Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu uzi hauna future nzuri kwa vijana hasa kwenye tasnia ya kilimo
Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
Hyo kawaida kabisa , tena bila hata mboleaHekari moja kwa 250,000/- mbona hii gharama ni kubwa sana?! Ulilima kwa mashine na ukaweka mbolea pia?
Halafu kuna pumbavu moja linaitwa Mauki linatuita "wasanii"Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
xHalafu kuna pumbavu moja linaitwa Mauki linatuita "wasanii"
Naanza kwa kutoa experience yangu.
Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.
Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.
Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.
Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.
Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.
My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
Picha wanazotumia motivational speakers kuturaghai!
Mkuu kwa kukadilia ulitumia sh nhp nataka niingie field ekari 3.Mwaka jana nimelima eka tatu za mpunga, mnvua ikagoma mwanzoni ikaja mwishoni, nikapata matumaini, ulivoanza kukauka ikanyesha mvua ya mawe,ikapukutisha wote uliokuwa umekauka.
Niliambulia gunia 13, sijaziuza nasubiri bei ipande Sijakata tamaa, mwaka huu nalima tena. Mungu atie baraka zake
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Halafu kuna pumbavu moja linaitwa Mauki linatuita "wasanii"
Karibuni Mbarali ila huku ujipange kifedha kama unataka mashamba y uhakika kuvuna ata mvua zikisuasua bt kwa mashamba ya kukodi 200k lazima umwombe Mungu ucku na mchana mvua iwe ya wastanNendeni Same kuna kilimo cha mpunga cha umwagiliaji uhakika wa mazao mkubwa na mpunga hauharibiki unaweka stoo unasubiria bei ipande.
Mkuu upo ubaruku?Karibuni Mbarali ila huku ujipange kifedha kama unataka mashamba y uhakika kuvuna ata mvua zikisuasua bt kwa mashamba ya kukodi 200k lazima umwombe Mungu ucku na mchana mvua iwe ya wastan
Nalimia kapunga mashamb ya nje ya mradi wa mwekezajiMkuu upo ubaruku?