Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Bibi yangu yeye namkumbuka kwa mengi especially hadithi zake zamani huko mambo ya Mwaka wa njaa,, ati mama ake(mama ake bibi) alikuwa anabandika jiwe kwenye chungu na maji mpaka juu anawaambia wachochee wasifunue kabisa bhasiii wanachochea mpaka yao anakuja wanachochea Wee mpaka wanasinzia wanamuacha anachochea, kustuka Kumekucha!! Walikuja jua hii kitu wamekuwa wakubwa lol
Pili bibi yangu anapenda ela uyoo (asili yake inachangia nadhani) Yaani Kama wewe ni mjukuu wazazi wako njema jua utapendwa hatarii na watoto wake pia kuna anao wapenda kuliko wengine
Anapenda wajukuu wenye majina yake pia,, also alinichapa mpaka nikaacha kukojoa kitandani Jamani aliniambia ataniletea Kobe nimkalie mbona niliacha kukojoa mweeh
Nakumiss bibi see you kwenye holiday
Ukienda Holiday unakuta kobe
 
kitu kobe hata me kilihusika kutishwa nacho sasa mbaya zaidi siku nikitishwa ndo nakojoa
Hhhhaaa mlikojoa mkiwa na miaka mingapi?wengine tuliacha kukojoa tukiwa wadogo
 
hahahaha Dina bibi yako amenichekesha sana vituko vyake....aiseee hakuna bibi asiye na vituko ngoja leo nisome kwanza nami nitashare siku nyingine....
Asante nimecheka sana tena sana ila mabibi wote wana mapenzi sana na watoto hasa wajulkuu...
Uje utuelezee wako wapoje
 
Bibi yangu mimi sifa yake kubwa uchoyo, wakati tupo wadogo tulikuwa tunakaa naye kijijini yaani watoto wake wakieanda kumtembelea mkimpelekea chakula mjue hatopika mpaka waondoke akibaki mwenyewe ndio anapika eti wanavila sana mjini, so watoto wake wanamjua hivyo wanampekea vyakula vilivyokaushwa ili asile vilivyochacha, siku akipika chakula kizuri kama nyama hivi ujue sufuria anakaa nalo yeye anachomvyea humo nyie anawagawia na mkono [emoji23][emoji23][emoji23]..pia alikuwa hapendi tucheke cheke ovyo eti tutakuwa vichaa na sisi siku tukiamua kumuudhi tunacheka hata kama hakuna la kuchekesha. Dah yaani tukikumbushana tunacheka kinoma
 
Bibi yangu mimi sifa yake kubwa uchoyo, wakati tupo wadogo tulikuwa tunakaa naye kijijini yaani watoto wake wakieanda kumtembelea mkimpelekea chakula mjue hatopika mpaka waondoke akibaki mwenyewe nfio anapika eti wanavila sana mjini, so watoto wake wanamjua hivyo wanampekea vyakula vilivyokaushwa ili asile vilivyochacha, siku akipika chakula kizuri kama nyama hivi ujue sufuria anakaa nalo yeye anachimvyea humo nyie anawagawia na mkono [emoji23][emoji23][emoji23]..pia alikuwa hapendi tucheke cheke ovyo eti tutakuwa vichaa na sisi siku tukiamua kumuudhi tunacheka hata kama hakuna la kuchekesha. Dah yaani tukikumbushana tunacheka kinoma
Mim bibi mzaa mama ni mchoyo hata sinaga hamu nae kwakweli
 
Bibi yangu ana gubu na nongwa yaani ukiwa karibu yake muda wote anatoa kasoro tu ila ole wake mtu mwingine amuige kusema wajukuu zake kinawaka,Ukipigwa au kusemwa na mtu yeyote anamuwashia moto,Tulikua tunaogopa hata kumwambia mtu akitusema hata kama sisi ndio tuna makosa;kuna mwalimu alimsema binamu yangu akasikia,siku moja mwalimu akapita kwa bibi akamsalimia alijuta na akawa anatuogopa kutusema
 
Mim bibi yangu upande wa baba ana vituko huyo,anaongea kuanzia asubuhi mpaka tunaenda kulala
Bibi yangu hua anaamka saa 12 asubuhi ole wako uchelewe kuamka ataanza kusema sijui mtaolewa na kina nani mpo wavivu vivu tu
Akija mtu anauza mboga au chochote bibi atataka apunguziwe na kuanza kusema mbona hata sio kizuri chukua hela wewe unakataa pesa(cha kwake sasa bibi yangu weee umwambie apunguze bei mkali kama nini)
Alilazwa hospital hua ana kisukari hiyo hospital ilikua mpya so kukawa na wagonjwa baadhi ,jumla wakawa wanne akiwemo na bibi yangu,ikifika asubuhi anaanza kuwaamsha kua wafanye usafi wafue nguo zao,mara wakaoge yaan utafikiri ye nurse wa zamu
Akiwa hayupo kwake anaona kila kitu hakiendi anaona kama anaibiwa vitu so muda mwingi yupo nyumbani na anataka kila kitu kikae sehemu yake
Hata itokee safari hataki kuondoka kwake anaona wafanyakazi wataiba

