Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,576
Mashamba yako milimanistrawberries unapandeje milima
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mashamba yako milimanistrawberries unapandeje milima
Kama kulima ntalima na bangi,najua siwezi pata hasaraKilimo na Ufugaji ni vitu ambavyo nitavikwepa daily. Bora kuwa mtu wa kati hapo faida lazima uipate tu.
Kilimo cha bangi hakiwezi kukuangusha
Nyie ndio mnalima strawberry Sumbawanga? Hizi nasikia soko ni changamoto sana
Naona ujanielewa ,sokoni bila ubunifu utaishia Julia hivyo hivyo,wakati umefika mjini unahangaika na masoko,hayo matikiti ungetafuta sehemu kama tatu zilizochangamka,unauza moja moja,ata kama mtu anataka kipandebl anapewa,ndani ya wiki mzigo ungekua umekwisha ,ungekua na ela nzuri Sana,ndo maana madalali walikupiga kote kote,inaonekana market strategy Hun kabisa,zeroMtu katua na fuso Dodoma unamshauri eti awe mbunifu afungue goli auze kwa kukata kata vipande hizo si ndo fursa za makaratasi hahahaha
Apo kwenye soko ata mimi nashangaaga Sana ,haswa biashara za vyakula,Mimi nashangaa wanaolalamia soko..mm mpka ss napigiwaga simu wanataka berries nawaambia sihusiki nazo tena..but mm nilijitangaza vilivyo!
Ukiwa na ilo fuso lako la tikiti tena,niambie ,sitaitaji ata kumi yako,ntakuonyesha namna ya kuuza,maana ishu za masoko zinakupiga chenga,huwezi ukatujua Kula kitu ndo maana watu wanaajiri marker managerMtu katua na fuso Dodoma unamshauri eti awe mbunifu afungue goli auze kwa kukata kata vipande hizo si ndo fursa za makaratasi hahahaha
Inaonekana walidukua mpunga wako,wenyeji.Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
Hongeraa kwa kuipenda familiaNilipiga heka za Mahindi 30.za.mahindi karibu 8m. huko Morogoro.kabla ya kuvuna Ngombe wakapita nikaambulia gunia 30.maana yake kila eka gunia moja.
nikarudia tena mvua ikazingua ktk eka 20 nikapata gunia 3.nikarudisha home.tumekula ugali mwaka mzima.
Nikajaribu matikiti eka 4 .kabla ya kuiva yakawa yanapasuka pasuka.sikuuza kabisa .sema tulikula matunda home na wanangu.
Nikajaribu matango. eka 2.hayo yakakubali.na yanakomaa ndani ya mida mgupi sana .nikachelewa kuvuna.nilikiwa safari ya kikazi.nikawambia madogo wasubiri nirudi wasivune nilihofia kupigwa.hivyo yakaiva yakawa na mekundu hivi .kumpeleka bos shamba ilil akanunue,akaishia kuniitukana eti nimemsumbua na kumpotezea muda wake wakati.mzigo wenyeqe hauuzilki
Nilijaribu kufuga kuku chotara.hao walikubali sana.sema wakiwa na miezi mitano wakapata ugonjwa wa ajabu ghafla.asubuhi tunaamka tinaona wanasinzia na kukohoa. walikufa kwa wingi ndani ya muda mfupi.ndani siku 4 kuku300 walikufa nikabaki na kama kuku 33.ndiyo naokota mayai ya kula na familia.
