Tulimzika rafiki yetu pembeni kabisa ya nyumba yake ili mkewe asiiuze

Tulimzika rafiki yetu pembeni kabisa ya nyumba yake ili mkewe asiiuze

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Pamoja na kuwa kuna wazee wa ovyo wengi ila bado kuna wazee wenye busara wengi pia.

Tuliwahi kupata msiba wa rafiki yetu ambaye alioa mke mrembo sana toka kaskazini,huyu mke alikuwa cha pombe na utulivu zero kabisa,hata kifo cha jamaa kilikuwa cha utata sana kuna watu walidai mke alihusika.

Kamati ya wazee ikaja na azimio kuwa marehemu azikwe pembeni kabisa bampa to bamba na nyumba yake ili huyu shemeji yetu asiweze kuiuza watoto wa marehemu wakakosa address

Nani atanunuua nyumba kaburi Limeegemea ukuta wa nyumba kaburi liko bamba to bamba na mlango wa uani na msalaba mkubwa
 
Hii issue ya kuweka makaburi mbele ya nyumba au pembeni ya nyumba naona sio nzuri.

Kaburi liwekwe nyuma ya nyumba, ndio maana hata haya makaburi ya jumuia mengi huwekwa mbali na makazi ya binadamu, mpaka mji ukikua ndio makazi ya watu kuanza kusogelea makaburi.

Kuweka kaburi mbele ya nyumba ili kuligeuza silaha ya kuwatisha wateja wa nyumba ni kulivunjia heshima, hata marehemu anastahili kustiriwa, awekwe nyuma ya nyumba hakuna yeyote anayeitaka nyumba atainunua hata kama kaburi likiwa nyuma ya nyumba.
 
Back
Top Bottom