Tulimzika rafiki yetu pembeni kabisa ya nyumba yake ili mkewe asiiuze

Safii
 
Unamzika baba, ili mama asiuze nyumba watoto warithi, halafu watoto unawaambia watafute vyao?

Sasa kwa nini huyo baba asingeiuza kabisa yeye kabla hajafa na kuwaambia hao watoto watafute vyao?
Ulishaona ikulu inauzwa,hapo ni home makazi ya kudumu ta wanafamilia
 
Hizo ni tabia za kijima.

Unafananishaje nyumba ya mtu na Ikulu?

Una kitu kinaitwa "delusions of grandeur", hiyo ni aina moja ya ugonjwa wa akili.
Sio kila nyumba inauzwa,babu yako angeuza ile ya kijijini ingekuwaje
 
Ni yule mangi wa TBS alizikwa kwa Mapinga au
 
Hivi nikiinunua hiyo nyumba halafu nikahamisha hilo kaburi kwenda huko makaburini kuna tatizo kisheria?
 
Sio kila nyumba inauzwa,babu yako angeuza ile ya kijijini ingekuwaje
Kwani nani kasema kila nyumba inauzwa?

Hapa umefanya logical fallacies kadhaa.

1. Strawman argument fallacy. Umeleta hoja ya "sio kila nyumba inauzwa" wakati mimi sikusema kila nyumba inauzwa.

2. Appeal to emotion. Umeleta habari za babu yangu kuniingiza kwenye majibizano ya kihisia badala ya facts. Fact ni kwamba hunijui, babu yangu humjui. Hujui kama alikuwa na nyumba, hujui kama imeuzwa au la.

3. Umefanya hasty generalization fallacy. Unataka kulazimisha kila nyumba isiuzwe.

4. Umefanya argument from tradition fallacy. Hata kama ni kweli tuna utamaduni nyumba zote za familia haziuzwi, hilo halina maana hakutakuwa na sababu nzuri ya kuuza nyumba.

5. Non sequitur fallacy. Kwa sababu huko nyuma nyumba hazijauzwa, hilo halimaanishi ni lazima huko mbele nyumba zisiuzwe.

Kwa sasa niishie hapa tu.
 
Kuna mwamba Kijenge alinunua na akajenga nyumba juu ya hilo kaburi
 
Kama katokea kwl kaskazn mkuu kabur linahamishika kabsaa maana Arusha niliwai kushuhudia kabur la familia likiamishwa kwanza la babu bb sjui nan kama nne lakn cha ajabu muuska akutoboa mwaka nae kafark kwa pgo za ajabu
 
Kuna Moja ilitokea mapinga,Bagamoyo.Na wao watu wa kaskazini hukohuko,ndugu wa mume wanataka kuzika hapo hapo nyumbani mapinga,sababu zao Binti bado mdogo na watoto bado wadogo,hawajui mbeleni nini kitatokea.
Ndugu wa Mke wakakataa,hoja yao ni tangu lini Mchagga akazikwa Dar na wazazi wake wote wapo wazima hapo Kilimanjaro!
Pia Mke alisisitiza kuwa hata baadae wakihitaji Kujenga Nyumba za kupangisha itakuwa ngumu kupata wapangaji,nani anataka kupanga Nyumba Ina kaburi la mtu asiyemfahamu!
 
Dadeq; nyie mtakuwa mmesomea cuba si bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…