Biashara ya mazao ya kilimo nayo inachangamoto zake;na source ya changamoto zote za kilimo zinasababishwa na sera mbaya ya kilimo ya kitaifa;na Pia hasa maamuzi mabaya ya viongozi watu!Ngoja nikupe experience yangu ndogo ya kuwa middleman kwenye mazao,Mwaka 2017 niliwekeza 7M kwenye kununua Mahindi kwa wakulima na lango lilikuwa ni kuyahifadhi na kuja kuyaudha baadae kwa faida hvyo nikatafuta sehemu ya storage na kulipia,Nika arrange transport kuyatoa shambani mpaka storage na vibarua wa kupakia na kupakua pamoja na gharama nyingine nk.;and offcourse kila kitu kikawa ok.And keep in mind kwamba faida unaipiga kwa gunia kulingana na kilo hvyo roughly katika mahesabu yangu gharama jumla ya kila gunia ilikuwa 55,000.During storage kuna gharama zake za kuya maintain na market value ya kugunia ilikuwa 70,000 ambapo kama ningeuza bei hii na kutoa gharama nyingine at least kila gunia nisingekosa chini ya 8'000 faida,after 2 months nikaona soko bei inaanza ku shake baada ya serikali kuzuia mahindi yasiuzwe nje;My friend 😆😆😆;kwenye soko la mazao saa moja linaweza kukupa ukichaa manake bei ya kilo asubuhi inaweza isiwe bei ya jion,gunia likashuka mpaka 52'000 na cost za kupambana na wadudu zikaaanza kupaa,baada ya 3 weeks gunia lilikuwa linaitafuta 40 na kitu na hapo sijamlipa dalali wala gharama nyingine plus energy lost sababu nilikuwa napambana nayo day and night;Nilichofanya nilimpigia simu dalali wa kuniuzia,nikatafuta na Fuso la kwenda kuyachukua storage nikamwagiza ndugu yangu akayasimamie kuuza sababu personally sikutaka kushuhudia matokeo ya hasara kwa macho yangu;nilikuwa very disappointed mnoo na kiukweli niliangukia Pua!Angalia wafanyabiashara wengine overnight walijikuta wanaamka maskini kutokana na serikali,hvyo bila serikali kuweka mipango bora ya kilimo maangamiz ya watu kwenye kilimo hayataisha.