Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Ukienda Holiday unakuta kobe
 
kitu kobe hata me kilihusika kutishwa nacho sasa mbaya zaidi siku nikitishwa ndo nakojoa
Hhhhaaa mlikojoa mkiwa na miaka mingapi?wengine tuliacha kukojoa tukiwa wadogo
 
hahahaha Dina bibi yako amenichekesha sana vituko vyake....aiseee hakuna bibi asiye na vituko ngoja leo nisome kwanza nami nitashare siku nyingine....
Asante nimecheka sana tena sana ila mabibi wote wana mapenzi sana na watoto hasa wajulkuu...
Uje utuelezee wako wapoje
 
Bibi yangu mimi sifa yake kubwa uchoyo, wakati tupo wadogo tulikuwa tunakaa naye kijijini yaani watoto wake wakieanda kumtembelea mkimpelekea chakula mjue hatopika mpaka waondoke akibaki mwenyewe ndio anapika eti wanavila sana mjini, so watoto wake wanamjua hivyo wanampekea vyakula vilivyokaushwa ili asile vilivyochacha, siku akipika chakula kizuri kama nyama hivi ujue sufuria anakaa nalo yeye anachomvyea humo nyie anawagawia na mkono [emoji23][emoji23][emoji23]..pia alikuwa hapendi tucheke cheke ovyo eti tutakuwa vichaa na sisi siku tukiamua kumuudhi tunacheka hata kama hakuna la kuchekesha. Dah yaani tukikumbushana tunacheka kinoma
 
Hhhhaaa mlikojoa mkiwa na miaka mingapi?wengine tuliacha kukojoa tukiwa wadogo
hahaha mkuu enzi hizo hujui hata umri wako wewe unaona kunakucha ,usiku mara umekojoa yaani ndo life lilikuwa ivo
 
Mim bibi mzaa mama ni mchoyo hata sinaga hamu nae kwakweli
 
Bibi yangu ana gubu na nongwa yaani ukiwa karibu yake muda wote anatoa kasoro tu ila ole wake mtu mwingine amuige kusema wajukuu zake kinawaka,Ukipigwa au kusemwa na mtu yeyote anamuwashia moto,Tulikua tunaogopa hata kumwambia mtu akitusema hata kama sisi ndio tuna makosa;kuna mwalimu alimsema binamu yangu akasikia,siku moja mwalimu akapita kwa bibi akamsalimia alijuta na akawa anatuogopa kutusema
 
Bila shaka upo kwa bibi(umeenda kumtembelea) ama utakuwa umemmisi

R.i.p marehemu bibi yangu na babu yangu pia[emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Bila shaka upo kwa bibi(umeenda kumtembelea) ama utakuwa umemmisi

R.i.p marehemu bibi yangu na babu yangu pia[emoji24] [emoji24] [emoji24]
Yaaa nipo kwa bibi
Nawe umereply uzi wote huo jamani
 
Siku zote ndio hivyo,,tusemane sisi kwa sisi tunaona kawaida
Hata bibi yangu asikie mtu anatusema vibaya weee kitawaka ye akitusema hakuna shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…