Mimi niliwekeza mkuranga kama 28 mil nikachimba Visima nk, Nikaweka Wafanyakazi wawili, Siku ya kwanza tukapanda Embe ekari nane, asubuhi miche yote imeibiwa ! Niliagiza miche SUA kila mche elfu 3... Roho iliuma hatari..
Nilisikitika mno, nikaanza mboga mboga, mpunga, basi bwana si nikaanza kilimo cha simu, sikuambulia hata shilingi moja ! Nikastop...
Nikahamia kwa broilers, île nataka kuwatoa soko likaharibika hata tuliyekubaliana awe anachukua akashindwa maana naye alikua anapeleka mahala, nikafanya batch nne nikaona sasa huu Msala... Nikastop...
Ila sasa Nimerudi tena kivingine, Nimepata mikataba ya broilers tumesaini ndo nimeanza, nitakua natoa broilers elfu moja kila Wiki, nilichojifunza Ni kutokukata tamaa na kufanyia kazi zile changamoto zilizokukuta, usiache.. Jitafakari anza tena !