Tulimzika rafiki yetu pembeni kabisa ya nyumba yake ili mkewe asiiuze

Alikuwa mdogo tu,below 30yrs!
Kwa Ile Nyumba tu kuwa nayo kwa umri wake ni hatua kubwa.
Hiyo ya kwamba hajajenga kwao ilikuwa janja janja tu ya kuzuia hiyo Mali isipotee.
Alikuwa na zaidi ya miaka 30.
 
Nikianza leo itanichukua mda gani kua kama wewe bwana kiranga napenda sana unavyojibu kwa hoja
 
Kama ni mke wa ndoa, mahakama itampa kibali cha kuhamisha kaburi la mumewe na kwenda kumzika anakotaka kisha nyumba anauza. Hilo la kumzika pembeni ya nyumba halitosaidia.
 
La msingi kila jambo lifanyike kwa faida hata kama mwenye mali kesha kufa,haina haja kuuza mali za Marehemu kwa hasara kisa warithi mmeshindwa kuelewana kuziendeleza!!
 
Hili sakata nililiona kwa ITV na kwa Gea Habibi kwenye kipindi chake cha hekaheka pale clouds!! Ila sijajua nani alishinda!!
 
La msingi kila jambo lifanyike kwa faida hata kama mwenye mali kesha kufa,haina haja kuuza mali za Marehemu kwa hasara kisa warithi mmeshindwa kuelewana kuziendeleza!!
Inawezekana pia kuuza mali kwa faida hata kama warithi wameelewana.

Kwa nini watu wanakariri kwamba kuuza nyumba ni kitu kibaya tu?

Kuna jamaa alipiga bonge la deal, akajenga bonge la jumba Mbezi beach.

Baadaye akaja kugundua kwamba sehemu kubwa ya pesa ambazo angezitumia kufanya biashara ameziweka katika kujenga nyumba, ambayo haitumii kibiashara. Nyumba haikuwa inaingiza faida kibiashara.

Akaiuza ile nyumba aongeze hela kwenye mtaji wake ili aweze kuizungusha ile hela, yeye akahamia nyumba ndogo zaidi. Na biashara zikaenda vizuri tu kwa sababu kuuza nyumba kuli boost sana mtaji wake.

Tanzania kuna watu kibao wanalalamika majumba yao ni makubwa sana kuliko mahitaji yao. Watu wamejenga mahekalu huko Mbezi Beach na Mbweni, halafu hakuna mtu anayekaa. Nikiwauliza kwa nini hamyauzi mnunue pengine nyumba ndogo zaidi, watu wanaona kuuza nyumba ni kama kukata mkono vile.

Sasa, kwa nini mnakariri kwamba kuuza nyumba ni kitu kibaya kinachofanywa watu wakifarakana tu?
 
Unajua nini?kuuza nyumba ya mjini sio shida,shida kuuza nyumba ya kijijini ambayo ndio inakutanisha wanafamilia ni kukosa address,mfano nyumba ya babu yangu kijijini japo sio ya gharama haiiziki,pembeni kuna makaburi sita,baba ,shangazi na wajukuu wamezaliwa na kukulia pale.
Kabla hujashangaa watu wa mbezi na mbweni kutouza nyumba,shangaa wa kariakoo,ilala,na magomeni maana wanaishi kifukara sana na nyumba zao zina thanani sana kutokana na location kuliko hata huko mbezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…