mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Huu uzi kuna watu watapita kama hawaoni maana wengi mwaka huo walikuwa viunoni mwa wazazi wao, wengine mlikuwa Sitimbi huko hamjui hata video ni mdudu gani.
Mwaka 1986 kulikuwa na fainali za Kombe la Dunia nchini Mexico, Germany Magharibi anapigwa 3-2 na Argentina, Argentina anachukua ubingwa. Bonge moja la mechi haijawahi tokea ila imefunikwa na mechi ya jana achana na Messi kuna mtu akiitwa Zicco unamkumbuka.
Kuna timu ya Uruguay walikuwa wanasifika kwa kucheza rafu mbaya hadi huku mtaani timu ikicheza rafu ikawa inaitwa Uruguay.
Kipindi hicho Dar nzima tunaenda Magomeni Mikumi kwa sheikh Yahya ndio alikuwa na hiyo video big screen mithili ya ukubwa wa kioo cha fuso.
Hii screen iliwekwa nje ya nyumba yake sehemu ya wazi watu tulijazana kama tuko Uwanja wa Taifa
pembeni amepaki range rover milango sita.
Huyu ndiyo alikuwa Don Dar nzima, Bakhresa kipindi hicho hajaanza hata kuuza mikate anauza icecream tu.
Mwaka huo Tabata nzima bar ziko mbili tu,Camp bar na Hai bar