Mkuu, najua umeweka ukingo wa madarasa kwenye kuchangia huu Uzi lakini kwa ujumla maisha ya shule ni yenye viroja sana. Samahani kama nitakuudhi kwa hili.
Kuna mwanangu mmoja nilifahamiana naye kidato cha ii, huyu jamaa alikuwa kiboko. Darasa zima rafiki yake alikuwa ni mimi tu, mimi nilikuwa na Afro ila lake lilikuwa kubwa zaidi. Alikuwa na mwili mkubwa ule ambao juu mnene halafu kwa chini wa kawaida A.K.A "carrot body". Binafsi, ndani ya darasa nilikuwa natafsiriwa kama kauzu ila kwa huyu mwana nilisubiri. Darasani alikuwa anaingia mda wowote anaojisikia, hajali kuna mwalimu anafundisha ama la yeye anaingia tu. Na katika ukaaji wa dawati na meza ulivyopangwa na mwalimu wa darasa mwanamke anakaa katikati kulia na kushoto wanakaa wanaume.
Basi tuliwekwa na mwanamke mmoja alikuwa ni miongoni mwa pini za darasa. Laaa haulaa! Binti hakuwa anatufahamu vizuri bhana akawa anatuletea mapozi, basi jamaa anamwambia yule demu " wewe ni mbovu tu siku nyengine unakuja hapa unanukia u' chimpanzee u' chimpanzee unatupa mafua tu. Kuna day huyo "she" alienda toi ile "she" anarudi kukaa kwenye dawati lake mwana ananishtua yupo " Oi little Afro, mbona kama navuta hewa ya mmavi mmavi hapa, mi nikamjibu; sijui nini kimetokea. Jamaa akamwangalia yule demu kisha akasema kumbe huyu demu ametoka chooni ndomana tunasikia harafu ya mmavi mmavi hapa"
Ila jamaa alikuwa mkali wa math balaa.