Mtu Asiyejulikana
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 2,254
- 5,161
Watanzania wengi kwa ukosefu wa Elimu bora na Ufahamu jumuifu walijikuta wanashabikia sana Vita ya Urusi na Ukraine. Wengi sana wakichukua pande kama wanavyoshabikia Simba na Yanga.
Na wengi walikuwa hawaelewi kwa nini NATO au USA haiingizi miguu yake. Kwa akili ile ile ya kishabiki wakimsifu either putin au rais wa ukraine.
Na wakaenda mbali kusema NATO wanaiogopa Urusi au pengine Urussi inaiogopa NATO. maneno mengi na ubishani vijiweni na kwenye mitandao usio na tija.
Leo mnaona Watawala wanatumia Vita hivi kuwaumiza wananchi zaidi. Kodi zinachomekewa humo ndani kwa ndani ukiuliza utaambiwa ni Vita ya Urusi Ukraine.
Athari za Vita hivyo zipo, lakini kuna wahuni ambao wameamua kwa makusudi to swim with the current. Tutegemee ufisaidi mkubwa sana kipindi hiki hasa kwa nchi zetu za kiafrika nyingi. Zila chache kuna marais wanapambana kupunguza makali ya maumivu kwa wananchi wao.
Na kwa zile ambazo zina bahati mbaya Marais wanatumia nafasi hiyo kuwa nyonya damu wananchi wao. Sasa kila kitu kimepanda. Hadi pipi zimepanda bei. Vita vya Urusi Ukraine.
Je, tuendelee kushabikia kama tunavyozishabikia Manchester na Liverpool au sasa tuanze kuangalia tuna viongozi wa namna gani?