Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Nina baby yng mmoja,, alikuwa anajifanya yeye ni mjanja wa zamani,, yeye kila kitu anajuwa,, mnaweza kukaa sehem akapita msichana,, utamsikia Enzi zangu sokoni hafiki yule,, nishambadilisha muelekeo,, yaani kila kitu Enzi zake yeye ni noma,,, aliletewa Simu na mwanae mmoja,, yeye alikuwa ni mgeni na Simu lakini anajifanya mjuaji,, simu inafungwa na KITAMBAA isichubuke,, basi tukawa tukimwona katulia tuna BEEP NAMBA YAKE,, kabla ya kupokea tunakata,,, basi atatukana sana,, SIJUWI NANI HUYU ANATAKA KUNIMALIZIA PESA ZNG kwenye Simu,,, kuni beep beep tu,, basi ikawa mchezo,, yeye aliamini simu IKIITA TU akipokea PESA ZINALIWA,, akitulia tu tunabeep,,, aisee,, ilikuwa BALAA,, yaani akigunduwa Kama ni wewe unayemsimbuwa ni KESI KUBWA,,, basi tunacheka sn tu
 
asee heshima zenu nitaendelea kuwapa maana sio wewe tu, khantwe RRONDO, Asprin kasi ya kuitwa mtoto humu imezidi..

Inabidi nijitathimini.
Hehehe we ni katoto
 
Mimi babu na bibi yangu wapo(ahsante MUNGU japo changamoto za uzee lukuki) bb yangu hana shida ila babu yangu jamaniiii..

Kwanza akiamka asbh anapika hodi kutoka chumbani kwake,na awahi kuamka,itapigwa hodi mpaka anatoka nje anaenda kukaa anasubiri Chai...

Akishakunywa chai,anaenda kuoga,sasaa nguo zinaanza kuchojolewa "mesini" ukimwambia babu jamani mbona unafanya hivi mbona unatàka kutupa laana za wazi anakujibu "mm sioni jamaniiii sifanyi makusudi" (ana shida ya macho hayaoni vzr)basi imekuwa kama nongwaa kila kitu ukimuambia au kumuelekeza anajibu mm sioni yaani ndio kama silaha yake....

Akitoka kuoga hapo katumia masaa ma3,.baada ya hapo ni kuitwa mpaka uvurugwe,.usipite karibu yake utamsikia " ww nani unapitapita hapaaa ww jambazi nini??"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Na wanapenda kula chips,nyamanyama eeh vitu vya kunona ukiwapa maharage hata kama hawajala wiki nzima watasononeka hao hatarrrriiii.....yaaani MTU kuna muda inabidi ucheke tuu maana unapata hasira mpaka inalainika kwa vituko vyao,...bibi akianza kumgombeza babu hahhahhhaah basi buanaa.....
 
Mimi babu langu alikuwa na nyumba zake mtoni mtongani sasa likizo huwa namtmbeleaga
Kuna siku nilipomtembelea nilikuta anaugomvi na mpangaji wake nilipofika tu akanambia nakupa mtihani ukiweza utakaa hapa likizo yote ukishindwa kweeenuuu, nikamwambia poa aknipa peni na karatasi akanambia anataka nataka umuandikie barua joseph ahame hivyo andika kama ninavyoongea usipunguze hata herufi moja akaanza na fyonyoo akambia andika ,akaja nyoooo' akaendelea JOSE JOSE SIKUTAKI KWANGU KAMA UMESIKIA HIKI KITUO CHA KULEA MASIKINI SIO KWANGU ,MTOTO HUNA HAYA KUTWA KUMUANGALIA MKE WANGU fyonyo la pili,,,,akaendelea HUKUNISAIDIA MCHANGA WALA KOKOTO (tusi) hukuleta mchanga wala nondo (tusi) kazi kuning'iniza...(tusi) akanigeukia na mimi ole wako lipungue neno nami nikala tusi laini akaongeaaaaa jioni nikawakuta baa wanakunywa pamoja eti mimi ndo mbaya nimetunga maneno nalazimisha urithi nilikuwa 4m4...dah yule mzee wa bandari alikuwa burudani saaana na alikuwa anapenda mnoooooo mis him much
 
Bibi yangu mzaa mama (RIP)alikuwa anapenda wageni jamani yaani hata mtu anapita njiani hapo kwake ni njia akimsalimia tu ataanza story nae hadi mtu anasimama masaa anamsimulia habari hata hazimuhusu. Alikuwa napenda kuteta watu "gossiping"
Dingi alinifukuza home nilipata ujauzito usio na maelezo mother akanipeleka kwa bibi. Yaani nilitetwa mimi halafu nasikia kabisa watu wakimuuliza tu Bibi mbona huonekani wee anaanza "nitaonekana vipi nimeletewa mzigo mzito kweli umo ndani, mzigo hauna mahari wala posa."

