Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Mimi nililima mpunga heka kumi ukakubali kweli kweli shamba lilikua langu bwana bwana kukaa hivi napigiwa simu wasukuma wameingiza ng'ombe usiku wamekula shamba lote aisee nilidata. Alafu washenzi wale wamehonga polisi ukienda kushtaki unapigwa danadana tu nilitamani nikapige risasi ng'ombe wote. Morogoro iyo

Acha kuwaonea Wasukuma bana
 
kanyagio Naomba sana Mchango wako hapa. Najua unahitajika zaidi ya Maelezo.

Huu uzi usiishe kabla ya kuweka Mchango wako Tafadhali.
 
Naanza kwa kutoa experience yangu.

Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.

Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.

Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.

Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.

Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.

My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
WANAKUJA NA MWONGOZO WAO MKUU.
 
Aisee aisee ila nitarudi siku moja, kilimo kina changamoto sana na nikizuri
 
kanyagio Naomba sana Mchango wako hapa. Najua unahitajika zaidi ya Maelezo.

Huu uzi usiishe kabla ya kuweka Mchango wako Tafadhali.
Mkuu wanasumbua sana mkoa morogoro wamejaa naona mheshimiwa rais kaliona kaamua kuleta mkuu wa mkoa mkali ili kuweka mambo sawa ila bado nna hasira nao
 
usikate tamaa mwaya,Kilimo hakithaminiwi sababu serikali haijagundua potential ya kuwekeza kwenye kilimo,siku zitakuja ambapo serikali ita invest kwenye kilimo na kila mlimaji atanufaika nacho..
Sikati tamaa najipa Moyo najiona kama nipo mafunzoni nazidi kujifunza
 
Mie pia nilianza kilimo serious mwaka 2015...!nililima mchicha nusu eka..nikanogewa....nikalima tena na trna ..awamu ya 4kumbe chuo nachopeleka mchicha kimefungwa..nikala hasara nikauzs shamba zima kw shilingi 20000!
Nikahamia kwa tikiti..mara ya kwanza nilipata faida...ss nilikuja angukia pua kupitia hao the so called madalali.... Nijajifanya mm mjanja niwazunguke niuze mwenyew... Nilisumbuka mwez mzima nauza tikiti....
Nikaja gundua ishu ya 🍓🍓..naamini nilikua wa kwanza kbs kufanya hii mishe kiutalam zaidi hzi nikastick nazo km miaka mi3...nadhan kilimo ambacho hakina chngamoto sn ni matunda tu..nikapata ajali mbaya nikachefukwa kbs kuskia kuna strawberries...nikawa nasema naacha lakini daily unapata oda...kiukwel it pays..ila inachosha sn kupanda milimani!...nimewaachia watu waendeleze tu ...!kilimo cha Tz ni changamoto sna sna!...
 
Hao presenters waliowaambia vijana hamtumii brain vizuri naona bado wapo sahihi.

Umegundua wanaonufaika ni madalali na wafanyabiashara lakini bado umekomaa kulima tu.

Nadhani fursa hapo utakuwa umeiona ni udalali!

Au kilimo ni hobby yako nini?
 
Hao presenters waliowaambia vijana hamtumii brain vizuri naona bado wapo sahihi.

Umegundua wanaonufaika ni madalali na wafanyabiashara lakini bado umekomaa kulima tu.

Au ni hobby nini?
Baada ya kulima mara nyingi ndo nimekuja gundua wanaonufaika ni madalali na wafanyabiashara saizi nipo kwenye kilimo cha mazao ambayo soko lake ni nje ya nchi
 
Mie pia nilianza kilimo serious mwaka 2015...!nililima mchicha nusu eka..nikanogewa....nikalima tena na trna ..awamu ya 4kumbe chuo nachopeleka mchicha kimefungwa..nikala hasara nikauzs shamba zima kw shilingi 20000!
Nikahamia kwa tikiti..mara ya kwanza nilipata faida...ss nilikuja angukia pua kupitia hao the so called madalali.... Nijajifanya mm mjanja niwazunguke niuze mwenyew... Nilisumbuka mwez mzima nauza tikiti....
Nikaja gundua ishu ya 🍓🍓..naamini nilikua wa kwanza kbs kufanya hii mishe kiutalam zaidi hzi nikastick nazo km miaka mi3...nadhan kilimo ambacho hakina chngamoto sn ni matunda tu..nikapata ajali mbaya nikachefukwa kbs kuskia kuna strawberries...nikawa nasema naacha lakini daily unapata oda...kiukwel it pays..ila inachosha sn kupanda milimani!...nimewaachia watu waendeleze tu ...!kilimo cha Tz ni changamoto sna sna!...
Safi sana saiz nalima brucoils, green beans na corneflowers nayemuuzia anapeleka UAE najipanga na mm nitafute ardhi yangu nianze kusafirisha nje mwenyewe
 
Safi sana saiz nalima brucoils, green beans na corneflowers nayemuuzia anapeleka UAE najipanga na mm nitafute ardhi yangu nianze kusafirisha nje mwenyewe

Umewahi peleleza abc za kutransport hizo mambo kwenda nje mkuu😎!anywys kila la heri!
 
Umewahi peleleza abc za kutransport hizo mambo kwenda nje mkuu😎!anywys kila la heri!
Yap kupitia nayemuuzia changamoto kubwa nje wanataka mazao yenye high quality na pia wanataka msign contract ujicomit kua kila mwezi utaoeleka minimum tani ngapi. Hapo lazima uhakikishe una mashamba yako mwenyewe si chini ya ekar 20 ambayo utayapanda ktk vipindi tofauti kuhakikisha unakua na uhakika wa kusupply mzigo mwaka mzima. Hivi vi ekari 2 tatu tunavyokodi mwenye shamba hachelewi kukuzingua akachukua shamba lake
 
Sikiliza mzee baba...wanataka cheti ulichopimia udongo wako mara water content ya shamba lako sijui zao lako..wanataka uwe na vyeti sio chini ya vinne!kuvipata sasa ndo napochoka na hii nchi...yaan hizo broccoli ziwe safi zisishikwe na finyofinyo lolote....nimesahau had majina a hayo madude wanayotaka..kifupi mie nili🙌🙌..nikaishia kuwa member wa TAHA tu nikiwamisi naenda tu wanipe moyo...!lakini ni safari ndefu usikate tamaa..! Serikali hii km huna connection hata hawana muda wa kukusaidia ..nimehenyeka sn kwenye wizara husika ila wapi..labda miaka hii
 
Back
Top Bottom