Huyu dada nilianzaga kumuona kwenye FEMINA magazine kisha FEMA kama mhariri msaidizi huku CHIKU LWENO akiwa mhariri mkuu kama sijakosea. Japo sikuelewa yaliendaje yeye na yule AMILIBUS(nadhani nimekosea kuliandika) na LYDIA. baadaye akahamia kwenye HAKI ELIMU. kile kipindi kilikuwa kizuri alikuwa anakwenda mpaka vijijini tena nakumbuka kipindi kimoja alielezea mtoto aliye anguka darasani kwa mapepo.
baadaye kwenye kipindi cha wanawake cha itv nikamuona kwenye show ile huku akiwa na asasi yake inayoitwa GIRL INNITIATIVE.
HUYU DADA MIMI NIMEMPENDA JAPOKUWA MKUBWA KWANGU. HUWA NIKISIKIA SHOW YAKE NTAFANYA YOTE ILI NISIIOKOSE.
MUNGU AMTANGULIE KATIKA KILA HATUA APIGAYO