Ila alikuwa sio mchoyo wa chakula na hodari wa kulisha ila hazingatii ratiba breakfast babu anapewa saa sita lunch jioni kwa sababu ya kupenda kuongea na kila mtu kazi zake zinasimama. Ana ng'ombe wake anakamua maziwa anauza. Siku mteja akikosa maziwa tu akute maziwa yameisha ataanza kuniteta

"Kuna mzigo upo ndani unakunywa maziwa kama maji ya kunywa kwa kweli nashindwa kuelewa karibu nitakosa hata pesa ya madawa sasa maziwa ya biashara yote anamaliza "

Basi nikisikia naishia kulia tu.

Kituko sasa nimejifungua mwanangu bibi yangu anamwambia mama yangu ee uje upesi mtoto analia mdomo wake una sauti kali sijui kabila gani huyu mtoto halafu halali usiku kwani huyu mwanao kazaa na nani asije kuwa kazaa na majambazi maana ndio hayana adabu yanakesha usiku kuiba" anaongea hivyo kwa kutumia simu yangu hatanii anamaanisha. Halafu tupo wote hapo hapo.

Akimaliza hapo anakuletea uji wa maana na supu yaani nilikuwa nalia lakini misosi unafurahi na roho yako

Bibi yetu alikuwa hapendi kabisa ukae na Babu (RIP) kuongea chochote akikukuta tu lazima atawavuruga anasema mwacheni aongee na TV yake huyo si anaongea na wanawake zake wazungu. Kisa babu alizaa na mzungu watoto wawili miaka hiyo huko Uingereza wakati keshamuoa bibi alienda kusoma.

Babu alitangulia kufa baada ya siku tano bibi akafa wote walikufa wamelala. Walale salama huko waliko. [emoji1431]
Jamani sanduku la bibi lilikutwa na pesa nyingi sana. Alikuwa ana pesa haishiwi. Pesa yake ya maziwa inakaa kwenye sanduku pesa ya matumizi watoto zake walikuwa wanampelekea kila mwezi. Na ile pesa babu hagusi. Ya kwenye sanduku hakuna aliyekuwa anajua kuwa kuna mipesa ndani Bibi yangu namkumbuka sana kwa kuteta na masimango mchaga yule mwisho.
 

Akii hii story imenivunja mbavu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Nimempenda bibi yako wallah....[emoji39] [emoji39]
 
Hahahgashghahahah mzigo!
 
Aisee kababu yangu nikilala nako ni stori tu nikisinzia kananiamsha daaah, vistori vingi hua ni fix basi anafurahiii
 
Akii hii story imenivunja mbavu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yaani wazee wangu basi tuu,halafu babu yangu anapenda kuuliza SAA(muda)hata uwe umeenda Pluto hamjaonana miaka 20,ukiingiza tuu mguu ndani cha kwanza kukuuliza ni "hivi sasa ni SAA ngapi hapo"[emoji23] yani hana kummisi MTU wala nn hajui umerudi ukechooooka au vipi yy ni SAA tuu usipomjibu utamsikia " najua nawakera ila hamnipendi tuu"[emoji23] [emoji23] ..na ukimjibu labda SAA 6:30 mchana baada ya dk 2 anauliza tena....eeeh unatamani umkate vibao akalazwe muhimbili[emoji1] [emoji1]
 
asee heshima zenu nitaendelea kuwapa maana sio wewe tu, khantwe RRONDO, Asprin kasi ya kuitwa mtoto humu imezidi..

Inabidi nijitathimini.
Ujitathimini nini sasa kwani ni kosa lako kuchelewa kuzaliwa?
 
bas bibi angu akija mjini kaz yake kuokota vitu vilivyotupwa ka makopo ya lotion viboks na nin anaweka chumba anacholala,na mkitupa ni ugomvi mkubwa na anarudi tena kuokota,cku ya kuondoka anachukua roba chafu anaviweka na ole wako ubadilishe roba sasa,siku moja tukachukua roba usiku tukalitupa asubuh sasa anapelekwa stand akauliza mzgo wake na akasema siondok ad nipewe mzigo wangu ikabidi tukamtafutie roba lenye vitu vyake
 
daby hii inakama ka ukweli flani mfwate mshana akufafanulie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…