Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Mim bibi yangu upande wa baba ana vituko huyo,anaongea kuanzia asubuhi mpaka tunaenda kulala
Bibi yangu hua anaamka saa 12 asubuhi ole wako uchelewe kuamka ataanza kusema sijui mtaolewa na kina nani mpo wavivu vivu tu
Akija mtu anauza mboga au chochote bibi atataka apunguziwe na kuanza kusema mbona hata sio kizuri chukua hela wewe unakataa pesa(cha kwake sasa bibi yangu weee umwambie apunguze bei mkali kama nini)
Alilazwa hospital hua ana kisukari hiyo hospital ilikua mpya so kukawa na wagonjwa baadhi ,jumla wakawa wanne akiwemo na bibi yangu,ikifika asubuhi anaanza kuwaamsha kua wafanye usafi wafue nguo zao,mara wakaoge yaan utafikiri ye nurse wa zamu
Akiwa hayupo kwake anaona kila kitu hakiendi anaona kama anaibiwa vitu so muda mwingi yupo nyumbani na anataka kila kitu kikae sehemu yake
Hata itokee safari hataki kuondoka kwake anaona wafanyakazi wataiba

Anapenda watoto wa kiume hakuna mfano wa kike kwake hawana maana kabisa

Akiwa hataki mtu aende kwake na akaenda ukimsalimia tu au kumuuliza chochote anakua mkali na kuanza kulalamika kua huyu kijana hana adabu anaweza niuliza maswali ya hivi mim mzee,,yule mtu akiondoka ,watakuja baba zangu wadogo anaanza kuwapa mashitaka sasa akiona hawamjali,akija mtoto wake mwingine anamuhadithia na kuongeza chumvi ili yule kijana apigwe basi wakiona vile wanajifanya kukasirika na kusema wanaenda kumtafuta yule kijana wamfundishe adabu,basi bibi akisikia hivyo roho kwatuu,

Bibi yangu anaweza sema hivi baadae kikiharibika kitu anawakana wote kua mmesingizia,,

Hapatani na mmewe kila mtu analala chumba chake,,wakianza kurushiana maneno na babu kila mtu ni mbaya,,ataanza kumwambia na ufe tu sijui unasubiri nin mzee mbaya wewe huna maana,,bibi anapenda watoto wake na wajukuu zake kuliko mmewe

Kuna kipindi nilienda kuwasalimia nikawa namtengea babu chakula ,,kabibi kanamuambia babu subiri dinazarde aondoke uone nani atakupa chakula utakula jeuri yako

Bibi yangu watoto wa kiume hata wafanye nin haoni ubaya,nyie wa kike sasa ataongea siku nzima

Akianza kusimulia kua ye alikua mzuri utasema sijui alikuwaje haha

Kila mda anataka mle ye hali ila nyie mle tu chakula ndio furaha yake

Akianza kuchamba siku hiyo tutacheka tu maana siku hizi kabakiza mdomo tu ,maana anakua kakaa kwenye kiti hawezi kutembea haraka kama zamani wala kupiga

Hali kwa watu akiamini sio wasafi kama yeye,akitembelea sehemu atakunywa soda tu chakula hagusi

Bibi yangu ana mdomo huyu ,babu yangu humuambia kwisha habari yako naenda kuoa msichana mdogo,,nae anamuambia nenda umechelewa tukutolee mabegi

Siku moja nilikuta wanagombania kahawa,bibi kamnyima babi kahawa,alitaka kuweka kwenye maziwa
Anamuambia kanunue pesa zako unapeleka wapi

Basi inabidi kesho babu akanunue ile kahawa kubwa

Babu yangu sasa,ana ng'ombe wengi anawapenda kuliko sisi wajukuu ,,ukimuomba hata mmoja anakuambia ng'ombe wangu wagonjwa wamevunjika miguu
Ameanza kusahau pesa hua tunamchenjia buku buku,,akitembea na laki anaweza nunua sweta la 10000 akauziwa 80000,siku hiyi ikabidi wamuambie wee aksema pesa zangu zinawahusu nin nyie,mbona nyie mkinunua kitu siwaulizi,nikinunua mim tu mnatoa macho,,
Bibi yangu sasa utafikiri 80000 zake aliongea na kusema yule kijana afungwe sijui nin,babu anamkatisha nyamaza we mwanamke mzee

