Rip dearest bibi yangu. Alikuwa na vituko sana alinipenda kuliko wajikuu wote wa ukoo mzima, walikuwa na uchoyo Fulani ila kwangu hakuna kitu ambacho sikula kwake.
Historia inaonesha hakuwai kulala na babu (rip) yaan wakati wa kupata mimba wazee walikuwa wanakuja wanamkamata, babu anafanya yake, mimba tiyari ndo mwisho, hadi mtoto mwingine.
Wakati nakua nilikuta kila MTU analala kivyake. Babu ndo alitangulia mbele za haki.
Vituko vyake sasa uzee kweli fainali,walikuwa ana uwezo wa kukimbizana na wajukuu baadae ya kuiba maembe anakukimbiza umbali wa km hata 300
Alinipenda balaa, alikuwa akipika kabla hajala atatoa ndizi moja tu, aweke kwenye sahani aje kwetu, atauliza luckyline yupo WAP mama alisema hayupo atanisubiri hapo chakula amekifunika kitambaa nikija ananipa nakupa peke yangu ndo ataondoka.
Alikuwa awezagi kula chakula kilicjopikwa na MTU yeyote labda mm. Alikuja kula chakula kilichopikwa na MTU mwingine baadae ya kuzeeka sana.
Alinipenda kupitiliza mpaka kijiji kizima kilijua.
Alipoona nguvu zinapungua akamjulisha kila MTU kuwa siku akifa mm sio wasimzike, wanisubiri nifike,
Kweli mwaka 2015 bibi aliumwa uzeee, kila siku alimwambia mama niende nyumbani bibi nguvu kwisha, Bahati mbaya ndo nilikuwa nimepata kazi sehemu nyingine hata mwezi, nilikosa ruhusa.
Siku moja nilikosa usingizi usiku asubuhi nikamwambia mkurugenzi naomba niende kumuona bibi kabla hajafa ilikuwa j4 mkurugenzi akasema jitahidi uende jmosi kabla ya jos j5 bibi kafariki, nililia sana
Mama alinambia, mpaka anakufa alikuwa anauliza Niko wapi, sijui alitaka kunambia nini?
Basi upendo wa bibi kwangu ulisababisha wajukuu wengine wasinipende, baada ya bibi kufa wakataka wazike kisa mm Niko mbali, kijijin hakuna mochwari, wajukuu wanakomalia wazike, wazee nao wakakomaa, wanisubiri bibi alisema.
Tangu naanza safari nililia kwenye basi nilishindwa kujizuia, nakumbuka upendo wa bibi, yaani zamani bibi akijua nakuja likizo alikaa barabarani na kusubiri Gari nikishuka alitamani anibebe, jamani bibi alinipenda.
Anyway nilipofika msibani nilikuta wapumbavu wajukuu kaka zangu Dada zangu midomo wameivuta hawaniongereshi, sikukuta maandalizi yoyote, namaanisha zile mbwembwe za wajukuu, maua/shada na nilijua hawatafanya, nilivyofika Mjini nikatengeneza yakutosha na nikatafuta waandaaji wa sehemu ya ibada.
Nilipofika nilipokelewa wazee waliopigania wasizike waliponiona walifurahi sana huku wengine wamenuna kuwa wananisubiri mm nani,simnajua mambo ya kijijini, nilipofika nilipata nguvu process zote zikaanza upya. Na bibi yangu akazikwa kama nilivyotaka mm.
Kweli mpaka sasa siamini kama bibi yangu siko nae tena ,nilimkuta kashakuwa wa baridi ndani ya jeneza macho hanioni tena nililia sana nikamuomba msamaha kwa kutofika mapema nilitamani nimbebe mgongoni ila haikuwezekana. Ila naamini alinisikia kuwa nimefika maana niliambiwa kuwa kabla sijafika mambo yalikuwa hayaendi walikuwa wakilazimisha wazike kabla sijafika hata jeneza liliwashinda. Nilipofika tu kila kitu kilikuwa chepesi
Apumzike kwa amani, alifariki akiwa 96-age.nampenda hata Leo.