Anapenda watoto wa kiume hakuna mfano wa kike kwake hawana maana kabisa

Akiwa hataki mtu aende kwake na akaenda ukimsalimia tu au kumuuliza chochote anakua mkali na kuanza kulalamika kua huyu kijana hana adabu anaweza niuliza maswali ya hivi mim mzee,,yule mtu akiondoka ,watakuja baba zangu wadogo anaanza kuwapa mashitaka sasa akiona hawamjali,akija mtoto wake mwingine anamuhadithia na kuongeza chumvi ili yule kijana apigwe basi wakiona vile wanajifanya kukasirika na kusema wanaenda kumtafuta yule kijana wamfundishe adabu,basi bibi akisikia hivyo roho kwatuu,

Bibi yangu anaweza sema hivi baadae kikiharibika kitu anawakana wote kua mmesingizia,,

Hapatani na mmewe kila mtu analala chumba chake,,wakianza kurushiana maneno na babu kila mtu ni mbaya,,ataanza kumwambia na ufe tu sijui unasubiri nin mzee mbaya wewe huna maana,,bibi anapenda watoto wake na wajukuu zake kuliko mmewe

Kuna kipindi nilienda kuwasalimia nikawa namtengea babu chakula ,,kabibi kanamuambia babu subiri dinazarde aondoke uone nani atakupa chakula utakula jeuri yako

Bibi yangu watoto wa kiume hata wafanye nin haoni ubaya,nyie wa kike sasa ataongea siku nzima

Akianza kusimulia kua ye alikua mzuri utasema sijui alikuwaje haha

Kila mda anataka mle ye hali ila nyie mle tu chakula ndio furaha yake

Akianza kuchamba siku hiyo tutacheka tu maana siku hizi kabakiza mdomo tu ,maana anakua kakaa kwenye kiti hawezi kutembea haraka kama zamani wala kupiga

Hali kwa watu akiamini sio wasafi kama yeye,akitembelea sehemu atakunywa soda tu chakula hagusi

Bibi yangu ana mdomo huyu ,babu yangu humuambia kwisha habari yako naenda kuoa msichana mdogo,,nae anamuambia nenda umechelewa tukutolee mabegi

Siku moja nilikuta wanagombania kahawa,bibi kamnyima babi kahawa,alitaka kuweka kwenye maziwa
Anamuambia kanunue pesa zako unapeleka wapi

Basi inabidi kesho babu akanunue ile kahawa kubwa

Babu yangu sasa,ana ng'ombe wengi anawapenda kuliko sisi wajukuu ,,ukimuomba hata mmoja anakuambia ng'ombe wangu wagonjwa wamevunjika miguu
Ameanza kusahau pesa hua tunamchenjia buku buku,,akitembea na laki anaweza nunua sweta la 10000 akauziwa 80000,siku hiyi ikabidi wamuambie wee aksema pesa zangu zinawahusu nin nyie,mbona nyie mkinunua kitu siwaulizi,nikinunua mim tu mnatoa macho,,
Bibi yangu sasa utafikiri 80000 zake aliongea na kusema yule kijana afungwe sijui nin,babu anamkatisha nyamaza we mwanamke mzee

Babu yangu siku moja ananipa pesa ile anatoa akadondosha kondom moja nilicheka mpaka nikaanguka chini

Akiona mkewe kalazwa hayupo siku nyingi nyumbani anasema mleteni mke wangu,akifika siku hiyo tu wanakosana hahaha

Hua nacheka mno mie ,bibi yangu anaweza badili maneno mpaka ukashangaa na kusema juu eti dina mim nilisema hivyo inabidi umfurahishe kua hakusema wakati alisema na sisi tulikuwepo

Babu yangu akiugua mkipeleka ile ile hospital siku nyingine anakataa,,kua hiyo hospital imemchosha nipelekeni Dar nipande ndege,,,inabidi wampeleke tu

Anaweza ondoka bila kuaga akapanda gari akaenda Arusha anaenda kumtafuta mtoto wa ndugu yake ni daktari na kumuambia naumwa sana,akipimwa hakuna kitu
Huku watamtafuta balaa,mpaka simu ipigwe ndio wanamfata

Babu anatupenda wajukuu wa kike kuliko wa kiume,,sie wakike ndii hutupa pesa wa kiume anaawaambia nendeni kwa bibi yenu huko

Hebu elezeeni visanga vua huko kwenu
Bila shaka upo kwa bibi(umeenda kumtembelea) ama utakuwa umemmisi

R.i.p marehemu bibi yangu na babu yangu pia[emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Bila shaka upo kwa bibi(umeenda kumtembelea) ama utakuwa umemmisi

R.i.p marehemu bibi yangu na babu yangu pia[emoji24] [emoji24] [emoji24]
Yaaa nipo kwa bibi
Nawe umereply uzi wote huo jamani
 
Bibi yangu ana gubu na nongwa yaani ukiwa karibu yake muda wote anatoa kasoro tu ila ole wake mtu mwingine amuige kusema wajukuu zake kinawaka,Ukipigwa au kusemwa na mtu yeyote anamuwashia moto,Tulikua tunaogopa hata kumwambia mtu akitusema hata kama sisi ndio tuna makosa;kuna mwalimu alimsema binamu yangu akasikia,siku moja mwalimu akapita kwa bibi akamsalimia alijuta na akawa anatuogopa kutusema
Siku zote ndio hivyo,,tusemane sisi kwa sisi tunaona kawaida
Hata bibi yangu asikie mtu anatusema vibaya weee kitawaka ye akitusema hakuna shida
 
Back
Top Bottom