Babu yangu siku moja ananipa pesa ile anatoa akadondosha kondom moja nilicheka mpaka nikaanguka chini

Akiona mkewe kalazwa hayupo siku nyingi nyumbani anasema mleteni mke wangu,akifika siku hiyo tu wanakosana hahaha

Hua nacheka mno mie ,bibi yangu anaweza badili maneno mpaka ukashangaa na kusema juu eti dina mim nilisema hivyo inabidi umfurahishe kua hakusema wakati alisema na sisi tulikuwepo

Babu yangu akiugua mkipeleka ile ile hospital siku nyingine anakataa,,kua hiyo hospital imemchosha nipelekeni Dar nipande ndege,,,inabidi wampeleke tu

Anaweza ondoka bila kuaga akapanda gari akaenda Arusha anaenda kumtafuta mtoto wa ndugu yake ni daktari na kumuambia naumwa sana,akipimwa hakuna kitu
Huku watamtafuta balaa,mpaka simu ipigwe ndio wanamfata

Babu anatupenda wajukuu wa kike kuliko wa kiume,,sie wakike ndii hutupa pesa wa kiume anaawaambia nendeni kwa bibi yenu huko

Hebu elezeeni visanga vua huko kwenu
babu akiandaliwa chakula ale na wajukuu anadai wanampunja [emoji15] akitengewa ale peke yake anasema mnamnyanyapaa na kumuona mchafu[emoji15] [emoji4]
 
Babu yangu ana vituko nadhani hakuna,, haha

Alisema anakuja dar,, mjomba wangu akaenda kumfuata ubungo akamleta kwetu( yani kwa mamangu) ili akae siku tatu then atamfuata aende na kwake( mjomba angu ana mke ila hana watoto so kule hamna wajukuu),, basi akaja nyumbani siku ya tatu mjomba akaja kumfuata kuwa twende na kwangu baba,,,akamjibu,WAKATI NATOKA KIJIJINI NILIKUA NA LIST YA MAJINA KWENYE KARATASI YA WALE NITAKAO WATEMBELEA ,NA KILA NINAYEMUONA NAMTIKI,,SASA WEWE NISHAKUTIKI NILIVOKUONA TU UBUNGO SO SIJI.
Afu mkavuu na kamaliza .

Siku moja tukamwambie twende mjini tukuoneshe maeneo ,,akasema mi sijaja kuona maeneo nimekuja kuona watu,,yani anakatisha tamaa vibaya,, ila ukikaa naye ni kucheka muda wote



haaaaaaaaaaaaaaa!jamani!
 
babu akiandaliwa chakula ale na wajukuu anadai wanampunja [emoji15] akitengewa ale peke yake anasema mnamnyanyapaa na kumuona mchafu[emoji15] [emoji4]
Yaan bibi yangu mzaa mama yupo hivyo kabisa
 
Bibi mzaa Baba alikuwa mpole na kunipenda kuliko wajukuu wote R.i.p Bibi alinihadithia mambo mengi ambayo katika maisha ya sasa ndio nayashuhudia. Alikuwa na upendo kuliko kawaida. Babu mzaa baba alikuwa alikuwa mkokorofi balaa. Akiwa km 10 Akipiga kelele wote mnaanza kukimbia mashambani kwenye mahindi na usiku. Alikuwa anawapiga hadi akina baba mdogo na ukijikuna wakati akikupiga ni kosa maana ake utakuwa umepigana nae. R.I.P Babu.

Bibi mzaa mama alikuwa mlevi balaa. Ni kulala porini wacha akuone anaangua kilio kumbe lilikuwa lichawi bhana. R.i.p bibi yangu mchawi. Babu mzaa mama alikuwa mpole mpaka bibi ndio ana Sauti kinyume kabisa na Mila zetu. R.i.p Babu. Ukweli mtoto kukuta babu na bibi ni raha sana
 
Back
Top Bottom