na ndugu yako

#@RipMagufuliRipMzeeKibao.
 
Kwa hiyo mtekaji ni nani sasa? Manake polisi hawahusiki, TISS hawahusiki, JW security unit hawahusiki. Mkuu wa nchi ambaye ndiyo sauti ya mwisho nchi hii naye anasema hii kitu ni drama. Kama ni vyama vya upinzani mbona hawakamatwi? Shida Iko wapi?
Deep state
 
1. Kuna uwezekano ilifanyika kuonesha JPM ndo alikuwa mbaya ili kupata uungwaji mkono dhidi ya upinzani na mahasimu wa JPM kwenye chama kwa wakati huo
2. Sasa inawezekana reverse is true. Mahasimu wa Her Excellence ndani ya chama wameungana na wapinzani kuonesha kutokuwa na uwezo wa kuwa comfort in chief Kwa kushindwa kidhibiti uhalifu nchini hata kama unafanywa na genge la wahuni wakitokea walikotokea
3. Mama anahitaji kupata washauri wazuri asije akavurugwa halafu wahuni waseme ameshindwa kazi, hafai kuendelea 2025

Mnatatfuta visababu vya kuhalalisha mauaji yenu. Mnafiki mkubwa.
 
Magufuli alisingiziwa mengi.

Apumzike kwa amani shujaa Magufuli;mtoto wa Africa; mzalendo halisi .

Alisingiziwa na nani na lini? Punguza unafiki. Magufuli na Samiah lao moja. Uzuri Magufuli alilshalipwa kwa ubaya wake.
 
Ni swala la CCM kuanzia Nyerere...ila wanaomsema Mbowe wasibezwe maana sio malaika

Msipende kutafuta sababu za kijinga kukwepa ukweli. Taarifa za Mzee Ally kushushwa kwenye basi zilitoka mapema, polisi walichukua hatua gani?.
 
Msaidizi wa Mwenyekiti Mbowe,alivyopotea tukasema Magufuli kamteka eti msaidizi wa Mbowe alikuwa anapinga PhD ya Magufuli,Leo kapotea Msaidizi wa katibu Mkuu Mnyika,Je tutamsingizia nani wakati Magufuli hayupo!?

Soma Pia: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Magufuli hana namna anaweza kukwepa lawama juu ya mambo haya kwani haswa kama sio muasisi aliyaboresha na kuwafundsha wafuasi wake kwamba ndio njia sahihi ya kufanya siasa. Hawezi kujitenga hata kidogo. Hivyo yanayofanyika na muendelezo au maboresho ya kazi yake. "Aliwambia speaker Ndugai wafukuze bungeni kwakua wana kinga na wakija huku nitawashughulikia kwakua hawana kinga" Bashite aliweka bayana kuwa apewe kazi ya kuwashughulikia wakosoaji wake na akafanya hivyo kwa vitendo. TAL alipopigwa risasi aliagiza jeshi la polisi kuhakikishwa kwamba makanisani na misikitini hakuna watu wanaofanya ibada kumtakia siha njema, mathalani kule tanga watu walikamatwa walipokusanyika kwa ajili hiyo. Yeye na serikali yake na polisi waliwazuia wanachama wa CHADEMA siku ya kuchangia damu kujitolea damu kama comemoration ya damu ya TAL iliyomwagwa na wahuni ndani ya eneo la makazi ya wabunge tena Speaker lenye CCTV canera na walinzi. Magufuli na serikali yake kwa kushirikiana na JOB walikataa katu katu kumlipa stahiki za matibabu kama mbunge na walichofanya ni kusema hawajui yuko wapi na wakamvua ubunge rasmi. hakwepi hili hata kidogo.
 
Huwa bado nawaza sana balozi Simoni Sirro enzi akiwa IGP aliwahi kusema kuwa Polisi wana ushahidi kamili kuhusu mashitaka dhidi ya Freeman Mbowe katika kesi yake ya 'ugaidi' iliyokuwa inahusisha pia utekaji na mipango ya mauaji kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa na tuliona kina Kingai wakienfa mahakamani kutoa matokeo ya upelelezi wao, ambapo mahakama ilimkuta Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu; mara ghafla bin vuu tukaona DPP amesita kuendelea na kesi, Mbowe akatoka jela yeye na washtakiwa wenzake, siku hiyo hiyo akaenda Ikulu kuonana na Samia, mara ghafla tukaambiwa maridhiano, Kisha IGP Sirro anatolewa U-IGP na kuteuliwa kuwa balozi Zimbabwe;....
Polisi waachane na Siasa na Uchawa shida inaanzia hapo
 
Upumbavu mwingine! Unajua nguvu alizonazo rais? Unajua vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yake? Unajua kuwa ana uwezo wa kuomba hata Scotland Yard waje kusaidia? Yule mpumbavu Magufuli alikuwa muuaji na kipindi chake utekaji ndiyo ulizidi.
Moja ya kitu ambacho mimi sijakielewa ni uzito na ulazima wa kutekwa au kuuliwa kwa hao watu ambao tunadai wanauliwa/kutekwa na Rais. Utawala uliyopita Rais wa wakati huo amekuwa anashutumiwa hadi sasa kwa kuteka na kuuwa raia, ajabu na utawala huu nao tena rais anashutumiwa kuuwa raia yani, sasa ni yapi hayo hasa yenye kumlazimu rais hadi kuuwa hao watu?
 
Huenda ikawa makamu wa kipindi chake ndiyo alikuwa inaisuka mipango hiyo miovu.maana Hadi Sasa inaendelea na aliyesingiziwa alishafariki.
Lakini huyo Magufuli tulikuwa tunaambiwa alikuwa anafanya hayo kwa sababu alikuwa ni katili na wengine wakasema hakuwa na asili ya Tanzania ndio maana alikuwa na hiyo roho ya kinyama, ila zaidi tuliambiwa kuwa wakati wa Magufuli Samia akiwa makamu alitaka kujiudhuru kwamba hakuwa akikubaliana na anayofanya Boss wake ila kwamba akalazimishwa na wengine wanasema akaombwa.
 
Back
Top Bottom