Uhalisia upo hiviNaona ujanielewa ,sokoni bila ubunifu utaishia Julia hivyo hivyo,wakati umefika mjini unahangaika na masoko,hayo matikiti ungetafuta sehemu kama tatu zilizochangamka,unauza moja moja,ata kama mtu anataka kipandebl anapewa,ndani ya wiki mzigo ungekua umekwisha ,ungekua na ela nzuri Sana,ndo maana madalali walikupiga kote kote,inaonekana market strategy Hun kabisa,zero
Cc manengeloMimi nililima mpunga heka kumi ukakubali kweli kweli shamba lilikua langu bwana bwana kukaa hivi napigiwa simu wasukuma wameingiza ng'ombe usiku wamekula shamba lote aisee nilidata. Alafu washenzi wale wamehonga polisi ukienda kushtaki unapigwa danadana tu nilitamani nikapige risasi ng'ombe wote. Morogoro iyo
Nyanya nasikia inasoko mwezi december na january kipindi cha mvua sema huko shambani ndio changamoto manake kila mtu anakua amekimbia inabidi uwe kama komandoo huko porini ndio utoboeKilimo cha nyanya kimenifanya nikakata tamaa maana kilichukua mpaka senti yangu ya mwisho
unalima kibishooHakuna aliyefanikiwa kwa kilimo cha cm make sure 90% ya muda wako upo shamba na ujikane na anasa zote za dunia. Inafikia kipindi hata kwenda shamban ukiwa umebeba mkononi maji ya kunywa makubwa unaonekana kama unafanya anasa hahahaha
😁 😁 😁 😁 😁 😁 😁 🏃♂️🏃♂️🏃♂️yani nilitamani niutelekeze mzingo..ila sikua na jinsi nikauza hivyo hivyo kwa hasara..
Ufuta mvua zikienda vizuri unatoka ingawa nalo wakati flani soko linazingua Ila alizeti uhakikaHahaaaa..ngoja nicheke tu..mwezi wa8 nililima bamia kama heka na nusu..nimezipiga vzr tu..msimu wa mavuno umefika...siku napeleka mzigo sokoni nikakutana na bamia zimeteremshwa kama mvua kipindi cha nuhu..bei iko chini..yani nilitamani niutelekeze mzingo..ila sikua na jinsi nikauza hivyo hivyo kwa hasara..
Nimevuna kama mara mbili..imebidi nmeachie dogo avune atafute hata hela ya kujikimu akisubiri vyuo vifunguliwe..
Kimsingi kilimo kina changamoto sana..kama sio shambani basi sokoni.
Ila siachi kulima..nmekodi shamba heka 10 najipanga kulima ufuta na alizeti.
GOD IS GOOD.
Hapo mwisho ndio msumari ulipo. Madalali wa kibongo ni hovyo kabisa halafu wanajifanyaga kama hawana shida na madharau kibao pindi wanapokagua bidhaa ya mkulima. Ipo siku mimi itatwanga mtu makofi mbele ya polisi.Naanza kwa kutoa experience yangu.
Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.
Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.
Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.
Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.
Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.
My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
Ukulima ki-bongo bongo ni kujitafutia umaskini tu kwako na kizazi chako.
[emoji38][emoji38]aseeehMi niliingia ktk kilimo kwa partnership na ndugu zng wa huko bush ili km ikibuma basi maumivu yawe ½!
Msimu wa kwanza tulilima cabbage kwa kumwagilia! Niliwatumia ndugu zangu wa huko shamba kama nguvu kazi! Mimi nikatoa fund kwa ajili ya pembejeo!Cabbage ikatupiga hatari! Ilipigwa na ugonjwa, ikazaa chini ya Makadirio! Kidogo iliyopatikana tuliuza pale pale Kijijini!
Changamoto!
1. Mtu tuliemuamini km mtaalamu wa cabbage hakua na utaalamu husika na hivo alitupeleka chaka ktk maeneo km mbolea na sumu za wadudu waharibifu!
2. Tulilima kwa kutumia maji ya mto, kutokana na wingi wa wakulima, maji haya yalikuwa na zamu lini na lini wamwagilie akina nani. Ilifika wakati ikifika zamu yk let's say Juma5, mto hauna Maji!
Suluhisho!
Tumechimba kisima shambani. Pump tunayo!
Msimu huu tumelima MAHINDI Gobo gobo! Kila kitu kimeenda sawa! Yamezaa vizuri sana!
Hofu:
Tuna hofu na bei ya sokoni ya MAHINDI ya kuchoma!
Plan B:
Km MAHINDI ya Gobo gobo hayatakuwa na bei nzuri, tutayaacha yakauke ili tuvune MAHINDI ya Ugali! Kwa sasa sokoni bei ya ipo vizuri. Kijijini kwa sasa debe ni 20k!