Hujui usemalo.
Wanafunzi wazembe, wajuaji, wanaoshinda kwenye mitandao whatsup, instagram wakiangalia video za ngono usitegemee wataweza kufaulu...
Aisee, hili ninaloliongea nina uhakika nalo 100%. Hapa nilipo kuna wanafunzi wa sekondari wapo form 4 kwa sasa. Sasa hawa wanafunzi kuna siku nilikuwa nipo free, nikajisemea ngoja niwaite niwaulize mawili matatu juu ya shule na masomo. nikawaambia siku nitakayokuwa free, kweli, siku ilipofika wakaja (wapo watatu) tukaanza stori za hapa na pale.
katika stori nikajikuta nimewauliza somo gani ni gumu kwao, Watoto wakanijibu kuwa hisabati ni gumu kwao. Mimi nikawauliza gumu kivipi.? wakaniambia wakifundishwa huwa hawaelewi. nikawaambia ok, leteni mitihani mnayofanya niione, maana nilidhani labda wanatungiwa maswali ya additional mathematics siku hizi. Wakaendea kufuata mitihani, Kuja kuiona nikakuta maswali ni yaleyale ya enzi zetu.
kwamba maswali ya kutumia four figure, logarithm, exponents, repeating decimals, sets nk yaani kama vile ilivyokuwa enzi zetu na ilivyokuwa miaka yote. Nikawauliza sasa hapa kigumu ni kipi.? wakasema hayo hatuyawezi, na kweli ilikuwa hawayawezi kwani walikuwa wamepata single digits katika ile mitihani. Basi bila hiyana nikawaambia kwa sasa hamjachelewa, mkitaka kufaulu hesabu mtafaulu ingawa inahitaji jitihada za dhati. Nikawaambia mimi nitawasaidia, wao wawe wanaandaa maswali yote yanayowashinda nami nitakuwa nawaelekeza weekend nikiwa na nafasi.
Nilipokuja kuwafundisha, Inaonekana weupe kabisa kichwani, hata basics hawazifahamu. Mtu form four haelewi standard notation, significant figure, exponents rules, logarithms, sets, nk. walipowaletea maswali nikaona njia sahii ni kuwa nawasolvia maswali ya katika mitihani. Nikatoa pesa nikawaprintia past papers za necta zote toka 1996 mpaka sasa. Nilichowaambia sasa hivi nawafundisha muelewe, na nawafundisha muwe na uwezo wa kujibu maswali ya section A maswali rahisi, Kwani muda haupo on their side kiviiile. na wakishamaster maswali korofi na wakiwa wana uwezo wa kujibu maswali matano ya section A, means watakuwa na uwezo wa kupata marks 30, Kisha nitawatafutia maswli mawili ya section B ambayo wapate 20 ambayo itawarusha paka katika daraja C. Kupata maswali matano section A si kitu kigumu, kwani ukicover standard notations, exponents, sets, statistics, vector, coordinate nk hukosi maswali ya section A matano ya kujibu. Section B ukisoma Matrix, Linear programming, coordinate geometry, kinematics un=kamaster huwezi kosa maswali mawili ya kujibu.
Ninachofanya, nachukua subtopic swali lake, nawaelekeza na pia nawapa in and out posible ways maswali yanavyoweza kuja ya hiyo subtopic husika. Nikimaliza wafundisha nawapa task, wakachukue ile mitihani ya necta na mitihani mengine waliyokuwa nayo watafute maswali yanayofanana na hayo kisha wajaribu kuyafanya, tukikutana weekend nitawasahihishia kama wamekosea. Sasa hivi naweza sema wanaelewa, na nimeanza nao na maswali mepesi ambayo ni must occur in necta exams. na nikwambie tuu, toka nianze nao i am proud kuwa wanaweza solve questions zote za subtopics ambazo nimewaelekeza. itu ambacho ni maendeleo makubwa sana kwao na inanipa matumaini kuwa hawatofeli hesabu katika miezi minne ijayo wanayotaraji fanya Necta.
Nilichogundua mpaka watoto wanakuwa hivi, ni kwamba hawaelekezwi vyema na waalimu hawaweki mkazo juu ya elimu ya watoto. Sawa watoto ni wasumbufu, lakini inapaswa uingie katika saikolojia yao uendane nao kama umri wao. Kwa hawa nilionao, kwa sasa wanafurahia hesabu kwa kuwa wanaelewa, na ninavyoona hawawezi pata F wala D katika matokeo yao katika hili somo.