DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,256
- 4,647
Natumai siku imeenda vizuri!
Moja kwa moja kwenye mada, katika jamii yetu ya Kiafrika kuwa na wake zaidi ya mmoja (ndoa ya mtaala) ni jambo la kawaida toka enzi. Changamoto iliyojitokeza ni ujio wa dini ambayo kwa kiasi kikubwa ilitumika kutuweka chini na tamaduni zetu hivyo wengi wetu walipojiunga na dini ya mkoloni husuani ukristu, waliona ni dhambi.
Kwa wengine sisi ambao baadae tulitambua upuuzi uliokuwepo nyuma ya pazia, badala ya kujificha eti una mke mmoja anayetambulika huku nje ya ndoa kuna vimada lukuki, tumeamua kujitokeza hadharani kuitetea huu utamaduni.
Mimi binafsi nina wake wawili, wanafahamina na hapa nipo mbioni kuongeza watatu na wanne ifikapo mwakani.
Ninapokutana na mwanamke, mimi nakuwa muwazi kabisa toka mwanzo hivyo anajua anaingia kwenye uhusiano wa aina gani.
Kuna changamoto nyingi tu kama mahusiano mengine ila mafanikio ya ndoa ya aina hii, mwanaume lazima uwe unajitambua, uwe na msimamo, usiwe mbaguzi, kulinda heshima ya wake zako, usiongee madhaifu ya mke A na mke B.
Hebu wengine tuoeane maujuzi.
Uzi tayari.