Tuliofunga gesi kwenye magari njooni tupongezane, bajeti ya mafuta kutoka 900,000/= hadi 200,000/= kwa mwezi

Tuliofunga gesi kwenye magari njooni tupongezane, bajeti ya mafuta kutoka 900,000/= hadi 200,000/= kwa mwezi

Toa hoja kwanini uhisi hivyo, otherwise ni kutishana bila sababu, ni kama mimi nije halafu nikwambie nahisi hiyo simu yako ni bomu na litalipuka, yaani from nowhere and without basis
Mimi ndiye ninahisi tena? Aidha haujasoma hizo post zangu vizuri au post za mdau hapo juu zimekuondoa kwenye mood. Ila hata hivyo nasema ahsante.
 
BINAFSI NILIWASIKIA HAO DIT WAKIHOJIWA CLOUDS FM NA WALISEMA KWASASA WANABADILISHA MAGARI YANAYOTUMIA TU PETROL YA UKUBWA WA AINA YOYOTE KWA GHARAMA YA TSH, MILIONI MOJA NA LAKI NANE (1,800,000) WAKASEMA VIFAA VYA KUFUNGA MAGARI YANAYOTUMIA DIESEL WAMESHALETA ILA BADO HAWAJAANZA KUFUNGA ILA SOON WATAANZA PIA YA DIESEL.
PIA WALISEMA KWENYE DASH BORD KUTAKUA NA ALAMA INAYOONESHA KIWANGO CHA GESI KILUCHOPO KAMA TU INAVYOONYESHA MAFUTA, PIA KUTAKUWA NA BUTON MAALUM YENYE UWEZO WA KUSWICH OFF UPANDE WA GESI KAMA IMEKWISHA NA KURUDI UPANDE WA MATUMIZI YA PETROL.
NA WALISEMA KWASASA KILO MOJA YA GESI NI TSH, 1500 NA KWA GARI DOGO INA UWEZO WA KUTEMBEA MPAKA KM 27 KWA KG, 1 NAFIKIRI KIDOGO NIMEELEWEKA.
Kwa gari za diesel naskia gari za TBL wamefunga hiyo system ya gesi kama nishati mbadala samabamba na diesel.
 
Mimi ndiye ninahisi tena? Aidha haujasoma hizo post zangu vizuri au post za mdau hapo juu zimekuondoa kwenye mood. Ila hata hivyo nasema ahsante.
Usitafute huruma, toa hoja, hiyo hatari ya gesi ni ipi ambayo kwenye haya mafuta haipo?
 
Ni kweli kwamba zifuatazo ni baadhi ya changamoto au madhara ya kuweka na kutumia mfumo wa gesi asilia kwenye gari?

1. Ufanisi wa gari unashuka kwa 10% au zaidi.
2. Life span ya engine ya gari inapungua.
3. Nafasi ya kuhifadhi mzigo kwenye buti ya gari inapungua kutokana na kuweka hiyo mitungi.
4. Ikiwa idle gari huwa inasumbua kwenye ku-start.
5. Kuna uwezekano wa kutokea ajali ya moto iwapo connection ya mfumo wa gesi haikufanyika vizuri.
Hivi ndivyo vitu, watu wenye akili inabidi waulize sio kila bidhaa inayokuja wewe unafakamia tu
 
Sasa na wewe ndugu yangu acha uvivu,umeshapewa idea,yanayobaki na wewe fuatilia,we unataka kilakitu ufanyiwe???!!!!?
Unajua si kila kitu utakua unaujuzi nao na utaweza kutafuta ufafanuzi hapa na pale. Umewahi kusikia Mwalimu akikuambia Hakuna suli la kijing? Ina maana uliza chochote unaloweza kuuliza.
Mimi niko nje ya nchi na tumeshatumia gari VW passat iliku ikitumia gesi, mundo wake uko tofauti na hii ilioandikwa hapa, hilo gari ilikua huna haja ya kubonyeza buttom pale gesi inapokuishia, inajibdilisha automatic kwenda kwenye petroli. Mimi sijasomea ufundi na wala sijui kuhusu ufundi, fani yangu ni ya biology. Kwahiyo lazima niulize hapo TZ kukoje juu ya hili suala ndio maana nikaweka masuali mengi ambayo itawasaidia wengi
 
Maisha yatazidi kuwa marahisi,
Tutegemee gharama za usafirishaji kupunguakea kasi,
Serikali iweke kodi kwa magari yote yenye gas ii kuongeza pato la taifa
 
Maisha yatazidi kuwa marahisi,
Tutegemee gharama za usafirishaji kupunguakea kasi,
Serikali iweke kodi kwa magari yote yenye gas ii kuongeza pato la taifa
Waweke kodi gani tena? Si tutarudishana kule kule kwenye gharama kubwa za mafuta?
 
Usitafute huruma, toa hoja, hiyo hatari ya gesi ni ipi ambayo kwenye haya mafuta haipo?
Mkuu nikiri kwamba huu uzi wako ulinivutia na kunifanya kufuatilia hatimaye nikakutana na hayo madai kutoka kwa watu wengine wanaodai pia kuwa na uzoefu na magari ya aina hiyo na ndiyo na mimi nikaona si vibaya niyalete kwenye huu uzi ili kuulizia kama madai hayo yana ukweli. Kwa kuzingatia kwamba kwa kiasi fulani nimefaidika na huu uzi uliouanzisha sioni sababu ya kuanzisha ligi na wewe. Ahsante.
 


Wenye V6, V8 na Uber meno yote nje, hongereni DIT
Mhhh fafanua zaidi

Magari ni haya ya petrol/diesel ama ni ya gas specific?

Ikiisha mnaenda gas station zipi?.
mbona umekuja kimzaha sana!!rudi moja.
Button inakua wapi

Gauge ya gesi inasoma wapi na ya mafuta ya kawaida wapi?.
Unatofautishaje?.
Uzi bila picha[emoji55]
Dah kweli japo unafujo aueleweki ila nimejitaidi kukuelewa.
 
Back
Top Bottom