Tuliokurupukia kuanzisha biashara baadaye tukajua hatujui tukutane hapa

Nilipomaliza chuo wakati nasubir ajira nikaona nihangaike kutafuta ela za vocha nikaamua nianze biashara ya kuuza juis fresh na uhitaji ulikuwa mkubwa na kwa siku nilikuwa nauza hta glass Mia kwa masaa kadhaa tu Ila matunda yalikuwa ni ya kuagiza dar nakumbuka nikaagiza mzigo wa kutosha mzigo unafika tanesco wakakta umeme siku nne ndo unarudi ela iliniuma balaa japo haikuwa nyingi Ila kwa kipato changu enzizile nilitamni kulia lkn nikaendlea na Mambo yakawa sawa Hadi nilipoamua kufungua biashara nyingine kubwa zaidi....


Biashara changamoto Sana hasara zipo za kutosha tu Ila muhimu kufanya research kabla hujafungua biashara
 
Kumbe mrembo unaweza nifundisha mambo ya busines...naja pm unioe maujanja
 
Wewe mwenyewe uliamua kufeli mwenyewe ulishindwa kutumia mandala wa umeme wa Tanesco kama Generator, solar power system, gas n.k?
Maana kama kubreda matunda na kuyafreeze lazima ungefaulu.
 
Wewe mwenyewe uliamua kufeli mwenyewe ulishindwa kutumia mandala wa umeme wa Tanesco kama Generator, solar power system, gas n.k?
Maana kama kubreda matunda na kuyafreeze lazima ungefaulu.
Ilikuwa ni nyumbn hatuna generator alafu nilikuwa natengeneza siku hiyohiyo kwaiyo nilikuwa siwez kulaza ili isipungue ladha...
 
Biashara inachangamoto nyingi sana ambazo lazima upite ujifunze all in all Mimi Huwa najinenea,"Nikiweka mkono wangu hakuna kitu kufa Yani ni mwendo wa kusonga mbele Tu"
All in all there are a lot of factors to consider before initiating any business.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa moyo wa uthubutu,inaonesha wazi una nia,shida ilikuwa pale ulipotegemea kikubwa,labda nikupe ushuhuda tu labda unaweza kukutia nguvu,kuna jamaa mmoja niko nae ofisini hapa,yeye aliamua kuanzisha baishara ya chipsi kwa kuwa aliona mafanikio ya mwenzie ambae kasimamia biashara yake mpaka akawa nikiwa kufungua vibanda zaidi ya 50,sasa kwa Mara ya kwanza akafungua sehemu yake ya kuuzia chipsi akianza na mtaji wa 1,000,000 kwa kuwa hakuwa na usimamizi mzuri biashara alifunga baada ya wiki mbili,akaja kufungua tena mwaka jana akaamua kutenga 3M kama mtaji akaanzisha upya,kweli ikaanza kwenda vizuri kwa sababu alikuwa anapata mda wa kwenda kutizama biashara yake na akawa anapambana kwelikweli shida ikaja kutokea tu pale alipohamishwa kituo kwa mda wa mwezi mmoja hapo ndio na biashara ikaharibika kabisa,akapata hasara ya pesa yote hiyo maana hata vitu vingine viliharibika ikabidi havitupe,mwaka huu mwezi wa nne akafungua tena sasa hiki kipindi akaweka 6M akijua kwamba akimuweka ndugu atasimamia vizuri na mambo yataenda,Yaani mauzo aliyokuwa analetewa hesabu ikawa inamlazimu awe anaongezea hela kwa ajili ya maemezi maana pesa iliyokuwa inakuja ikawa haitoshi hata kwa maemezi ya kesho yake,biashara imedumu kwa mwezi mmoja tu akafunga maana alikuja kupiga hesabu akajikuta amepata hasara kubwa mno,akaamua kufunga tena,Yaani alichoambulia ni vitu tu alivyo kula ameanzia biashara basi
 
Kiukweli biashara inataka uwepo mwenyewe kuisimamia. Yaani haina tofauti na malezi ya mtoto. Ikishakomaa na kukua una maamuzi ya kuiuza au kuipanua.
Binafsi nipo kwenye biashara ya Audio production na kwa kipindi cha miaka minne nimefanikiwa kupata ujuzi na uzoefu mkubwa sana aisee. Isingekuwa ubishi wangu hii biashara ningeshaifunga muda sana kwa sababu nilianza huku ninatafuta uzoefu kazini na nilikuwa na mtaji hafifu(kama 7m hivi) ambayo nilikopa kwa rafiki yangu japokuwa mpaka leo sijawahi kuirudisha. Ila kipindi ambacho unataka kukata tamaa hapo ndipo mafanikio yalipo kiukweli. Mpaka kufikia mwaka jana ndio nilikuja kupata suluhisho la kuifanya biashara ya muziki kuwa profitable na effective baada ya kuunda mfumo madhubuti wa kuintegrate huduma ya production studio na biashara ya muziki.
Itabidi niandae thread yake ili wengine wajifunze wasije kurudia makosa kwa maana hii biashara ni ngumu sana na watu wengi huja kichwa kichwa sana.
 

Sasa hapo umemtia moyo au umemkatisha tamaa kabisa 😂
 
Nimempa ndani wa mtu ambae pamoja na kupoteza pesa nyingi ili bado hakati tamaa

Mtu ambayale hajakata tamaa ila anaendelea kupoteza pesa tu. Doesn't sound like encouraging to me.

In business, one has to know when to call it quits. Lazima ujue this is not working na uanze kuangalia upande mwingine. Kupoteza sana pesa haimaanishi ipo siku utakuja fanikiwa unaweza poteza milele zote. Uvumilivu una kiasi.
 
Yaani wewe hata sikuhurumii aisee. Afadhali tu yaani hali ilikuwa kama ilivyokuwa kha!

Halafu unavyosimulia masikini. Kama nakuona usiku umelala unawaza mbona watu hawafi? Hii Korona vipi? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Hahahah..wewe jamaa huna akili.
 
Hqpo kwenye wasukuma kupiga pedeli nimecheka sana [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kwamba baiskel inapanda milima kama inashuka ...unapigwa upepo km upo kwenye boda...daaah umenikumbusha mbali sana
 
Pole sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…