Tulioishi Dodoma miaka ya 90's mpaka miaka ya 2000 tukutane hapa tujikumbushe

Kitambo sana Dodoma. Toka Makole Primary nakatisha kiwanja cha Ndege kati navuka naenda twisheni kwa Mwal. Kikanya hapo K/Ndege shule ya msingi. Area C walikuwa wanakaa watoto wa matajiri, enzi hizo Area D ndo inaanza chipukia. Dah nimekumbuka mengi sana Dodoma. Matajiri walikuwa wakina Mzee Chove wa mabasi ya Urafiki. Bunge enzi hizo lipo mjini huku karibu na Hospitali ya General. Kwa leo ngoja niishie hapo.
 
kikanya na paper zake za 50 kwa mtihani kila weeken kama hakutajirika basi tena
 
Daaah dodoma ile ya shule ya Mazengo, Club NK, Ushuani area C tulikua tunaenda kutembea for no reason, Matajiri walikuwa wananunua viwanja area d Chan'gombe ilikuwa ya watukutu, kisasa ilikuwa vichaka tu, hakuna ilazo makuru ndio mapori kabisa hatugusi
 
Kamji kalikuwa kadogo mno.. mji unaishia maili mbili, kikuyu, kizota, makole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na sisi wa Bahi na wa Mpwapwa tu comment wapi? Au ndio kusema sisi hatukukaa Dodoma?
 
DODOMA YA VUMBIIIIII TU PUMBAFU.
Acha hizo,huwezi kulinganisha Dodoma ya miaka hiyo na sasa,ambapo barabara nyingi zina lami na maeneo mengi ni makazi ya watu,sasa vumbi linatoka wapi,sikatai msimu wa baridi kuna vumbi kama ilivyo Morogoro na mikoa mingine kwa sababu ya upepo.Ushauri ninaotoa kwa authorities,mvua zinakuja wahamasishe upandaji wa miti mkoa mzima hasa mijini kwani msimu wa mvua ni karibu miezi 5 hivyo unatosha sana kuotesha miti...
 
Daah Dodoma yangu, enzi hizo wagogo walibeba mzegamzega kupeleka mkaa na nyanya mjini.

Kingcross, urafiki, mshikamano na zafanana zinapita Iringa road kuelekea huko Bihawana hadi Iringa.
 
Daah Dodoma yangu, enzi hizo wagogo walibeba mzegamzega kupeleka mkaa na nyanya mjini.

Kingcross, urafiki, mshikamano na zafanana zinapita Iringa road kuelekea huko Bihawana hadi Iringa.
Mnzega daaaah unakuta anavyotembea linanesa nesa linatoa kasauti Fulani hivii[emoji28][emoji28]
 
Mnzega daaaah unakuta anavyotembea linanesa nesa linatoa kasauti Fulani hivii[emoji28][emoji28]
Mtu anatembea kwa kutroti kidogo, ukichoka bega hili unahamishia bega jingine.

Namkumbuka mzee Chakula Bora alituletea sana maji kipindi cha ukame na shida ya maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…