Tuliokurupukia kuanzisha biashara baadaye tukajua hatujui tukutane hapa

Nyamwage

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
712
Reaction score
1,748
Nilipojua kua sijui yangu ilikua katika biashara ya nafaka

Ilikua mwaka 2011 baada ya kufanya vibarua vya hapa na pale nikawa nimesave pesa kiasi cha tsh 750,000 nilikua na shauku sana ya kujiingiza katika biashara yoyote ya halali ili niachane na vibarua vya kutokua na uhakika wa kukipata kila siku

Sasa katika tafuta tafuta ushauri nikakutana na jamaa mmoja zamani alikua anafanya biashara ya nafaka lakini aliacha kwa kufilisika aliwekewa dawa za usingizi kwenye pombe na wahuni wakatoroka na pesa zake zote

basi jamaa hakuwa mchoyo akanipa muongozo wote wa jinsigani gani alikua anafata mahindi huko porini akanipa na mawasiliano ya rafiki yake mmoja ni mkazi wa hicho kijiji pale ambapo jamaa alipokua anafikia analala hapo kwa huyo jamaa

jamaa anafamilia mke na watoto wengi kiasi huyu mshikaji akaniambia kua kule wanahitaji mboga tu sababu ugali wanao basi nikaenda soko kuu pale mwanza nikanunua dagaa visado viwili nyanya na vitunguu

nikanunua na mifuko ile ya debe 6 na kamba na sindano ya kushonea magunia akaniambia pia nitafute debe la plastic na kisado nivichemshie maji ya moto alafu vikiisha pata moto nijaze mchanga huku naushindilia ili hilo debe na kisado vitanuke ili niweze kupata mahindi mengi kutoka kwa wanakijiji

alafu inahitajika niwe na chenji noti ndogo ndogo ili iwe rahisi maana kule nako chenji ni tabu nikaenda bank kuu pale mwanza karibu na keep left nikawaambia shida yangu wakachukua pesa zangu 750,000 wakaziweka katika mashine ya kuhakiki noti kama ni bandia

zote zilikua safi basi wakanipa chenji za vibunda vipyaaa vya 2,000 na 1,000 na 500 bila vikwazo vyovyote basi asubuhi nikaenda stendi ya mabasi nyegezi nikapanda vi HIACE vya kwenda MISUNGWI MISASI
nikashuka misasi kuna baiskeli za kwenda huko porini kijijini panaitwa NKUNGUHUMULU nauli ya baiskeli ni 500
ni kipande kirefu aisee wasukuma wanapiga pedeli baiskeli inapanda mlima kama inatelemka unapigwa na upepo tu kama umepanda bodaboda

nilifika pale kijijini jamaa mwenyeji akanipokea nikamuelezea basi akawajulisha wanakijiji kuwa kwake kuna mnunuzi wa mahindi basi wana kijiji wakaanza kuniletea mahindi mwenye kisado mwenye debe moja mwenye gunia sawa ilinichukua kama siku 3 kukamilisha gunia 21

nikawa nimebakiwa na akiba ya 80,000 nikasema hapa inatosha sasa nirudi maana mjini nimeeacha mahindi gunia wanauziwa 38,000 mpaka 40,000 kwa bei ya jumla na mimi nimemenunua kila gunia 27,000 mpaka 28,000 nikawa napiga hesabu za kwenda kukunja 200,000 kama faida

sasa kipengele kilikua usafiri kumbe kule porini fuso haiji kama hauna gunia 100 maana wale wenye fuso wanabeba kila gunia moja kwa bei ya 1,000 basi nilisota huko porini maji ya kunywa yenyewe wanachota kwenye bwawa ambalo wanako kunywa maji ng'ombe na punda wanyeji wenyewe wanayatwanga hawaoni tatizo mimi ndio siwezi yaani maji ukiyaangalia hunywi mpaka uangalie juu ndio unywe

nimekaa kama siku sita nika mpigia tena jamaa alie nielekeza, kaka vipi natokaje huku jamaa akawapigia wadau wenzake wa zamani kama wapo vijiji jirani ili anionganishe nao ili fuso lije lituchukue wadau wanasema bado mzigo wao hawaja maliza wako mjini bado

dah nimeka jamaa kampigia mdau mwingine na yeye akawa ana gunia 25 na yeye kakwama porini
basi kuna fuso moja inaitwa MAMBO YA CHINGA ilikua imeleta wamachinga vijijini sasa wanatafuta mzigo wa chap wapeleke mjini ili jioni wawarudie machinga wao hio ndio ikawa ponapona yangu ya kutoka porini

tukapakia mzigo tukafika sehemu kuna watu wa ushuru tukalipa ushuru kila gunia moja 1,000 jumla gunia moja likawa limesimamia 30,000 tumeenda mpaka sehemu moja inaitwa bugarika kuna masine ya kuuza mahindi nikapiga mzigo wangu pale kwa kua jamaa mwenyeji alikua ana kijiwe pale basi mzigo nikawa naulaza bure

tatizo likawa hapa katikati kipindi nilipokua polini kumbe kuna watu wenye mitaji mikubwa wamemwaga mahindi pale mwanza kila mtu ana mahindi basi na bei ikaanza ku drop ikashuka mpaka 34,000 kwa kila gunia da nikazidi kuvurugwa nikasemaa niki kaa sana hapa mahindi yanaweza yakashuka zaidi nikapata hasara basi mimi nikashusha bei maradufu nikayauza 32,000 mengine nikawakopesha wanao uza lejaleja lakini walinilipa kila walipo maliza mzigo

dah nikaja piga mahesabu faida niliyo pata ni 40,000 na hela yenyewe ya faida nimeshaila kuangalia mkononi mtaji wangu umebaki kiasi gani najikuta nina 690,000 kati ya 750,000 kwahio nikawa nimepoteza muda na pesa yangu kama 60,000 imepungua wanaosema biashara ni mtaji hawakukosea kipindi hicho ningekua nina mtaji kama 3,500,000 hata kama kwa kila gunia ningekua napata faida ya 2,000 bado ningekua na faida nzuri tu

