Hii issue ya kuweka makaburi mbele ya nyumba au pembeni ya nyumba naona sio nzuri.
Kaburi liwekwe nyuma ya nyumba, ndio maana hata haya makaburi ya jumuia mengi huwekwa mbali na makazi ya binadamu, mpaka mji ukikua ndio makazi ya watu kuanza kusogelea makaburi.
Kuweka kaburi mbele ya nyumba ili kuligeuza silaha ya kuwatisha wateja wa nyumba ni kulivunjia heshima, hata marehemu anastahili kustiriwa, awekwe nyuma ya nyumba hakuna yeyote anayeitaka nyumba atainunua hata kama kaburi likiwa nyuma ya nyumba.