BIASHARA NI MTAJI

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu ila ulijifunza mambo mengi katika biashara, biashara za mtaji mdogo sio rahisi kutoboa hapa bongo.
 
Ulikata tamaa mapema. Wakati mwingi biashara ni timing na kuwa na habari sahihi. Na kwako kuna kitu kimoja ulikosea.

Baada ya kupata habari zote kwa mshikaji ungeenda kwanza huko kijijini ili kupata habari zote muhimu hasa hiyo ishu ya usafiri kwa sababu naona ndiyo ilikuwa karibu ikuharibie kila kitu...

Kwa hakika hukupoteza pesa nyingi kiasi kile na kwa vile sasa ulikuwa na habari sahihi ilikuwa imebakia kufanya tu timing nzuri ya soko.

Mi nilishaunguza milioni 5 nzima tena kwa mwezi mmoja tu. Yaani hata senti sikupata lakini nilijifunza sana na nikarudia tena na mambo hayakuwa kama mwanzo; na ile milioni 5 iliyopotea nikairudisha.

Biashara kusema kweli simuliwa tu au soma humu mitandaoni lakini ukiingia lab kwenye practical ni shughuli pevu! Na kwa hapa Bongo kwa wenye mitaji midogo mazingira siyo rafiki!
 
Biashara na ujasirimali kiujumla ni safari ya mafunzo na mafanikio. Mafunzo ni sehemu ambazo unashindwa, unakosea, unapata hasara. Inabidi kufanya tathmini hili linapotokea ili mara zijazo uwe na somo litalokusaidia mbeleni hata kama ni vitu kama uvumilivu na bidii.

Nishawahi fanya biashara zaidi ya 20 hadi sasa na ni biashara 5 tu zilipata faida na mbili tu zilizoniingizia zaidi ya milioni 100. Kila moja ilikuwa na funzo katika hatua moja au nyingine. Naamini nisingefika hapa bila kupitia biashara ambazo zilifeli.
 
hongera sana mkuu ila navyowajua wabongo wakisoma comment yako hapa kitu pekee watachokielewa ni "zilizoniingizia zaidi ya milioni 100"[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mkuu biashara simuliwa tu ili ukiingia ndani unajifunza zaidi.Ujumbe murua huu
 
hongera , ila

1. weka aya kwenye stori, nimesoma mistari yote kwa 'mouse' ili nisije ruka

2. hongera kwa uthubutu

3. motiveshen spika wamekalia kilimo cha makaratasi, ila kuna variables kibao ukiwa field ngumu kutabirika
 
Sasa si bora wewe umepata hasara ya 60,000 mzee

Kuna muda michongo inakugomea kila uki force chenga tu unajikuta unazidi kupoteza pesa zako kwa ile dhana ya kusema "biashara ni uvumilivu" siku unakuja kustuka tayari ume damage pesa nyingi na huwezi kuzi recover kwa muda mfupi

Huwa nasemaga siku zote attempt ya kuanza biashara kwasababu umemuona mtu fulani aliyefanya hiyo kazi imemfaidisha inakuwa ni stupid risk

Ndo mwisho wa siku watu wanapokuja kufeli kwenye biashara walizoiga kutokana na mafanikio waliyoyaona kwa mtu anayefanya hiyo kazi wanaanza kuitana fulani anatumia dawa kwenye biashara yake kwasababu yeye anafanya na hapati faida ambayo alikuwa akiifikiria
 
Ni kweli 'biashara ni mtaji'
Pia sio uongo "biashara sio mtaji''

Mwenye mtaji mkubwa akifanya biashara yoyote atapata faida kubwa, sababu inajulikana.
Mwenye mtaji mdogo sio kila biashara atayo fanya atapata faida kubwa, hapa lazima achague biashara husika ndo atapata faida kubwa.

Mfano kuna mshakaji wangu alikuwa na biashara yake mtaji ni 70k - 100k anauza tu sigara, condom, pipi, fresh, big G, anauzia nje ya club anapanga bidhaa zake kwenye meza katulia na kiti chake. Condom Dume bukubuku na rough rider 4000, sigara tatu buku,
pipi ivory, big G, na fresh, vitatu jero.

Pia kuna casino pembeni watu wakiliwa hela wanatoka nje wanavuta sigara kupunguza hasira, wengine wakizinguana huko ni kuja kununua tu sigara wanawasha, wengine wanaondoka na malaya wanachukua condom, hapo kila hela anayouza faida ni nusu yake kwa siku alikuwa anauza 80k - 120k siku za kazi ni nne wastani faida 50k kwa siku. Hapo ndo nikagundua 'biashara sio mtaji mkubwa' pia sio uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…